Hongereni kina mama wote JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongereni kina mama wote JF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quinty, May 8, 2011.

 1. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mama ni rafiki wa kweli pale tunapopata majaribu na shida za dunia hii zinapotuelemea na kukosa mwongozo. Wakati maovu yanapochukua nafasi ya mafanikio; wakati wa shida ambapo marafiki tuliowaamini wametukimbia; wakati dhiki zimetuzunguka kila pande, lakini mama yuko pamoja nasi, kurudisha matumaini yaliyopotea, kutuvuta toka bondeni tulipozama, kutupa ushauri wa nini la kufanya, na kuondoa giza lililotuzunguka, kurudisha amani katika mioyo yetu na maisha yetu.
  Nawapongeza kinamama wote wa JF kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwa kinamama.
   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Unaongelea akina mama wote au baadhi? kuna akina mama wengine hizo sifa ulizotaja hawana kabisa...
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata kama nimechelewa,

  Ila naomba wamama wote wajue kuwa nawapongeza. Ni watu muhimu katika maisha ya kila mtu. Kwangu mimi binafsi, mama ni kiumbe wa pekee. Ni kupitia kwa mama (mzazi au mke) tunapata faraja na kujidai, tukitembea kifua mbele kama binadamu wenye akili kamili!!

  Nawapenda sana mama wote ambao ni responsible mothers!

  DC
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Dark City tunakushukuru sana kwa moyo wako wa kujua umuhimu wa mama nani kama mama bwana
   
 5. c

  chetuntu R I P

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanx mkuu me pia ni mama. Ubarikiwe.
   
 6. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa dear
  Hongera kwa wa mama wote..
   
 7. I

  ILUVUG Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na kwa kwa waliotangulia mbele za haki....we miss them alot........RIP
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Usijali ndugu,

  Talking of Mama means tears to me....Ahsante sana Mama yangu, ahsante sana mama wa watoto wangu na ahsante akina mama wote duniani.

  My promise to all mothers...I will never abuse a woman by my own hands or words!.....So Help Me GOD!!!!

  Mzee DC!
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana ndugu,

  Hao mara nyingi tunawasahau. Na ukizingatia wengine walipoteza uhai wao wakati wanahangaika kuleta viumbe wengine duniani..Very sad in deed na ni upendo uliopita kipimo kufa kwa ajili ya uhai wa mtu mwingine!


  Hii thread ni nzito sana kwangu....Tears tears tears of love to all mothers.

  Mungu awapunguzie adhabu hata kama mlimkosea kwa kiasi gani...Mnahitaji pumziko la milele baada ya kazi nzito mliyoifanya hapa duniani...!!
   
 10. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mbarikiwe sana kwa kutambua umuhimu wa mama...namshukuru Mungu nami aminijalia kuwa mama. Mbarikiwe wamama wote!
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hongera sana dada yangu kwa kufikia hicho kilele cha mafanikio hadi ukaitwa MAMA. Natumai utakuwa kweli ni mama...kwa matendo yako na kuwajibika kwako!

  Wapo wengi waliotamani sana kuitwa mama, na kusikia hivyo kwa masikio yao wenyewe. Lakini hawakumudu kufikia hayo mafanikio...na mbaya zaidi wengine wameitwa mama wakati hawapo tena duniani. Na pia kuna wengine kama auntie yangu alipoteza maisha yao kwa kujaribu kuyaweka sawa maisha ya watoto wao.....Tuwaombee sana kwa Mungu.

  Hakika ukimheshimu mama (siyo mama yako mzazi tu) utaishi maisha ya amani sana duniani hapa...I can say that AGAIN and AGAIN!!

  Mbarikiwe wote akina mama na watu wote wanaowapa heshima yenu stahiki!
   
 12. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Asante sana Mzee DC, kwa kweli ninamshukuru sana tu kupata neema ya kuwa mama. Namwomba Mungu anisaidie siku zote kuwa mama mzuri na anayewajibika kwa watoto wangu.
  Ubarikiwe DC
   
 13. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nami pia ni mama.Asante sana mkuu kwa kutukumbuka.
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hongera Jo,

  Hilo ni daraja la juu sana kati ya madaraja ya heshima anayaweza kupewa binadamu. Jitahidi uilinde hiyo hadhi na kuitendea haki.

  Ubarikiwe sana na akina mama wote.....Hasa wale ambao sauti zao zinafinyangwa finyangwa kwa uonevu wa hali ya juu!
   
 15. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu DC post zako kwenye híi thread zimenitoa machozi, me ni mama na kwa sasa ni mjamzito, napata complications sana. Nimesoma post zako nimepata faraja. Ubarikiwe kwa kuwa kinywa cha maneno mema kwa wamama wote.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Dada E,

  Hongera sana kwa kuwa mama. Pia hongera kwa hilo jukumu ulilonalo la kujiandaa kumleta duniani mtoto wako mpendwa.

  Hata sijui niseme nini ila nadhani tuanze kwa kuileza dunia kwamba haiwatendei haki akina mama wote na hasa hasa wale wanyonge wanaoishi vijijini. Kazi muhimu sana wanayoifanya, ila hawapati malipo yanayolingana na uzito wa kazi yao.

  Nitafikiria jinsi ya kuanzisha kampeni ya kuwatetea akina mama wote. Why not...Hawasitahili kuteseka.

  Labda nimalizie kwa kusema kuwa....Walaaniwe watu wote wanaowatesa akina mama!! Narudia tena...walaaniwe wote wote!!!

  Mzee DC
   
 17. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nikiwa nimeshuhudia maumivu, uchungu na kila aina ya karinyekarinye ambayo ilihitishwa na mime kupewa mtoto ambaye leo ni mwanangu, kitu ambacho kilinikumbusha hali kama hiyo ilivyokuwa zamani zaidi za kunileta mimi hapa duniani, nawaheshimu na kuwapa pendo langu la dhati kabisa wamama wote duniani! hongereni na poleni sana kwa shughuli nzito ya kutuleta duniani.
   
Loading...