Tikerra, njia pekee ya mfanyakazi kuonyesha frustration zake kwa employer ni kugoma. mfanyakazi mmoja hawezi kugoma, kwani atawajibishwa mara moja. Nguvu ya mgomo ni pale unapowashirikisha wafanya kazi wote. whether wanafanikiwa kupata madai yao au hapana. Serikali yetu inaendesha mambo kibabe mno, ndio maana hakuna mgomo ambao umekuwa successful zaidi ya ule wa TRL. Tanesco walijaribu kugoma kupinga network group wakakandamizwa na Mkapa akimtumia Kapuya kuwatisha. Muhimbili madaktari wanafunzi waligoma miaka ya 2005, wengi waliishia kufukuzwa kazi.
Lakini vitisho na haki havitangamani. Ghiliba za serikali kwa wafanyakazi ndizo zinazofanya wafanyakazi katika sekita mbalimbali wagome. Na ni haki yao kugoma. Hata wale wazee wastaafu wa East Africa communinty wangeweza kufanikiwa tu kupata madai yao kama wangekuwa kazini na kuamua kugoma.Serikali inawadharau kwakuwa hawako kazini na hawawezi kugoma! nionavyo, mgomo wa NMB wenye nguvu zaidi uko njiani unakuja. Nasi tulio nje tunatakiwa tuwasupport! Kugoma ni haki yao hadi kieleweke. Na serikali iache ghiliba! ishughuklikie madai yao sasa kwa kuwa inayafahamu. Watakapo goma tena taifa litapata hasara kubwa zaidi. Na akakayedhurika zaidi ni mlalahoi mtanzania!!