Hongereni STRABAG! Dar Rapid Transit imefana mno!

Hongereni STRABAG! Dar Rapid Transit imefana mno!

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,530
Reaction score
46,614
Strabag wamefanya kazi kubwa mno..., em' ona mwenyewe..!

Dart4_zps86ebdba6.jpg


Dart5_zps39a1712e.jpg


Dart3_zps87ecc1ba.jpg


Dart2_zpsf6127c56.jpg
Dart1_zps53c442c4.jpg
 
Kweli kazi nzuri sana kwa miji ya kisasa
Kasoro ndogo tu ni kwamba Sio rafiki kwa walemavu wavuka njia.
Fuatilia Kipindi alichorusha Zembwela Jpili iliyopita sehem za kuvukia hasa kwa walemavu ndio utapata jibu.
 
Tujiandae kuhama mji sababu ya foleni...no enough feeder roads
 
Naomba kujuzwa, barabara za DART zitakuwa na hizi daladala za kawaida tena?
Nauliza hivi coz nilikuwa na argument na rafiki yangu, tulipita njia hiyo lakini sikuona bus stops za kawaida, aside zile za mabasi ya mwendo kasi, ndio maana nauliza, daladala za "kimara-k.koo, kimara-posta, kimara-mwenge'' zitatumia njia hiyo?
 
Technically hiyo barabara italeta ajali sana hususani magari kupigana pasi.
Kweli mkuu barabara zimepunguzwa upana sana kiasi kwamba malori mawili kwenda sambamba kama ilivyokuwa zamani ni shida. Zamani ilikuwa magari makubwa na madogo yanaweza kwenda sambamba na kisha nafsi kubaki hata ya mwendesha baiskeli,pikipiki mtembea kwa miguu kupita lakini sasa ni shida. Labda kuwe na mpango wa kupunguza upana wa magari makubwa kama malori na mabasi
 
Utashangaa mpaka inazunduliwa rasmi sehemu nyingine zitakuwa zimeshabomoka!! maana miradi ya siku hizi, ubora ni zero lakini ukisikia fedha zilizopukutika utataman kulia!!
 
Ni ngumu kuamini kwa sasa kama hawa jamaa wamepiga kazi,nadhani cha kusubiri ni pale itakapofunguliwa rasmi ambapo hakutakuwa na madaladala barabarani.
 
Mimi kinachoniuma ni kitendo cha sisi wenyewe kutokuwa wastaarabu afu tunasingizia ubora si mzuri. Jamani watu wanatupa taka hovyo magari yanavyo overtake ni shida yaani mtu hatumiii hata akili ya kawaida tu kwamba hii barabara imekuwa nyembamba kwa hiyo hata uendeshaji inabidi uwe makini ili usiharibu miundo mbinu na chombo chako niko against na serikali kwa mambo mengi lakini kuna mengine tunawaonea tu. nimekuwa nikifatilia hata stand ya hapa mbezi asubuhi huwa inafagiwa ukipita hadi unafurahia subiri baada ya masaa 3. Na vyombo vya kuhifadhia taka pale vipo kabisa lakini utakuta uchafu hadi inasikitisha. Kuna mambo tuache kulalamika kabisa mtu akikutengenezea kitu wewe ukaki haribu kwa matumizi ya hovyo hata kingekuwa kitu imara au chenye ubora wa vipi kitaharibika tu kabla ya wakati wake tunapaswa kubadilika
 
Back
Top Bottom