Hongera Tundu Lissu: Hoja ya kurudisha Tanganyika!

Muungano hautavunjika moja kwa moja. Hapo cdm kwa majaliwa ikishika Dola itaanzisha serikali 3. Napo wazanzibari wakizingua ndipo Muungano unakufa kabisa. Itawagharimu sana wazanzibari walioko Bara kwani itabidi waanze upya mchakato wa aidha kurudi kwao ama kuomba vibali ya kuishi Bara.
 
Ujasiri wa Lissu ni kuwa yupo katika kufuata katiba yenu ya Muungano na siku zote anasimamia hapa
sharia hiyo ya Muungano inayobainisha Mamlaka ya JMTz No 15 Ibara ya 9 ya mwaka 1984. Kifungu cha 34. inayonena hivi


34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano

katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote

yahusuyo Tanzania Bara.

(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu

utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote

ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya

mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia

juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara,

yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,

madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa

ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu

madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika

utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.


katiba hizi mbili zina mikanganyo mikubwa sana mfano mdogo wakati katiba ya jamhuri ya muungano inataja uwepo wa waziri kiongozi rejea ibara ya 105 ya katiba ya JMT "105
.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar
litakalokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi;
(b) Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(c) Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(d) Wajumbe wengine watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba
ya Zanzibar.


Marekebisho ya katiba ya 2010 yalifuta madaraka ya waziri kiongozi na kuanzisha makamu wa rais wawili ambao hawatajwi popote kwenye katiba ya JMT kwa lugha nyingine JMT haitambui uwepo wa makamu wawili wa rais zanzibar lakini bado inatambua uwepo wa waziri kiongozi!!
 
Taratibu jamani muungano usije ukatutoa roho, Mhe. lissu taratibu mtani roho za watanzania na damu zao zitakulilia.
 
Tukiweka ushambenga na ushabiki kando Lissu ana hoja nzito sana kuhusu mustakabali wa taifa na muungano wetu! hizo ndio hoja ambazo mwanasheria mkuu AG Alitakiwa kuzi adress na ku clarify wakati anachangia sio kumrukia prof. Shivji na kuanza kumkashifu lissu! Kuna mgongano mkubwa sana wa kisheria kati ya katiba ya zanzibar ya sasa na katiba ya JMT! Haya mambo yakiendelea kufumbiwa macho yafumuka yenyewe na madhara yake ni makubwa sana kuliko ambavo yangejadiliwa sasa!!
Nakubaliana na hii observation.
Hatuwezi kuwa na laisszes-faire katka suala la muungano. Na muungano unapochezewa sehemu moja ya muungano basi wadau sisi ambao ndio wananchi tunabaki kushangaa AG na wanasheia wake wanafanya nini ofisini.

Either wana kazi ya kuutetea au hawana kazi.
Wenzetu wamekuwa na pro active stance sisi watu wetu hawana hoja wala maoni ya kutetea muungano.

Kwa mantiki ya kawaida kabisa tulitegemea katiba hizi mbili na makubaliano yoyote yawe syncronised kwa matokeo mazuri ya kuulinda muungano, on the contrary makubaliano ya kificho kati ya Hamad na Rais wa Zanzibar yanapelekea kuutibua muungano.

Ni wazi kuwa kuingia ikulu Zanzibar kwa Seif Sharrif Hamad pamoja na a relatively lack-lustre Zanzibar President, game la muungano limebadilika kabisa.

Wenzetu wana a common agenda-kunufaika kwa gharama yoyote katika muungano, au kuutosa.
Tanganyika inaelekea haina clear goals za kuhalalisha muungano apart from historical sentiments.

Sasa leo Zanzibar wamecheza kete yao and if things dont go their way- to hell with muungano,thankKys to Sherrif Hamad.

Sisi huku Tanganyika hatumuoni wa kucheza hii ngoma kwa niaba yetu serikalini.
Na ndio maana nampongeza sana Tundu Lissu kuibua hii hoja ili tujipime hata huku kwetu Tanganyika kama muungano una faida tena kwa kizazi cha leo.
 
warobaini wa muungano ni mchakato wa katiba mpya,hapa kitajulikana hicho kinachoutafuna muungano:lakini,lakini! Tuwaulize tanganyika ilikufaje nani aliiua wakati zanzibar bado ipo au yenyewe haikufa?.kama zanzibar haikufa basi na sisi hatuna budi kuifufua tanganyika,nafurahi kuzaliwa tanganyika
 
CCM wakipata madaraka wanasahau egenda zao, kumbuka 1995 Kundi la wana CCm 55 (G55)? Hata Mkapa naye alikuwepo na kina Sumaye... na nani tena? Halafu, yeye Mkapa alifanya nini na hoja ya Tanganyika?
 
Heshima kwa mh.Lisu,

Huyu jamaa kapasua jibu na katupa maelezo safi kuhusu ulaghai wa CCM kuhusu muungano.

Me naomba Watanganyika umefika wakati tudai Tanganyika yetu, kwa kweli najisikia aibu sana kuwasikia Wazenji wakijifaharisha na Uzanzibari wao, hayo utayaona zaidi ukiwa huko Zenji utatamani urudi kwenu haraka sana maana yanaudhi maneno yao.

i. Kwanini sisi Watanganyika hatujikusanyi ktk Taasisi zetu tukawashajihisha na kuwaelimisha wazalendo kuitafuta Tanganyika???

ii. Kwanini cku zote tuwe nyuma nyuma ktk suala uasili wa Taifa letu la Tanganyika??? Mkataa kwao ni mtumwa!!!
Uzalendo wa Tanganyika kwanza

Nawasilisha.
 
Yaani unataka tuanze kulalamikia mipaka tuliyotengenezewa na wakoroni?

Hapana Mkuu mipaka yote ya Tanganyiaka inajulikana na ya Z'bar inajulikana kama ilivoelezwa kwenye katiba yao ya 2010, si ndio au...???

Tunalotaka ni uwepo wa nchi yetu ya asili ya Tanganyika kama ilivo ya Z'bar kwa7bu hapa muungano haupo tena kuna ulaghai tu.
 
Kama unafikiri ni sahihi kuingia front kwenye project ya kuvunja muungano tunatumia mantiki gani kuhangaika kutengeneza miungano mingine ambayo tumeiundia mpaka wizara? hauoni kama tutakuwa tunabehave kinafki sana?
 
Salute kwako mh lissu, hawa jamaa me huwa siwaelewi kabisa, kila kukicha wanaona wao wanathamani sana katika muungano kuliko sisi, isitoshe wamekuwa ni mzigo tu kwa jamhuri, kama vipi kila mtu ale jasho lake, tupige chini haka ka union ka kizushi wabara warudi home then wazenji na wapemba waende kwao wakakae kwenye vilinge vyao waone kama kucheza bao na kupiga soga masaa 24 kutawapa hizo faida wanazoona wanapoteza
 
TANGANYIKA KWANZA.Tunaitaji nchi yetu,nchi isiyo na laana kama ya Tanzania,Tanzania ni laana ndo maana tunapata matatizo ya kiuchumi wakati tuna rasilimali za kutusha.Laana inatokana na Tanganyika kujigeuza kua wakoloni wa kuitawala Zanzibar wakati huo tukijifanya kupiga vita ukoloni huo ni unafiki unaotuletea laana.Ndugu zetu wazanzibar wanastahili kua na nchi yao nasi yetu alafu ndo tujadili muungano.

Hata hii tume ya katiba ni wazimu tupu, na ni matumizi mabaya ya pesa za watanganyika.Zanzibar hawaitaji tume ya katiba maana wamemaliza kutunga katiba yao juzi tu na wanaipenda na kuiamini iweje leo wajadili katiba nyingine tena isiyowahusu? NATAMANI WATANGANYIKA WENZANGU TUNGEAMKA TUKADAI NCHI YETU.
 
Watanganyika wapewe uhuru wao. Kwa Muda mrefu Tanganyika imejulikana kama Tanzania bara wakati huo huo Zanzibar imeendelea kuitwa Zanzibar. Ni rahisi kusikia Tanzania Zanzibar lakini kamwe hutosikia Tanzania Tanganyika. Tujiulize hivi tanganyika tuna shida na watu wasiotuhitaji? Hivi sisi hatupendi kutambuliwa na kuthaminiwa kama wazawa wa Tanganyika? Sioni faida ya muungano huu ila naona hasara nyingi sana.
Sipendi kujikomba kuomba urafiki na mtu asiokupenda na haswa anayedai kuwa unamnyanyasa. ZANZIBAR IBAKI KAMA JIRANI KAMA ZILIVYO NCHI ZINGINE TUNAZOPAKANA NAZO.

... wajinga ndio waliwao, na ilikuaje nyie mkaacha asili yenu na kujificha chini ye kivuli cha muungano, sasa tukigawana mbao mtabeba madeni yote ya Tanzania maana sisi ni wizara tatu tu, na hatujapata kitu, tunaishi kwa miguu yetu.
 
Tanganyika haitapatikana kwa bwabwaja ya Tundu Lisu here is free advice anzisheni sumsing like UAMSHO kama kweli mnaitaka Tanganyika vinginevyo Dr Ali Muhammad Shein atatumia kure yake ya veto kupinga hilo, na vile vile Tangayika ilikubali kubeba madeni ya Tanzania maana ndio iliokopo kwa wazungu, sisi tulisimama na miguu yetu.

Ili kuonyesha nia ya kweli kama mnataka Tanganyika yenu basi tupatieni chenji ya rada maana tunataka kutumia hizo pesa kuajiri "arbitrator" na mshauri mwelekezi juu ya mgao wa mali na madeni ya iliokuwa Tanzania kama alivyoiita huyu toto Tundu.
 
Nampa hongera sana lissu,ila katika uchambuzi wake inaonekana amekerwa na mabadiliko ya 10 ya katiba ya zanzibar kuitangazia uhuru.
Wakati huo huo unachambu katiba ya muungano na kukubali kuwa kuna makose yametendeka moja ni kuongeza mambo ya muungano kinyume na sheria.
Unafahamu kuwa muungano umeundwa na nchi mbili ambazo zilikuwa huru ? Sasa wewe umekerwa nini zanzibar kujitangazia uhuru wake ? Ile sio arusha wala mtwara.
Hoja ya lissu sio ya kudai tanganyika bali ilikuwa hoja ya kulalamika tu kwa sababu wazanzibari wamejinyakulia madaraka yao kwenye muungano !
Ikiwa kweli chadema na watanganyika wote munaipenda nchi yenu kwa nini mumeshindwa kuonyesha hisia zenu kama uwamsho walivyo waamsha wazanzibari kudai kura ya maoni huku wakidai uhuru wa zanzibar na mamlaka yake yote ambayo yamo kwenye muungano ?
Nikiangalia chadema ni sawa G55 ambayo iliyokuwa ikiongozwa na kikwete mmoja,g55 walidai tanganyika ,nyerere akawaita na kuwaweka kitako,aliwaambia kuwa tanganyika ni hii tanzania tunataka kuimeza zanzibar,na nakumbuka ile nguvu ya chadema ya hapo awali haipo tena,kikwete ameshawaeka kitako,mumekaa kimya,kama kweli wanaume na munaipenda tanyanyika ! Pelekeni mswada maalum wa kuirudisha tanganyika,hoja binafsi hiyo .
Pelekeni bungenii ! Musiwe wanafiki.

Kwani nyie zanzibar hisia zenu si mlianza kuzionyesha kama sisi tunavyoanza alfu mkafanikiwa???? msikelwe na kulalamikia kwetu mabadiliko ya katiba yenu, hiyo inatusaidia sisi kupata ngazi ya kuwapandia makuwadi hawa! Mwisho tutashinda na kwa namna yoyote tunahitaji tanganyika yetu.
 
Toto Tundu hana mpya fisadi tu na akili za kimbilikimo, kama kweli mnataka Tanganyika yenu azisheni kitu kama UAMSHO ili tujue mna dhamira ya kweli kudai Tanganyika yenu, vinginevyo Zanzibar itatumia kura yake ya veto kupinga kufufuka kwa Tanganyika chini ya katiba yetu mpya, jengine la msingi lazima mkubali kwanza kubeba madeni ya Tanzania maana njie ndio mliokopa kwa kujificha nchini ya mwevuli wa Muungano, Zanzibar ulisimama na miguu yetu wakati wote, mkubali hayo leteni MoU tuiangalie
 
Back
Top Bottom