Hongera Tundu Lissu: Hoja ya kurudisha Tanganyika!

Tundu-Lisu.jpg

  1. Ataka Serikali ya Tanganyika irudi
  2. Asema Zanzibar ilijitangazia uhuru

Lissu awasha moto

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unakabiliwa na hatari kubwa ya kuvunjika kutokana na kitendo cha Zanzibar kujitangazia uhuru, na kwa hiyo ni wakati mwafaka sasa wa kuanzishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika. Msemaji wa Kambi kwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Tundu Lissu, alisema hayo wakati akitoa maoni ya kambi hiyo kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa mwaka 2012/2013, bungeni jana.

Alisema misukosuko ambayo imeukumba Muungano tangu mwaka 1964 hailingani na hatari kubwa inayoukabili hivi sasa. Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema jambo hilo waliwahi kumueleza pia Rais Jakaya Kikwete katika waraka wao wa Novemba 27, mwaka jana.​

Hatari ya kuvunjika Muungano

Alisema hatari ya kuvunjika kwa Muungano inatokana na mabadiliko makubwa ya kikatiba yaliyofanyika katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kutokana pia na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

“Hii ni kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya mwaka 2010, inaashiria tafsiri mpya ya Makubaliano ya Muungano na ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inahoji misingi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kama nchi moja, mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, na mambo muhimu ya Muungano,” alisema Lissu na kuongeza:

“Katiba ya sasa ya Zanzibar inaelekea kuwa ni tangazo la uhuru wa Zanzibar zaidi kuliko waraka wa mwafaka kati ya vyama viwili (CUF na CCM) vilivyokuwa mahasimu.”​

Serikali itoe tamko kuhusu Zanzibar kujitangazia uhuru kutoka Muungano

Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alichambua vifungu mbalimbali vya Katiba ya sasa ya Zanzibar na kuitaka serikali kutoa tamko bungeni sababu zilizoifanya kuiruhusu Zanzibar kujinyakulia mamlaka juu ya mambo ya ulinzi na usalama ambayo alisema kwa historia yote ya Muungano yamekuwa ni mamlaka pekee ya serikali ya Muungano.

Alisema Katiba mpya ya Zanzibar siyo tu kwamba imetangaza uhuru wa Zanzibar kwa kuhoji misingi muhimu ya makubaliano ya Muungano, sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano, bali pia imehakikisha kwamba uhuru huo utalindwa dhidi ya tishio lolote la serikali ya Muungano.

Lissu alisema jambo hilo limefanywa kwa kuweka utaratibu wa kuwapo kura ya maoni ya wananchi wa Zanzibar kuhusu mabadiliko ya vifungu kadhaa vya Katiba ya Zanzibar.

“Kuweka masharti ya kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya vifungu vya Katiba mpya ya Zanzibar kuna athari ya moja kwa moja kwa uhai wa Muungano wetu. Hii ni kwa sababu hata vifungu ambavyo tumeonyesha kwamba vinakiuka misingi mikuu ya Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano haviwezi kubadilishwa bila ya kura ya maoni ya Wazanzibari,” alisema Lissu.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, masuala kama Tanzania ni nchi moja au la, majeshi ya ulinzi, polisi nakadhalika, ambayo yamekuwa mambo ya Muungano na Sheria ya Muungano siyo mambo tena ya Muungano hadi hapo wananchi wa Zanzibar watakapoamua kwa kura ya maoni kuyarudisha kwa mamlaka ya Muungano.

“Huku ni kutangaza uhuru wa Zanzibar bila kutaja neno uhuru. Huku ni kuua Muungano bila kukiri hadharani,” alisema Lissu.

Kwa mujibu wa Lissu, kwa mtazamo wa Katiba ya Zanzibar, Watanzania hawana tena nchi moja inayozungumzwa katika Katiba ya Muungano, bali wana nchi mbili.

Alisema kwa mtazamo huo huo, masuala ya ulinzi na usalama, polisi nakadhalika, siyo tena mambo ya Muungano kwa sababu kila nchi ina majeshi yake na kila moja ina Amiri Jeshi Mkuu wake.​

Tanzania kuna Marais wawili

Pia alisema Watanzania wana marais wawili, wakuu wa nchi wawili na viongozi wa serikali wawili. Alisema mambo yote hayo yanakiuka moja kwa moja makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano.

Lissu alisema kwa upande mwingine kwa mtazamo wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, Rais wa Muungano hana tena mamlaka ya kugawa mikoa na wilaya kwa upande wa Zanzibar na wala hawezi kumshauri tena Rais wa Zanzibar anapoteua wakuu wa mikoa wa Zanzibar.

Alisema pia Mahakama ya Rufaa ya Tanzania licha ya kuwa moja ya mambo ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Muungano, haina tena mamlaka ya kusikiliza na kuamua rufaa zinazohusu haki za msingi na uhuru wa mtu binafsi zinazotoka Zanzibar.​

Mtazamo wa Chadema kuhusu hali ya Muungano

“Kama ilivyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano umejitangazia uhuru, huu ni wakati mwafaka kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika,” alisema Lissu na kuongeza:

“Katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano siyo tu una serikali kamili, Bunge kamili, mahakama kamili, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, na sasa una nchi kamili yenye mipaka na eneo la bahari linalojulikana, una majeshi yake na Amiri Jeshi Mkuu wake, huu ni muda mzuri kwa serikali ya Tanganyika kuzaliwa upya.”

Alisema wanatambua kwamba sheria ya mabadiliko ya Katiba inaielekeza Tume ya Katiba kuongozwa na misingi mikuu ya kitaifa ya kuhifadhi na kudumisha kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.​

Jukumu la Tume ya Katiba

Lissu alisema hata hivyo, baada ya kujitokeza kwa wananchi wanaopinga kuendelea kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, alisema kwamba wale wanaopinga Muungano nao wajitokeze kutoa maoni yao kwa tume.

Kutokana na hilo, aliitaka serikali kutoa kauli mbele ya Bunge namna gani maoni ya wale wanaotaka alichokiita “kiini macho” cha Muungano kiishe yatashughulikiwa na tume ambayo imepewa jukumu kisheria la kuhifadhi na kukidumisha kiini macho hicho.

Alihoji ni kipi kitakachoizuia tume hiyo kupuuza maoni ya watu hao kwa hoja kwamba sheria inaielekeza tume kuratibu na kukusanya maoni na kutoa mapendekezo ya kuhifadhi na kudumisha Muungano.

Awali, Lissu alisema umefika wakati kwa serikali kuweka wazi nyaraka mbalimbali zinazohusu historia ya Muungano na mapato yake ili Watanzania waelewe masuala yote yaliyotokea yanayouhusu.

Alisema suala hilo ni muhimu kwa kuzingatia kwamba mataifa ya Magharibi kama vile Marekani na Uingereza yalikwishatoa hadharani nyaraka za mashirika yao ya kijasusi pamoja na balozi zao za Tanzania zinazoonyesha jinsi ambavyo serikali za mataifa hayo zilihusika katika kuzaliwa kwa Muungano.
 
Hii misemo mnaitoa wapi?mi nilijua tayari mtu kamwagiwa tindikali, unajua tena tangu uchaguzi wa igunga,COMMAND inaonekana ni wazee wa kumwagia watu tindikali
 
Ni halali kabisa bunge kujadili na kuchambua hotuba za upinzani badala ya bajeti za kifisadi maana kwenye hizo za upinzani ndiyo kuna issues za kujadili. NAUNGA MKONO HOJA YA UPINZANI!
 
Hata Mh.Nahodha aliunga mkono na kusema ni kweli tupu, ila si vizuri kuusema. Kwakweli hapo alinichanganya kidogo.
 
Hii lugha imenitisha, Pinda alisema liwalo na liwe Dr. Uli akatekwa na kuteswa, sasa uzi huu asije akauona ACP Msangi akaingia kazini na kumwagia tindikali kamanda Lissu, hawa wa Mabwepande akili zao ni kuiba, kutesa na kuua.
 
Tundu-Lisu.jpg

  1. Ataka Serikali ya Tanganyika irudi
  2. Asema Zanzibar ilijitangazia uhuru

Lissu awasha moto

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unakabiliwa na hatari kubwa ya kuvunjika kutokana na kitendo cha Zanzibar kujitangazia uhuru, na kwa hiyo ni wakati mwafaka sasa wa kuanzishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika. Msemaji wa Kambi kwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Tundu Lissu, alisema hayo wakati akitoa maoni ya kambi hiyo kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa mwaka 2012/2013, bungeni jana.

Alisema misukosuko ambayo imeukumba Muungano tangu mwaka 1964 hailingani na hatari kubwa inayoukabili hivi sasa. Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema jambo hilo waliwahi kumueleza pia Rais Jakaya Kikwete katika waraka wao wa Novemba 27, mwaka jana.​

Hatari ya kuvunjika Muungano
Alisema hatari ya kuvunjika kwa Muungano inatokana na mabadiliko makubwa ya kikatiba yaliyofanyika katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kutokana pia na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

"Hii ni kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya mwaka 2010, inaashiria tafsiri mpya ya Makubaliano ya Muungano na ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inahoji misingi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kama nchi moja, mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, na mambo muhimu ya Muungano," alisema Lissu na kuongeza:

"Katiba ya sasa ya Zanzibar inaelekea kuwa ni tangazo la uhuru wa Zanzibar zaidi kuliko waraka wa mwafaka kati ya vyama viwili (CUF na CCM) vilivyokuwa mahasimu."​

Serikali itoe tamko kuhusu Zanzibar kujitangazia uhuru kutoka Muungano
Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alichambua vifungu mbalimbali vya Katiba ya sasa ya Zanzibar na kuitaka serikali kutoa tamko bungeni sababu zilizoifanya kuiruhusu Zanzibar kujinyakulia mamlaka juu ya mambo ya ulinzi na usalama ambayo alisema kwa historia yote ya Muungano yamekuwa ni mamlaka pekee ya serikali ya Muungano.

Alisema Katiba mpya ya Zanzibar siyo tu kwamba imetangaza uhuru wa Zanzibar kwa kuhoji misingi muhimu ya makubaliano ya Muungano, sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano, bali pia imehakikisha kwamba uhuru huo utalindwa dhidi ya tishio lolote la serikali ya Muungano.

Lissu alisema jambo hilo limefanywa kwa kuweka utaratibu wa kuwapo kura ya maoni ya wananchi wa Zanzibar kuhusu mabadiliko ya vifungu kadhaa vya Katiba ya Zanzibar.

"Kuweka masharti ya kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya vifungu vya Katiba mpya ya Zanzibar kuna athari ya moja kwa moja kwa uhai wa Muungano wetu. Hii ni kwa sababu hata vifungu ambavyo tumeonyesha kwamba vinakiuka misingi mikuu ya Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano haviwezi kubadilishwa bila ya kura ya maoni ya Wazanzibari," alisema Lissu.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, masuala kama Tanzania ni nchi moja au la, majeshi ya ulinzi, polisi nakadhalika, ambayo yamekuwa mambo ya Muungano na Sheria ya Muungano siyo mambo tena ya Muungano hadi hapo wananchi wa Zanzibar watakapoamua kwa kura ya maoni kuyarudisha kwa mamlaka ya Muungano.

"Huku ni kutangaza uhuru wa Zanzibar bila kutaja neno uhuru. Huku ni kuua Muungano bila kukiri hadharani," alisema Lissu.

Kwa mujibu wa Lissu, kwa mtazamo wa Katiba ya Zanzibar, Watanzania hawana tena nchi moja inayozungumzwa katika Katiba ya Muungano, bali wana nchi mbili.

Alisema kwa mtazamo huo huo, masuala ya ulinzi na usalama, polisi nakadhalika, siyo tena mambo ya Muungano kwa sababu kila nchi ina majeshi yake na kila moja ina Amiri Jeshi Mkuu wake.​

Tanzania kuna Marais wawili
Pia alisema Watanzania wana marais wawili, wakuu wa nchi wawili na viongozi wa serikali wawili. Alisema mambo yote hayo yanakiuka moja kwa moja makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano.

Lissu alisema kwa upande mwingine kwa mtazamo wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, Rais wa Muungano hana tena mamlaka ya kugawa mikoa na wilaya kwa upande wa Zanzibar na wala hawezi kumshauri tena Rais wa Zanzibar anapoteua wakuu wa mikoa wa Zanzibar.

Alisema pia Mahakama ya Rufaa ya Tanzania licha ya kuwa moja ya mambo ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Muungano, haina tena mamlaka ya kusikiliza na kuamua rufaa zinazohusu haki za msingi na uhuru wa mtu binafsi zinazotoka Zanzibar.​

Mtazamo wa Chadema kuhusu hali ya Muungano
"Kama ilivyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano umejitangazia uhuru, huu ni wakati mwafaka kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika," alisema Lissu na kuongeza:

"Katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano siyo tu una serikali kamili, Bunge kamili, mahakama kamili, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, na sasa una nchi kamili yenye mipaka na eneo la bahari linalojulikana, una majeshi yake na Amiri Jeshi Mkuu wake, huu ni muda mzuri kwa serikali ya Tanganyika kuzaliwa upya."

Alisema wanatambua kwamba sheria ya mabadiliko ya Katiba inaielekeza Tume ya Katiba kuongozwa na misingi mikuu ya kitaifa ya kuhifadhi na kudumisha kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.​

Jukumu la Tume ya Katiba
Lissu alisema hata hivyo, baada ya kujitokeza kwa wananchi wanaopinga kuendelea kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, alisema kwamba wale wanaopinga Muungano nao wajitokeze kutoa maoni yao kwa tume.

Kutokana na hilo, aliitaka serikali kutoa kauli mbele ya Bunge namna gani maoni ya wale wanaotaka alichokiita "kiini macho" cha Muungano kiishe yatashughulikiwa na tume ambayo imepewa jukumu kisheria la kuhifadhi na kukidumisha kiini macho hicho.

Alihoji ni kipi kitakachoizuia tume hiyo kupuuza maoni ya watu hao kwa hoja kwamba sheria inaielekeza tume kuratibu na kukusanya maoni na kutoa mapendekezo ya kuhifadhi na kudumisha Muungano.

Awali, Lissu alisema umefika wakati kwa serikali kuweka wazi nyaraka mbalimbali zinazohusu historia ya Muungano na mapato yake ili Watanzania waelewe masuala yote yaliyotokea yanayouhusu.

Alisema suala hilo ni muhimu kwa kuzingatia kwamba mataifa ya Magharibi kama vile Marekani na Uingereza yalikwishatoa hadharani nyaraka za mashirika yao ya kijasusi pamoja na balozi zao za Tanzania zinazoonyesha jinsi ambavyo serikali za mataifa hayo zilihusika katika kuzaliwa kwa Muungano.

Mimi niliweka hotuba Nzima ya Mh. Lissu naona imeondolewa, hii inaleta HOJA inaleta mtafakuru
 
Wana JF wakati mwingine najiuliza hivi viongozi wanapojaribu kukwepa ukweli wanafanya hivyo kwa maslahi ya nani?
Zanzibar tayari wameshaamua kujitenga wameshakuwa na katiba yao na bado tunaendelea kuzungumzia muungano ni kujidanganya.Hebu tufikirie hatua mpya ya kuwa na serikali ya tanganyika, ya zanzibar na mwisho shirikisho kama inahitajika.
Nawaambieni wana JF.Mimi si mtabiri wala mpiga ramli lakini yakini nawaambia itawagharimu sana Wazanzibar kwa sababu hata mafuta wanayoyazungumzia kitaalamu yahitaji takribani miaka 6 kama yapo ndo waanze kuyaona wasifikiri ni kitu cha kusema kipo kikawepo.
 
Lissu.kama anataka Tanganyika atuonyeshe katiba ya Tanganyika

Sasa wewe unnataka akuonyeshe katiba ipi!!!!

Bunge liamue kisha tutengane ndipo upande wa Tanganyika watengeneze Katiba yao, kama walivyotengeneza WaZNZ.

KIYAMA YA CCM IMEFIKA!!!!!!!!

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Ka hili ka kuuchukia Muungano waziwazi ni moja ya mambo yanayowapunguzia credit...Watanzania wanawaona na kuwasikia mrengo wenu wa chokochoko kuanzia ile ya nchi haitatawalika, kuchochea social unrest etc.
 
Back
Top Bottom