Kwa taarifa tu ni kwamba waseminari zaidi ya ishirini wamefanya mtihani wa kuongea (oral examination) leo katika seminari kuu ya mt Paulo, Kipalapala. Wamehitimisha mtihani wa baccalaureate waliouanza siku ya Jumanne.
Kwa hatua hii wanahitimisha maandalizi yao kitaaluma kuelekea upadri. Ndugu mafrate, kwa niaba ya taifa lote la Mungu hapa JamiiForums nawatakia kila jema katika kujiandaa kupokea majukumu haya matakatifu ya upadri.
Ndugu wanajukwa tuwaunge mkono vijana hawa katika maamuzi yao ya kishujaa kuwa mapadri.
Ni mimi padri mtarajiwa
Umenikumbusha mbali ndugu yangu, mie nilifukuzwa nikiwa mwaka wa kichungaji parokia moja ya jimbo la musoma, sitokaa nimsahau marehemu askofu justine samba kwa aliyonitendea. :msela:
Umenikumbusha mbali ndugu yangu, mie nilifukuzwa nikiwa mwaka wa kichungaji parokia moja ya jimbo la musoma, sitokaa nimsahau marehemu askofu justine samba kwa aliyonitendea. :msela:
ulipitia seminary gani?? kipalapala au segerea. this vocation has no guarantee or security whatsoever. naamini umeweza kupambana kuwa mkristu mwema huko uliko. unajishughulisha na nini kwa sasa???
Ulikuwa Makoko mkuu mwaka gani?
O level makoko my, A level Nyegezi kisha nikaenda ntungamo na nikamalizia segerea
Kumbe tupo wengi eh