Hongereni sana wafanyakazi wa NMB,isipokuwa.........

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Hongereni sana wafanyakazi wa NMB,kwa ushindi mlio upata.Hata hivyo kumbukeni yafuatayo:
*Migomo kama ya NMB,haiumizi serikali isipokuwa wafanyakazi wengine
serikalini na wananchi wa kawaida ambao ni wadau wenu katika
'struggle.'
*Migomo kama yenu inaathiri uchumi wa nchi kwa kiwango kikubwa,
kwa hiyo ni vema ikafanywa tu kama silaha ya mwisho.
*Hakikisheni kwamba chama chenu yaani TUICO, kinafuata
sheria zote kabla ya kuitisha mgomo ili kuepuka usumbufu usio kuwa wa lazima.
 
Tikerra, njia pekee ya mfanyakazi kuonyesha frustration zake kwa employer ni kugoma. mfanyakazi mmoja hawezi kugoma, kwani atawajibishwa mara moja. Nguvu ya mgomo ni pale unapowashirikisha wafanya kazi wote. whether wanafanikiwa kupata madai yao au hapana. Serikali yetu inaendesha mambo kibabe mno, ndio maana hakuna mgomo ambao umekuwa successful zaidi ya ule wa TRL. Tanesco walijaribu kugoma kupinga network group wakakandamizwa na Mkapa akimtumia Kapuya kuwatisha. Muhimbili madaktari wanafunzi waligoma miaka ya 2005, wengi waliishia kufukuzwa kazi.

Lakini vitisho na haki havitangamani. Ghiliba za serikali kwa wafanyakazi ndizo zinazofanya wafanyakazi katika sekita mbalimbali wagome. Na ni haki yao kugoma. Hata wale wazee wastaafu wa East Africa communinty wangeweza kufanikiwa tu kupata madai yao kama wangekuwa kazini na kuamua kugoma.Serikali inawadharau kwakuwa hawako kazini na hawawezi kugoma! nionavyo, mgomo wa NMB wenye nguvu zaidi uko njiani unakuja. Nasi tulio nje tunatakiwa tuwasupport! Kugoma ni haki yao hadi kieleweke. Na serikali iache ghiliba! ishughuklikie madai yao sasa kwa kuwa inayafahamu. Watakapo goma tena taifa litapata hasara kubwa zaidi. Na akakayedhurika zaidi ni mlalahoi mtanzania!!
 
Bravo NMB
Mlifanya kilichopaswa kufanya na ona sasa wamewalipa ingawa hawajatangaza rasmi lakini wengine tuna taarifa ya yale yanayoendelea huko.
Mgomo ni siraha pekee inayoweza kuwasaidia taasisi yoyote kupata haki yao.
Very very very very unfortunately serikali yetu kwa kuwa siku zote kuwe au kusiwe na mgomo haimjali mwananchi either anaumia au uchumi unaumia, hata ukiwapa notice hakuna anayejali.
Mawazoni mwao wanasema shauri yao wacha waumie. After all wametumia pesa yao kufikia hapo walipo sasa wanajali nini?
Angalia kilio cha walimu na malimbikizo yao. Wameshatoa notice ya kugoma si leo! lakini hakuna anayejali.
Wanasubiri kuja na propaganda zao kwamba walimu wa Tanzania si wazalendo maana wamesitisha elimu ya mtoto wa Kitanzania na hivyo mwalimu aonekane mbaya.
Hivi ndivyo walifanya hata kwa madaktari.
Hakuna kiongozi wa nchi hii anayejali welfare za wavuja jasho. Hata Kikwete hajali. Believe me!
Suluhisho ni kugoma tu jamani.
Uchumi hauna maana kwa watawala tu bali unamaana kila mtanzania apate uchumi mzuri kwake pia. Na utakuwa hauna maana ikiwa mimi nafanya kazi na kulala njaa au wanangu hawawezi kupata mahitaji yao ya muhimu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom