Unyama uliofanywa na Mkurugenzi wa Shirika la Bima kwa wafanyakazi wake

vtuko

Member
Jun 12, 2016
41
25
1. Wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa walikua wanafanya kazi Kwa mikataba ya miaka 3 renewable kuanzia 2010 kwa sababu Shirika lilikuwa bado halijaondolewa kwenye listi ya mashirika yaliyotakiwa kubinafsishwa.

2. Kuanzia kipindi cha Aprili 2019 hadi agosti 2020 hatukupewa yoyote.

3. Mkurugenzi Mtendaji ameingia kazini tarehe 29 july 2019 na kutusainisha mikataba ya miezi 18 kuanzia mwezi Aprili 2019 mpaka Septemba 2020,Kwa lazima na vitisho pia kuondoa vipengele muhimu kwenye mkataba huo bila kushirikisha Wafanyakazi,wala Chama cha wafanyakazi(TUICO)

4. Wiki moja baada ya kusainisha mkataba Kwa nguvu akawapa wafanyakazi zaidi ya sabini (70) notice ya kuachishwa kazi.
Mkataba batili na wenye vitisho ( amb.email)
Bodi ya wakurugenzi ya shirika haikushirikishwa
Ameondoa wafanyakazi anaopenda yeye kwa matakwa yake binafsi bila kufuata vigezo. Hakuna tathmimi iliyofanyika kama taratibu za utumishi wa umma zinavyotaka na kuleta watumishi wengine kutoka PSSSF baada ya sisi kuwafundisha kazi.
Kutoa mamlaka ya bodi Kwa Kada ya wafanyakazi wa Memejimenti

5. Amewafukuza viongozi wa Tuico Kwa masaa 24 kisa tu walimwadikia barua mkurugenzi mtendaji wakitaka washirikishwe kwenye hili zoezi kama kanuni zinavyotaka unapoondoa wafanyakazi Kwa wingi ambao walikuwa hawana mkataba!!

6. Sheria inasema mkataba ukiisha kama mwajiri amekaa kimya bila kutoka mkataba mwingine., automatically wafanyakazi wanaendelea Kwa masharti na vigezo vya mkataba wa awali. Mkurugenzi Mtendaji amewanyima wafanyakazi gratuity Kwa utashi wake. Ameondoa kipengele cha renewal kwenye mkataba aliolazimisha tusaini,kwani kipengele hiki kilikuwa na kigezo cha tathimini ya utendaji Kwa kila mfanyakazi (Performance Appraisal)

7. Tulipeleka malalamiko yetu kwa bodi ya wakurugenzi lakini hadi leo hii hatujawahi kupata majibu ya fumbo hili la kupokwa haki yetu ya kuendelea kuitumikia nchi yetu.

8. Tunajiuliza kwanini shirika lina mikataba ya Aina mbili. Ya Kudumu Kwa wachache na asilimia 98 ya wafanyakazi wana mikataba ya miezi mitatu kinyume na Sera ya Ajira katika utumishi wa umma.Hawa wenye miezi mitatu mitatu ndiyo wahanga wa kuondolewa katika ajira!

9. Kwa nini Bodi inaruhusu shirika moja kuwa na mishahara ya Aina mbili bila kuchukua hatua za kuondoa ubaguzi Kwa wafanyakazi ambao hawajaongezewa mishahara kuanzia mwaka 2010?

TUNAOMBA YAFUATAYO:
1. Serikali itusaidie ili uamuzi huu wa Mkurugenzi Mtendaji (Dkt Elirehema Doriye) utenguliwe na turudishiwe haki yetu iliyopokwa ya kuwa sehemu ya wafanyakazi wengi ni vijana na wenye nia ya kuchapa kazi ili kusaidi mabadiriko chanya yanayofanywa na serikali ya Mh. Mama yetu Mpendwa Samia Hassan Suluhu

2. Kuishauri Serikali ili iweze kuchukua hatua za haraka kukomesha ajira za mikataba ya miezi mitatu - mitatu kwa wafanyakazi wa shirika la Bima la Taifa ili kufuata sheria za nchi na miongozo mbalimbali zinazo husiana na masuala ya ajira katika UTUMISHI WA UMMA.

HITIMISHO
Serikali kwa wakati wote imekuwa ikitupa tumaini la ajira ya muda mrefu au kuendelea kuwepo katika ajira, tunaona, ajira zetu zimekatishwa bila kufuata taratibu wala sheria za nchi.

Mkurugenzi Mtendaji amekiuka kanuni, taratibu na sheria za ajira ikiwa ni pamoja na kukinzana na Mamlaka za juu au viongozi wake, kwa kuwa uamuzi wa kusitisha ajira zetu haujapata ridhaa ya Mamlaka zilizo juu yake ikiwemo Bodi ya wakurugenzi wa Shirika

Sisi kama watanzania tuko tayari kuendelea kuitumikia nchi yetu kwa kufanya kazi serikalini kwa uzalendo, uchapakazi, uadilifu na ubunifu wa hali ya juu. Tuna imani kuwa, wizara yako ni sikivu na ipo katika nafasi ya kutenda haki. Hivyo tuna imani kuwa italishughulikia suala hili kikamilifu na kutupatia haki yetu iliyopokwa bila sababu za msingi.
 
1. Wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa walikua wanafanya kazi Kwa mikataba ya miaka 3 renewable kuanzia 2010 kwa sababu Shirika lilikuwa bado halijaondolewa kwenye listi ya mashirika yaliyotakiwa kubinafsishwa.

2. Kuanzia kipindi cha Aprili 2019 hadi agosti 2020 hatukupewa yoyote.

3. Mkurugenzi Mtendaji ameingia kazini tarehe 29 july 2019 na kutusainisha mikataba ya miezi 18 kuanzia mwezi Aprili 2019 mpaka Septemba 2020,Kwa lazima na vitisho pia kuondoa vipengele muhimu kwenye mkataba huo bila kushirikisha Wafanyakazi,wala Chama cha wafanyakazi(TUICO)

4. Wiki moja baada ya kusainisha mkataba Kwa nguvu akawapa wafanyakazi zaidi ya sabini (70) notice ya kuachishwa kazi.

Mkataba batili na wenye vitisho ( amb.email)
Bodi ya wakurugenzi ya shirika haikushirikishwa
Ameondoa wafanyakazi anaopenda yeye kwa matakwa yake binafsi bila kufuata vigezo. Hakuna tathmimi iliyofanyika kama taratibu za utumishi wa umma zinavyotaka na kuleta watumishi wengine kutoka PSSSF baada ya sisi kuwafundisha kazi.
Kutoa mamlaka ya bodi Kwa Kada ya wafanyakazi wa Memejimenti

5. Amewafukuza viongozi wa Tuico Kwa masaa 24 kisa tu walimwadikia barua mkurugenzi mtendaji wakitaka washirikishwe kwenye hili zoezi kama kanuni zinavyotaka unapoondoa wafanyakazi Kwa wingi ambao walikuwa hawana mkataba!!

6. Sheria inasema mkataba ukiisha kama mwajiri amekaa kimya bila kutoka mkataba mwingine., automatically wafanyakazi wanaendelea Kwa masharti na vigezo vya mkataba wa awali. Mkurugenzi Mtendaji amewanyima wafanyakazi gratuity Kwa utashi wake. Ameondoa kipengele cha renewal kwenye mkataba aliolazimisha tusaini,kwani kipengele hiki kilikuwa na kigezo cha tathimini ya utendaji Kwa kila mfanyakazi (Performance Appraisal)

7. Tulipeleka malalamiko yetu kwa bodi ya wakurugenzi lakini hadi leo hii hatujawahi kupata majibu ya fumbo hili la kupokwa haki yetu ya kuendelea kuitumikia nchi yetu.

8. Tunajiuliza kwanini shirika lina mikataba ya Aina mbili. Ya Kudumu Kwa wachache na asilimia 98 ya wafanyakazi wana mikataba ya miezi mitatu kinyume na Sera ya Ajira katika utumishi wa umma.Hawa wenye miezi mitatu mitatu ndiyo wahanga wa kuondolewa katika ajira!

9. Kwa nini Bodi inaruhusu shirika moja kuwa na mishahara ya Aina mbili bila kuchukua hatua za kuondoa ubaguzi Kwa wafanyakazi ambao hawajaongezewa mishahara kuanzia mwaka 2010?

TUNAOMBA YAFUATAYO:
1.Serikali itusaidie ili uamuzi huu wa Mkurugenzi Mtendaji (Dkt Elirehema Doriye) utenguliwe na turudishiwe haki yetu iliyopokwa ya kuwa sehemu ya wafanyakazi wengi ni vijana na wenye nia ya kuchapa kazi ili kusaidi mabadiriko chanya yanayofanywa na serikali ya Mh. Mama yetu Mpendwa Samia Hassan Suluhu

2. Kuishauri Serikali ili iweze kuchukua hatua za haraka kukomesha ajira za mikataba ya miezi mitatu - mitatu kwa wafanyakazi wa shirika la Bima la Taifa ili kufuata sheria za nchi na miongozo mbalimbali zinazo husiana na masuala ya ajira katika UTUMISHI WA UMMA.

HITIMISHO
Serikali kwa wakati wote imekuwa ikitupa tumaini la ajira ya muda mrefu au kuendelea kuwepo katika ajira, tunaona, ajira zetu zimekatishwa bila kufuata taratibu wala sheria za nchi. Mkurugenzi Mtendaji amekiuka kanuni, taratibu na sheria za ajira ikiwa ni pamoja na kukinzana na Mamlaka za juu au viongozi wake, kwa kuwa uamuzi wa kusitisha ajira zetu haujapata ridhaa ya Mamlaka zilizo juu yake ikiwemo Bodi ya wakurugenzi wa Shirika.

Sisi kama watanzania tuko tayari kuendelea kuitumikia nchi yetu kwa kufanya kazi serikalini kwa uzalendo, uchapakazi, uadilifu na ubunifu wa hali ya juu. Tuna imani kuwa, wizara yako ni sikivu na ipo katika nafasi ya kutenda haki. Hivyo tuna imani kuwa utalishughulikia suala hili kikamilifu na kutupatia haki yetu iliyopokwa bila sababu za msingi.
 
Kama mtu anahisi utaratibu haukufuatwa wakati wa kuachishwa kazi, zipo mahakama ya kazi kwa ajili ya kusikiliza kesi kama hizi. Watanzania tuna uwoga mwingi sana, haki yako ikisiginwa idai kunakohusika.
 
Poleni, tatizo la watanzania ni mabingwa wa kulalamika bila vitendo, mkiambiwa kudai katiba mpya mnaona itamnufaisha Mbowe na watoto wake nyie hamtaki kuchafuka, issue kama hii mlitakiwa kuandamana ili msikilizwe kwa haraka.
 
Uyu jamaa ameshirikiana na bank ku block account za bank kwa wafanyakazi waliochukua mikopo na sasa wanaishi kama digidigi watu hawana pesa za kulipa mawakili.
 
Poleni, tatizo la watanzania ni mabingwa wa kulalamika bila vitendo, mkiambiwa kudai katiba mpya mnaona itamnufaisha Mbowe na watoto wake nyie hamtaki kuchafuka, issue kama hii mlitakiwa kuandamana ili msikilizwe kwa haraka.
Watu wanaongelea matatizo yao kazini jinga moja linakuja na mambo ya gaidi na katiba, Hawa wafanyakazi wanahusikaje na kudai katiba wakati wewe muhusika uko kwenye keyboard unaweweseka na Mbowe?
 
Shirika lolote la bima halihitaji zaidi ya wafanyakazi 50 wa kudumu waliobaki wanatakiwa kuwa machinga walipwa kwa commission kwa kuleta wateja

Nice pesa kilikuwa zikiishia kulipa vi desk officers hivi kwenye ushindani kamahuu was ambako watu wanakata bima kupitia kampuni za simu za mikononi kuna haja hata ya kuwa na ghorofa kubwa kama la NIC lililojaa wafanyakazi kibao vi desk officers?
 
Ishu ni taratibu za kumwondoa mtumishi zimefuatwa acha ushamba wa kishamba wewe!!!
 
Shirika lolote la bima halihitaji zaidi ya wafanyakazi 50 wa kudumu waliobaki wanatakiwa kuwa machinga walipwa kwa commission kwa kuleta wateja

Nice pesa kilikuwa zikiishia kulipa vi desk officers hivi kwenye ushindani kamahuu was ambako watu wanakata bima kupitia kampuni za simu za mikononi kuna haja hata ya kuwa na ghorofa kubwa kama la NIC lililojaa wafanyakazi kibao vi desk officers?
Watajua hawajui!😁vijana mjiajiri!
Waende mahakama ya kazi, arbitration huko!
Hawa walikuwa ndiyo hao!
 
Shirika lolote la bima halihitaji zaidi ya wafanyakazi 50 wa kudumu waliobaki wanatakiwa kuwa machinga walipwa kwa commission kwa kuleta wateja..
Nimepata point kwenye kupunguza wafanyakazi. Ila kwenye maslahi yao na uonevu waliofanyiwa bado inatakiwa hatua zichukuliwe
 
Kama mtu anahisi utaratibu haukufuatwa wakati wa kuachishwa kazi, zipo mahakama ya kazi kwa ajili ya kusikiliza kesi kama hizi. Watanzania tuna uwoga mwingi sana, haki yako ikisiginwa idai kunakohusika.
Mijitu mingi miachishwa kazi Haina value addition kwenye mashirika hasa ya umma
Yaende mahakamani hopeless kabisa
Yana mchango gani wa kuongeza wateja NIC kuongeza Customer base?
 
Watu mnafurahia wengine wanapopata matatizo leo kwake kesho kwako
Hii inaonyesha ni roho mbaya kiasi gan watu wanashindwa kuelewa kuna watoto na ndugu wa ngapi walikua wanategemea kazi hyo hyo kwa kumfukuza kazi mtu 1 kumesabisha maumivu ya watu kiasi gani.
 
Nimepata point kwenye kupunguza wafanyakazi. Ila kwenye maslahi yao na uonevu waliofanyiwa bado inatakiwa hatua zichukuliwe
Upo sahihi mkuu mkurugenzi aliruhusu watu kuchukua mikopo ya miaka 5 baada ya mwaka 1 kuchukua akasimamisha kaz watu zaidi ya 70 akawasiliana na bank na kublock account hakuna ata mfanyakazi mmoja aliyechukua pesa yake bank mpaka leo!! Anavyosema twende mahakaman anajua hatuna pesa ya kuwalipa mawakili ns yy atashindaa
 
Back
Top Bottom