Hongereni: Wanawake wema bado mpo kwenye dunia hii

Hongereni: Wanawake wema bado mpo kwenye dunia hii

Afadhali wewe umekuja na uzi wa kusawazisha hali ya hewa maana humu huzungumnzwa madhaifu yao tu,
Ni saikolojia mbaya sana kwa mwanaume kufikiri kuwa kila mwanamke ni kahaba, ni mpumbavu, au ni mhuni.

wapo wadada wamejiweka tayari kabisa kuwa wake wema kwa waume watakao waoa. Nasema tena wapoo tena wanasubiri kwa hamu wanaume waliokomaa akili za kimwili na kiroho ili wawaoe.
 
daaah mkuu hongera afadhari umenipa moyo wa kuoa, ila mimi nitaoa humuhumu jf
na naamini atakuwa mwema kama wako,
na lazma nilete mrejesho
hahahahah
Mmh kila la kheri mkuu
 
Habari za siku nyingi wadau wa MMU. Nimerudi baada ya kupotea siku nyingi kutokana na majukumu ya utu uzima.

Ningependa kuwapongeza wanawake wote walioolewa wenye uvumilivu wa kushinda dhoruba mbalimbali zinazokabili ndoa zao. Mimi kama mme wa mtu nimejifunza na kukubali ya kuwa kuna wanawake wavumilivu, kuna wanawake sahihi wanaoweza kuishi na wewe katika shida na raha.

Kwa uzoefu wangu nimewahi kupitia changamoto kadha zikiwemo za magonjwa zilizopelekea kuyumba kiuchumi lakini bado mke wangu alizidi kunisapoti katika dhiki zote hizo. Ukweli ni kuwa hata dunia ichafukeje na kunuka kwa uovu mwingi bado wanawake wanaomcha Mungu wapo.

Kama hujaoa jibidishe kumpata mwanamke aliye sahihi kwa ajili ya maisha ya ndoa.

Hongereni wanawake wacha Mungu, Hongereni wanawake mnaojibidisha kuwatendea mema waume zenu pasipo kukata tamaa.
YESU KRISTO awaongezee amani ipitayo amani zote na furaha ipitayo furaha zote za ulimwengu huu na ulimwengu ule ujao.
 
Ni kweli kabisa wapo tena wengi , ni muhimu kuwa na macho ya rohoni tu, au hekima ya MUNGU kumpata, la basi upate bahati kumuona au kukutana na mkeo mwema au mumeo mwema.
Isaya 34:16 imeandikwa ," hakuna atakaye mkosa mwenzake".
Na kwa hakika maisha ya furaha ni maisha ya kuwa ndani ya agano la mwili mmoja , kati ya mme na mke na MUNGU uwabarikia( inakuwa paradiso)
NB:
Lakini kwa walio waaminifu kwenye kila idara ndoa(agano)Malaki 2:14.

Kwahiyo wenye kuhitaji kuoa au kuolewa msikate tamaa, mke au mme wako mwema yupo. Hacha uoga,
Uoga ni dhambi - Ufunuo 21:8.
Ni saikolojia mbaya sana kwa mwanaume kufikiri kuwa kila mwanamke ni kahaba, ni mpumbavu, au ni mhuni.

wapo wadada wamejiweka tayari kabisa kuwa wake wema kwa waume watakao waoa. Nasema tena wapoo tena wanasubiri kwa hamu wanaume waliokomaa akili za kimwili na kiroho ili wawaoe.
 
natania bhna hizi habari za mrejesho nawaachia akina Cutelove na mwenzake
Nilitaka kuzimia.... Mara paaap mrejesho unakuwa wa zesh na witmak255, cheiiiiii hahahahahahahahhaah
 
Hallelujah..!!
Finally mkombozi wetu Musa umetuvusha salama kwenye mikono ya hawa Pharaoh wa humu ndani.!!
Barikiwa wewe na mkeo mkuu,
Pharaoh..[emoji3][emoji3] ? Bila shaka ni wakina Asprin na Mshana jr ..[emoji23][emoji23][emoji23]...
Sisi wengine tunajua kubembeleza tu...[emoji7][emoji7]
 
Pharaoh..[emoji3][emoji3] ? Bila shaka ni wakina Asprin na Mshana jr ..[emoji23][emoji23][emoji23]...
Sisi wengine tunajua kubembeleza tu...[emoji7][emoji7]
Haha'
Usinigombanishe na hao watu mkuu, huyo mmoja naweza jikuta nimegandishwa kwenye paa..!
 
Shukuru Sana umepata kilichochema

Shukrani
 
Back
Top Bottom