Lissu kuitaka Tanganyika ni kosa ila Jussa kuitaka Zanzibar sio kosa?

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,034
Lissu aheshimiwe.

Lissu mara zote amekuwa akiipigania Tanganyika irudi na tuwe na muundo mwingine wa muungano, lazima mawazo ya Lissu yaheshimiwe na Lissu kuipigania Tanganyika anawakilisha mawazo ya watu wengi wanaoona nchi yao kupotea kiajabuajabu.

Ni muhimu sana Tanganyika irudi ili tuweze rasmi kuwa na muungano mpya au tubaki kama majirani wema ili Wazanzibari wabaki na nchi yao na Watanganyika wabaki na nchi yao ili maisha yaendelee.

Miaka ya nyuma Lissu alivaa hiyo tishirt akiwa Zanzibar, na tishirt hiyo inaonyesha Utanganyika wake na nchi ya asili yake.

IMG_1497.jpg
Bendera kwenye hiyo tishirt nyeusi ndio bendera ya Tanganyika,
 
Tanganyika ya nini sasa sisi tumezaliwa hiyo Tanganyika haikuwepo hizo ni porojo za wanasiasa wapate kula yao! Hivi seriously mi Tanganyika itanisaidia nn Bado nitakua hapa hapa
 
Lissu Aheshimiwe.
Lissu Mara zote amekua akiipigania Tanganyika irudi na tuwe na muundo mwingine wa muungano, lazima mawazo ya Lissu yaheshimiwe na Lissu kuipigania Tanganyika...
Nakuuliza hivi wale viongozi wa Chadema Zenji Hawa wanajiskiaje kujipendeleza Kwa.cha Cha wachagy?
 
Kama haufahamu Tanganyika ndio nchi yako halali una matatizo makubwa
Tuseme leo inaundwa serikali ya Tanganyika zaidi ya kuongeza ukubwa wa serikali na maumivu Kwa mlipa Kodi kuna jipya Gani? Jina Tanganyika lenyewe asili yake ni nini? Ni ukoloni. Tunaona fahari kuenzi miundo ya kikoloni?
 
Tuseme leo inaundwa serikali ya Tanganyika zaidi ya kuongeza ukubwa wa serikali na maumivu Kwa mlipa Kodi kuna jipya Gani? Jina Tanganyika lenyewe asili yake ni nini? Ni ukoloni. Tunaona fahari kuenzi miundo ya kikoloni?
Hao kina lissu wanajua ikiundwa Tanganyika hawakosi nafasi hii au ile sisi tunaopambana familia ipate msosi kuwe na Tanganyika au Tanga nini ni kazi bure
 
Tanganyika(Baba) + Zanzibar(Mama) = Tanzania(Ndoa) na inamiaka 59 sasa. Ups and down zipo ndio, ila hii ndoa ni ya milele daima amina. MUNGU IBARIKI TANZANIA, NA MBEGU ILE SAFI ULIYOIPANDA NDANI YAKE. SAMEHE YALE MAGUGU YALIYOPANDWA NA ADUI, KIPINDI CHA USIKU WAKATI MPANZI KALALA. MAANA HAYAJUI YALITENDALO.!
Muungano wa Kifala sana.
 
Back
Top Bottom