Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,602
Habari za siku nyingi wadau wa MMU. Nimerudi baada ya kupotea siku nyingi kutokana na majukumu ya utu uzima.
Ningependa kuwapongeza wanawake wote walioolewa wenye uvumilivu wa kushinda dhoruba mbalimbali zinazokabili ndoa zao. Mimi kama mme wa mtu nimejifunza na kukubali ya kuwa kuna wanawake wavumilivu, kuna wanawake sahihi wanaoweza kuishi na wewe katika shida na raha.
Kwa uzoefu wangu nimewahi kupitia changamoto kadha zikiwemo za magonjwa zilizopelekea kuyumba kiuchumi lakini bado mke wangu alizidi kunisapoti katika dhiki zote hizo. Ukweli ni kuwa hata dunia ichafukeje na kunuka kwa uovu mwingi bado wanawake wanaomcha Mungu wapo.
Kama hujaoa jibidishe kumpata mwanamke aliye sahihi kwa ajili ya maisha ya ndoa.
Hongereni wanawake wacha Mungu, Hongereni wanawake mnaojibidisha kuwatendea mema waume zenu pasipo kukata tamaa.