Heko Watanzania kwa mwamko mnaoonesha wa kufuatilia masuala nyeti ya nchi yetu. Laiti tungekuwa hivi miaka 30 iliyopita tungekuwa mbali sana kimaendeleo..
Mnajua ukweli huu?: HAKUNA NCHI YA WAJINGA NA WAOGA ILIYOWAHI KUENDELEA! Ukiona ujinga na woga vinatoweka basi ujue maendeleo yapo karibu.
Hata kama serikali inaendelea kupoka uhuru na haki yetu ya kufanya maandamano mitaani, basi kwa sasa tufanye maandamano hayo online!
Nawaambia watanzania wenzangu maandamano haya yana nguvu na impact kubwa kuliko tunavyofikiri na tukiendelea hivi tutaona viongozi wetu wakijiuliza maswali mengi na kujirudi.
Mtu asibeze tunachofanya mitandaoni. Kama ilivyo kwenye maandamano mitaani kinachotakiwa katika maandamano ya mitandaoni ni UMOJA na MSHIKAMANO!
Utafiti unaonesha dozi inafika vizuri tu kwa njia hii. Tunaweza kuondokana na kero nyingi kwa njia hii na kuleta kuheshimiana kati yetu na viongozi wetu.
Tuoneshe umoja na mshikamano wetu bila kuchoka na tutaona matokeo yake.
Mungu ibariki Tanzania!