Hosea aligeuzia Bunge kibao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hosea aligeuzia Bunge kibao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shapu, Aug 6, 2009.

 1. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Nimesoma kipande hiki cha habari Raia mwema.. Naomba tukijadili.

  =========================

  Katika hatua nyingine, taarifa zinasema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inazichunguza kamati kadhaa za Bunge, ikiwa ni pamoja na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ambayo ilihusika kuibua sakata la Richmond na kuiumbua TAKUKURU yenyewe.

  Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM), William Shelukindo na makamu wake, Dk. Harrison Mwakyembe,
  ilipendekeza kuchukuliwa hatua kwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Edward Hosea, na wasaidizi wake kutokana na kushindwa kubaini udhaifu mkubwa katika sakata la Richmond.

  Kamati hiyo iliituhumu TAKUKURU kuisafisha kampuni ya Richmond iliyopaswa kuzalisha umeme wa dharura, na ikapendekeza hatua zichukuliwe dhidi ya watendaji waliohusika katika mchakato wa kutoa zabuni kwa kampuni hiyo.

  Hatua ya sasa ya TAKUKURU kuchunguza kamati za Bunge inadaiwa ni ya kulenga kupunguza makali ya Bunge, kupitia kwa wabunge hao hususan kipindi hiki ambacho Bunge linaonekana kuwa moja ya taasisi zinazoungwa mkono na kubeba matumaini ya Watanzania wengi.

  Kwa mujibu wa habari zilizotufikia, TAKUKURU wamejipanga kutumia fursa za kisheria walizonazo kufanikisha mpango huo ikiwa ni sehemu ya kujibu mapigo ya wabunge, na mbali na Kamati ya Shelukindo iliyoshupalia Richmond, nyingine ni za Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

  Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa mambo mbalimbali yameanza kuchunguzwa katika kamati hizo ikiwa ni
  pamoja na safari za wajumbe wa kamati hizo kwenye maeneo mbalimbali ya nchi na hususan malipo ya posho, yanayodaiwa kuwa yanalipwa zaidi ya mara moja, kinyume cha taratibu.

  Raia Mwema ilizungumza na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila kuhusu suala hilo ana akasema ya kuwa hajapewa taarifa zozote kuhusu kuwapo kwa uchunguzi huo, lakini akaongeza ya kuwa TAKUKURU wanayo mamlaka kisheria kuendesha uchunguzi bila kutoa taarifa rasmi.

  Wakati wa uchunguzi wa mchakato ulioipa zabuni ya kufua umeme wa dharura Richmond, TAKUKURU, kupitia kwa Mkurugenzi wake, Dk. Hosea, ilitoa taarifa ya uchunguzi kuhusu kashfa ya kuwapo kwa rushwa na upendeleo katika utoaji zabuni kwa Richmond, ikieleza kuwa hakukuwa na rushwa wala upendeleo.

  Hata hivyo, ripoti hiyo ilibainika kupingana na uchunguzi wa sakata hilo uliofanywa na Kamati ya Teule ya Bunge, iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ambayo ilianisha kasoro kadhaa, zikiwamo za kuwapo mazingira ya rushwa.

  Kutokana na tofauti hiyo, kamati hiyo ilipendekeza bungeni Dk. Hosea na watendaji wengine mbalimbali serikalini, ambao ilidai walihusika na upendeleo wa utoaji zabuni kwa Richmond wawajibishwe, na Bunge liliafiki mapendekezo hayo na kuyapitisha kama mojawapo ya maazimio yake kuhusu sakata hilo.

  Kwa kuzingatia hali na hasa baada ya Serikali kutoa taarifa yake katika mkutano uliopita bungeni,
  taarifa ambayo ilikataliwa na Bunge, msimamo wa Bunge dhidi ya TAKUKURU na hususan mkurugenzi wa taasisi hiyo si mzuri na wabunge kupitia mijadala bungeni wamekuwa wakishinikiza wawajibishwe, ikiwa ni pamoja na kujiuzulu.

  Katika taarifa yake kuhusu adhabu aliyopewa Dk. Hosea, Serikali kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja ilisema mkurugenzi huo amepewa onyo kwa kutokuwa makini kuhusu Richmond, hatua ambayo inapingwa na wabunge.
   
 2. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Nikianza na hili binafsi kushindwa kubaini udhaifu kwa TAKUKURU litakuwa kosa tu pale itakapo thibitika beyond reasonable doubts kwamba walifanya uzembe katika kazi yao ya kuchunguza. Nadhani wanaiita proof on negligence (mtanisaidia wataalaam). Na hii ku toa ushaidi yaweza kuwa ni ngumu sana. Kwa mawazo yangu nadhani ndio imepelekea serikali kutomchukulia hatua. Hi ni kwa mfano dakitari akifanya upasuaji mtu kichwa alafu huyo mtu akafariki, ili huyu mtu awe na kosa lazima kuwe na ushahidi madhubuti kuwa daktari alifanya uzembe katika upasuaji. Kitu ambacho mara nyingi ni vigumu. Takukuru kama wakaguzi wengine au wachunguzi hutumia sample na available information. So if at that time uchunguzi unafanyika hawakupewa enough infos then wangeconclude vile na wasiweze kuwa hatiani hata kama baadae information zaidi zitajulikana na zikafanya ile conclusion yao ya awali kuwa tofauti.

  Kama kweli hii ndo nia ya TAKUKURU Basi kwa kweli watakua wamepoteza mwelekeo.


  Sawa hili la posho fanyeni kwani ndo kazi yenu.

  Hapa pengine nitatofautiana na wabunge kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kwamba there was intentional negligence katika kazi aliyoifanya Hosea. So hiyo adhabu wabunge wanayoitaka inatakiwa iambatane na facts. Otherwise Hosea atakuwa anaonewa. Tukifuata hisia utaona Hosea ana makosa lakini Profesional wise utagundua bado we need to prove some facts.
   
 3. H

  Heri JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kama tuhuma hizi (kuchunguzwa kwa kamati ya bunge ya madini nishati) ni kweli , PCCB itakuwa inafanya kazi kwa visasi..

  Tungependa kufahamu kwa sababu gani wanafanya uchunguzi? Je wametumwa na mtu/serikali?
  Wana vitu vingi vya kuchunguza. Binafsi sidhani ni kazi yao kuchunguza vitu kama kupokea posho mara mbili (CAG atafanya kazi gani).

  Inawezekana watumishi wa PCCB hawajui wajibu wao.

  Wanasimamia gate collection za TFF, Interviews za kazi.

  Je equivalent organization to PCCB ni zipi UK, USA, RSA?
  .
   
 4. l

  lovulovu Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hebu tuwe wakeli katika hili. ni kazi yao takukuru kuchunguza tuhuma zozote dhidi ya mtu yeyote anayetuhumiwa kuhusika kwa njia moja au nyingine na rushwa au kwa jina la siku hizi ufisadi. kwa hiyo waacheni takukuru wachunguze.

  ni makosa kama sisi raia tutawakingia kifua wabunge fulani au watu fulani kwa sababu tu tunawapenda. tusiajali mapenzi yetu hapa. kila mla rushwa awe zitto, slaa, mbowe au hamad na juma duni haji wake wachunguzwe tu, mbaya kumwonea mtu.

  tutakuwa tunaweka precedent mbaya kama tutang'angania akina mkapa, lowassa, rostam, manji, yona na jeetu pateli peke yao ndio wachunguzwe tu. tuwe na uchungu na mali yetu badala ya kuchagua nani awe na kibali cha kutuibia na asichunguzwe na nani aibe na achunguzwe!
  lovulovu
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Waachwe wafanye kazi yao sawa.Lakini isyo kwa mtindo wa tit for tat!
  Wanatakiwa wakati wote wafanye kazi zao kikamilifu bila kuangalia sura wala cheo na bila kujali kwa vile huyu kanifanyia hivi basi atakiona!
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Baada ya kuchunguzana saaana na kutofanyika jambo lolote la maana, tutaanza kuondoana roho kisasa( Sumu na Risasi). kurushiana Ndumba hirizi na vinyamkela ni nyenzo za juzi.
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hosea anatapatapa kwani anachotakiwa kufanya sasa ni kujiuzulu kwa kuwa haaminiki tena,sijui aliyemteua anasubiri nini kutomtema hadi sasa,huyu bwana Hosea ana taaluma nzuri ya sheria lakini kaiweka chini ya godoro na kukumbatia fedha.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Posho zimewatajirisha saana Waheshimiwa wetu hawa. Wanalipwa kila wanakoenda hasa ile Kamati ya mashirika ya UMMA kiasi kwamba hawaoni kabisa jinsi mashirika haya yanavyotafunwa. Ile taarifa ya Mh Ndasa kuhusu TANESCO imeishia wapi?
   
 9. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nothing is wrong with their UCHUNGUZI!
   
 10. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #10
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  TAKUKURU wana wajibu wa kisheria kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za kwamba Wabunge tumekuwa tukilipwa zaidi ya tunachotakiwa kulipwa kisheria. Wabunge hatuna kinga ya kufanya vitendo vya matumizi mabaya ya fedha za umma na hatua hii ya TAKUKURU itaondoa 'impunity'. Kwamba wanafanya hivi kwa visasi sio kweli. Ni wajibu wao. Uchunguzi huu unafanyika kwa Kamati zote za Bunge na sio hizi tatu peke yake. Hivi kama Mbunge analpwa pesa ili asafiri kwa siku 5, na yeye anasafiri kwa siku moja. CAG anagundua hilo katika ripoti yake, kwa nini TAKUKURU wasichunguze na kufungua mashitaka?

  Tuwaache TAKUKURU wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria. Bunge pia tufanye kazi yetu ya kuwasimamia hao TAKUKURU ili watende mema. Hiyo ndio checks and balances.
   
 11. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #11
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Ndio maana ni vizuri TAKUKURU wachunguze hayo malipo ya Waheshimiwa na kueleza ukweli. Kila kitu kitakuwa wazi. Ndasa hakuwa na Taarifa. Alichangia tu Bungeni na uchunguzi wa aliyoyasema unafanyika ili kuona kama ni kweli au siyo kweli. Kitu kimoja ninachojua ni kwamba TANESCO hawana sera ya kuuza nyumba.
   
  Last edited: Aug 6, 2009
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Zitto hapa umesema kitu kimoja ambacho huwa kinanisumbua sana; kwanini uchunguzi wa CAG usiwe msingi wa kuleta mashtaka dhidi ya wahusika? Kwanini CAG asipewe mamlaka ya kuleta mashtaka au kuwasilisha ushahidi wake kwa DPP kwa kuleta mashtaka badala ya chombo kingine kuchunguza kilichokwisha chunguzwa hasa kama wote wanaangalia ushahidi ule ule?

  Hivi TAKUKURU wakirudi na kusema kuwa hakuna matatizo katika uchunguzi wao (kama walivyofanya kwenye Richmond) ripoti ya CAG itaonekana vipi?
   
 13. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #13
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  MwanaKijiji ni suala la mgawo wa kazi tu kwani ikiwa CAG atafanya auditing na huyo huyo kuendesha mashtaka hapatakuwa na 'good governance' kwani principle inataka kila mmoja afanye kazi yake na kumwachia mwingine ili kuepuka mgongano wa maslahi ambao unaweza kutokea. Ndio maana hivi sasa tunaondoa waendesha mshataka kutoka Polisi ili kutofautisha kazi ya kuchunguza inayofanywa na jesh la Polisi na kazi ya kuendesha mashtaka iliyokuwa inafanywa na jehsi hilo hilo. Hivyo CAG akishaona kuna ubadhirifu yeye anaishia hapo maana yeye sio mtaalamu wa makosa ya jinai , mtaalmu wa makosa ya jinai ni DPP na kabla ya DPP kuchukua kesi ili kuendesha mashtaka Polisi wanafanya uchunguzi wao (na kama ni kosa la Rushwa, TAKUKURU wanaweza kufanya uchunguzi kuupeleka kwa DPP na kisha kuendesha mashtaka wao). Iwapo tukirundika auditing, uchunguzi na uendesha mashtaka kwa mmoja itakuwa na hatari (risk) ya Taasisi hiyo moja kuhodhi mamlaka na kuonea watu (absolute power corrupts absolutely).

  Huu ni mfumo unaotumika katika nchi zote za kidemokrasia. CAG wa USA anaendesha mashataka? Au FBI wanaendesha mashtaka? Hii ni mifano ambayo itakuwa rahisi kwako kuchimba zaidi. Nadhani mfumo wa sasa ni mzuri na unaweka checks and balances. Huko mbele ya safari tutapa DPP anaefanya kazi kwa uadilifu, usijiali kaka
   
  Last edited: Aug 6, 2009
 14. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo hata wewe kamati yako inachunguzwa. Hiyo ni aibu!

  Kwa nchi zilizoendelea ki utandawazi na uwajibikaji wa viongozi, hii ingekuwa ni kashfa kubwa kwa mtu kama Zitto, ambaye ndio kama mwokozi au mtume fulani wa kisiasa akatokea na yeye tume yake inachunguzwa.

  Zitto shukuru Mungu uko kwenye uongozi nchi kama Tanzania ambapo kitu kama hicho watu hawajali.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Zitto; kuna mgawanyo mzuri wa kazi na mgawanyo mbaya wa kazi. Kwa vile umetolea mifano taasisi za Marekani niseme hivi.

  Taasisi mbalimbali za hapa zina uwezo wa kukusanya ushahidi ambao unaweeza kutumika mahakamani na zaidi ya yote zina uwezo pia wa kukamata (arresting power). Hivyo utaona kuwa idara hizi zina nguvu tofauti tofauti.

  Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Marekani (iliyoko chini ya Wizara ya Biashara) ina wakaguzi wa aina mbalimbali lakini pia ina wale wanaoitwa "Special Agents" ambao ni maafisa wa kusimamia sheria wakiwa na nguvu za kuzuia, kukamata na kupekua kupata ushahidi. Wanapofanya uchunguzi na wanapoamini kuwa uhalifu umefanyika wana uwezo wa kumkamata mhusika na kukusanya ushahidi wa tukio la kihalifu na wakapelaka ushahidi huo kwa Waendesha mashtaka wa Marekani (Federal Prosecutors).

  Wale FPs wao wanapitia ushahidi huo na mara nyingi wanafungua kesi kwa kutegemea ushahidi uliokusanywa na maafisa wa Mkaguzi Mkuu ambao huitwa kama mashahidi wa upande wa mashtaka.

  Hilo pia linahusu FBI ambao kama unavyojua ni law enforcement agency. FBI wana uwezo wa kupekua kukamata na kukusanya ushahidi wa suala la kihalifu na ushahidi wao huuleta kwa FPs ambao hufungua mashtaka kwa kutegemea ushahidi uliokusanywa na FBI.

  Kinachoepukwa ni kurudia uchunguzi mwingine tena. Yaani FPs hawaanzishi uchunguzi mwingine ila wasiporidhika wanawaambia watu wa hiyo idara kuwa ushahidi wao siyo mzuri n.k

  Ni kweli tumeondoa uendeshaji mashtaka toka mikononi mwa Polisi lakini bado hatujajenga mfumo mzuri wa kushughulikia uhalifu. Kwenye suala hili tunalolizungumzia naamini CAG anapaswa kuwa na maafisa wa usimamizi wa sheria ambao wakati CAG anafanya uchunguzi na kukuta kuwa jambo fulani lina ushahidi wa kutosha wa uhalifu basi anaweza kumkamata mhusika na idara mojawapo ya CAG ikaandaa kesi na kuipeleka kwa Prosecutor ili waiendeshe.

  Kwa kufanya hivyo, tutaondoa duplicity of roles isiyo ya lazima. Kama CAG kaingia Wizara ya Maji na katika uchunguzi wake kaona shilingi bilioni 2 hazina maelezo, kauliza nyaraka hakuna, kauliza vilivyonunuliwa hakuna; anaambiwa nileteeni ushahidi jamaa wanasua sua halafu yeye anaandika kwenye ripoti "nyaraka tuliagiza lakini hatukupewa" na ripoti inapokelewa ikionesha "ufisadi" wa bilioni 2. Hii ni kejeli.

  Ingepaswa kuwa baada ya kuulizia taarifa muhimu toka Wizarani na hazipati maafisa wa CAG wawe na "trigger clause" katika sheria yao ambapo mhusika asipoleta taarifa za suala linalozidi shilingi milioni 1 basi wana nguvu ya kuitisha akaunti zake na za ndugu zake wa karibu, mali zake, na zaidi ya yote kumuweka kizuizini wakifanya uchunguzi. Na wakiona kuwa upo ushahidi wa suala la kihalifu basi ushahidi wote haupelekwi tena TAKUKURU bali kwa mwendesha mashtaka (wa wilaya, mkoa n.k, hata Tarafa kama tunaweza kuwa nao)

  Jukumu la huyo mwendesha mashtaka utaona siyo tena kuanzisha uchunguzi wa jambo lile bali kuandaa kesi dhidi ya wahusika na maafisa wa CAG wanakuwa ni mashahidi wa upande wa mashtaka.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  tangu lini idara kuchunguzwa inakuwa ni aibu? Kwani wakati wote uchunguzi lengo lake ni kutafuta ubaya.
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  hao ni panya na panya (sijakosea) wanakamatana mikia.
   
 18. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Uchunguzi siku zote lengo lake ni kutafuta kama kuna mabaya. Hakuna uchunguzi wa kutoa zawadi za mazuri.

  TAKUKURU wameshuku kwamba tume hizi, ikiwemo ya Zitto, kuna ubadhilifu, ndio maana wanachunguza. Hawaendi pale kutoa zawadi za birthday kwa kina Zitto, bali kuchunguza suspicion za ubadhilifu wa kina Zitto.

  Hizo kamati nyingine sio jambo la ajabu, CCM ni wabadhilifu. Zitto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu, Mbunge wa upinzani, anaejiweka kama adui wa ufujaji na rushwa na ufisadi. Kamati yake inachunguzwa kwa kulipana kibadhilifu. Kashfa! Na unajua ni kashfa, Mwanakijiji; Unatetea kwa vile wewe huwa ni shabiki, unaendeleza "a mission." Ukishaniambia uko "on a mission" huwezi kuja kujaribu kunipotosha kwamba una chembe ya objectivity.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280

  sasa kufanyika uchunguzi siyo sawa na kukutwa na ubaya; kwa sababu uchunguzi usipokuta ubaya inakuwaje mtu aone aibu kuchunguzwa? Sasa haiwezekani kuwa kashfa iwe katika kuchunguza! Kashfa iko kwenye matokeo ya uchunguzi. Maana tukikubali kuwa uchunguzi tu unatosha kuunda kashfa basi tuna kashfa nyingi zaidi kuliko tunavyofikiria!.

  Mhandisi akifanyia uchunguzi daraja haina maana daraja hilo ni bovu!
   
 20. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Najua unapenda historia na literature, utakuwa umemsoma Kaisari.

  Isitoshe Kaisari ni favorite subject wa idol wako, Mwalimu Nyerere. Naamini umesikia mambo yake.

  Kwa nini Kaisari alisema mke wake hatakiwi kushukiwa? Nini logic ya hiyo concept iliyo maarufu duniani?
   
Loading...