Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,719
- 5,368
Huu ni mtazamo wangu na ni kwa mujibu wa katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa uhuru wa mawazo (soma ibara ya 18 ya Katiba yetu).Nimetanguliza hili kwa sababu kuna upuuzi sasa umengia katika Nchi yetu, eti vyombo vya Inteligencia sasa uwezo wao umekuwa mkubwa tu katika kukamata watu wenye mawazo tofauti au wanaotoa maoni tofauti na kinzani na yale yaliyozoeleka! Na si katika kupambana na Wahalifu/Magaidi kama hawa walioua askari wetu wa8 hivi karibuni!
Nimefuatilia magazeti ya leo na nika-conclude kuwa Wanahabari wetu wameanza kuonyesha uweledi mkubwa katika kazi zao na mimi kama Mtanzania hapa kijijini kwangu Mwanduhitinje NAWAPONGEZA SANA wanahabari wote!
Kuna matukio makubwa kama matatu jana katika Nchi yetu yametokea na ambayo yalipaswa leo kupewa kipaumbele katika vyombo vyetu vya habari! La kwanza na kubwa ni kuagwa kwa miili ya Mashujaa wetu wa8 ambao wamepoteza maisha yao wakiwa wanatutumikia Watanzania! na matukio mengine ni uzinduzi wa Hosteli za UDSM na Kotazi za Magomeni zilizofanywa na Mheshimiwa Rais Magufuli.
Mtazamo wangu unanituma kwamba Rais wetu alipaswa kutoa kipaumbele katika kuaga miili ya hao Mashujaa wetu wa8 na hata ingebidi kuahirisha masuala ya uzinduzi wa hayo "Mahosteli" na "Makotazi !.Kupoteza maisha si jambo la mchezo mchezo! tumeona juzi tu hapa Bunge la Uingereza lilivamiwa na watu wa5 wakapoteza maisha na Dunia ikatikisika na Waziri Mkuu Bi.Theresa May akahutubia Taifa kuelezea hali ya Nchi kiusalama!
Wanahabari kwa uweledi wao mkubwa wameamua kutoa kipaumbele kwa habari ya vyeti vya kughushi vya Watumishi badala ya Uzinduzi wa "Mahosteli" na "Makotazi" na hii ni kama ujumbe fulani kwa watu fulani wanaofikiri wao kwa kuwa na madaraka basi wanadhani wana akili kuliko wengine na wakati hata elimu zao kutoka chini ni za kuunga unga tu au za HAPA na PALE!
Ki ukweli habari kubwa iliyopaswa kupewa kipaumbele na hata Shughuli za Mheshimiwa Rais ingebidi kusimama jana ni kuagwa kwa MASHUJAA WETU wale waliopoteza maisha yao na kuacha familia zao katika simanzi kubwa sana! Eti Waziri Mwigulu anasema stahiki zao hazitacheleweshwa! kauli za kitoto kabisa!
Kauli za IGP na akina Mwigulu ni za kawaida mno na hata hao wanaowaita wao Majambazi zimezoeleka kwao na sasa wanaziona sawa na nyimbo za mapenzi za akina DIAMOND tu! Kama unabisha unaweza kusemaje kuhusu mfuatano wa matukio haya kuanzia lile la Kituo cha Staki Shari ambalo Askari wetu waliuawa na Silaha kuchukuliwa! lile la hivi karibuni ambalo walifanya uhalifu na hata kuamua kugawa mkaa uliokuwa umezuiwa kituoni! na hili la sasa la kuua Askari wetu wa8 na kuchukuwa Silaha!
Hawa yawezekana si majambazi kama anavyodai Kamanda NSATO,hawa wanaweza kuwa MAGAIDI na tena MAKOMANDOO kabisa! Jambazi gani anawezi kupiga mkono "Defender" ya Polisi yenye Askari zaidi 8 tena wenye SMG! Kwa nini Taifa hili tunafanywa kama vile limejaa watu mambumbu kwa asilimia 99%?! TUNATAKA KUSIKIA KAULI YA AMIRI JESHI WETU MKUU KUHUSU USALAMA WA NCHI YETU na jana ndio ilikuwa mahali pake katika kuaga miili ile ya MASHUJAA WETU!
Kauli za wasaidi au wapambe kuwa Rais hapangiwi cha kufanya ni kauli za watu wenye NJAA na ambao kazi yao sasa ni kujikomba tu ili siku ziende na si kauli za kulisaidia Taifa hili! Ni watu walioamua kwa makusudi kabisa kutumia matumbo yao kufikiri badala ya Vichwa vyao! Na ujumbe wangu kwao ni kuwa tutawapinga muda wote kwa NGUVU zote bila kujali wako wangapi na wana NJAA kiasi gani!
HONGERENI TENA WANA HABARI WETU KWA MAARIFA YENU KATIKA KUFIKISHA UJUMBE!
Ahsanteni na Karibuni tule PASAKA hapa Mwanduhitinje !