Hongera Tundu Lissu: Hoja ya kurudisha Tanganyika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Tundu Lissu: Hoja ya kurudisha Tanganyika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by masopakyindi, Jul 5, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,897
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Watanganyika tuwe na misimamo mingine ambayo ni ya kizalendo kama hoja hii ya Tundu Lissu Bungeni.
  Nmeipenda hoja ya Tanganyika.
  Kama Wazanzibari wameweza kujitoa katika muungano na wakawa na sera moja juu ya muungano(iwe CCM au CUF).

  Gazeti la Nipashe leo 5 Julai 2012, (uk. wa 4)lina kichwa cha habari:

  "Lissu ataka Serikali ya Tanganyika irudi

  Na Muhibu Said, Dodoma
  Kambi ya upinzani Bungeni imesema muungano wa Tanganyika na Zanzibar unakabiliwa na hatari kubwa ya kuvunjika kutokana na kitendo cha Zanzibar kujitangazia uhuru, na kwa hiyo ni wakati mwafaka sasa wa kuanzishwa tena kwa Seikali ya Tanganyika."

  Mh Lissu ametoa argument yenye mantiki ya kutosha Bungeni kutetea hoja hii.
  Kama walivyokubaliana kule Zanzibar(CCM na CUF) , kambi ya CCM Bungeni tunawaomba waone mantiki ya hoja ya Mh Lisuu katika hili suala la Muungano na hatma yake.
  Tanganyika inabidi irudishwe kutokana na yaliyotokea Zanzibar , na kuelekea kukubalika na viongozi wote.
  Wabunge wa CCM tafadhali walione hili bila woga.
  Nawasilisha
   
 2. m

  mwelimishaji Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanganyika wapewe uhuru wao. Kwa Muda mrefu Tanganyika imejulikana kama Tanzania bara wakati huo huo Zanzibar imeendelea kuitwa Zanzibar. Ni rahisi kusikia Tanzania Zanzibar lakini kamwe hutosikia Tanzania Tanganyika. Tujiulize hivi tanganyika tuna shida na watu wasiotuhitaji? Hivi sisi hatupendi kutambuliwa na kuthaminiwa kama wazawa wa Tanganyika? Sioni faida ya muungano huu ila naona hasara nyingi sana.
  Sipendi kujikomba kuomba urafiki na mtu asiokupenda na haswa anayedai kuwa unamnyanyasa. ZANZIBAR IBAKI KAMA JIRANI KAMA ZILIVYO NCHI ZINGINE TUNAZOPAKANA NAZO.
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  Magamba hawawezi kukubali kwani wanapata wabunge wa bure toka Zenj over 50. Na wanajua wabaya wao hawawezi. Ukweli ni kwamba Zenj ikitoka 2015 huku Tanganyika lazima wamwagwe
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,832
  Trophy Points: 280
  Ati tunaitwa TANZANIA BARA.......bara vipi wakati tuna beach kibao
   
 5. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,672
  Trophy Points: 280
  Na kama ni muungano kuvunjika na iwe hivyo kabla ya 2015 sababu CHADEMA itakaposhinda Bara na CCM kushinda Zenji sipati picha kama huo mseto wa muungano utakuwa vp?
   
 6. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,143
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Ningependa sana endapo muungano huu ungevunjikia mikononi mwa CCM. Tunahitaji Tanganyika yetu. Tumefanywa nchi ya kufikirika kwa miaka mingi wakati wazanzibari bado ni taifa huru lenye sifa zote za kuwa taifa huru. Wacha tubaki kama majirani wema lakini kila nchi iwe taifa kamili.
   
 7. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Watakubali tu, upepo wa kisulisuli inaivizia CCM.
   
 8. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Itakuwa poa sana, lakini mwisho chumbe.
   
 9. m

  mob JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  tanganyika freedom is coming soon
   
 10. M

  Mr. Teacher JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 330
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Nilisikitishwa sana jana na kauli za Vuai Nahoha na Fredrick Werema wakati wakijibu hoja za Mh. Lissu kuhusu hotuba yake abt muungao. Jambo la kwanza nlilojifunza ni kuwa serikali ilipanic sana kutokana na hotuba ya Lissu, hadi ikabidi wajipange watu wengi kumjibu!!!la pili ni ujinga kujibu hoja bila kufikiri, eti Nahodha anasema si vizuri kusema ukweli kila wakati, kha, hii ina maana govt huwa inatudanganya kwenye mambo mengi tuu!!!!!!

  Lakini cha zaidi huyo Nahodha anatetea kitu asichikiamini, yeye ni mmojawapo wa watu watata abt Muungano, ila b'se ni minister anajifanya kutetea mambo ambayo anajua ukweli ambao hawezi kuusema hadharani!!!! werema nae na mashaka na taaluma yake ya sheria, ni ujinga kupinga points amabzo ziko wazi kabisa from Lissu!!!

  Na Chiligati nae anatetea ujinga, eti Z'bar ina jeshi gani, hivyo vikosi vina uwezo gani kivita!!! anasahau kuwa hata M'buyu ulianza kama mchicha!!!!!lakini cha zidi jamani, Z'bar wanapokuwa now wana makamu wa rais wawili kiitifaki inakuwaje? Wanakuja bara na kupewa heshima zote kama viongozi wa kitaifa wakati katiba ya muungano haiwatambui, remember katiba ya sasa muungano inamtambua waziri kiongozi; halafu hapo unasema katiba ya muungano haijavunjwa? kha!!! hapa ni kuangalia facts ni sio kuangalia vyama, ktk hili siko pamoja na wana CCM wenzangu!
   
 11. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,897
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kumpinga Tundu Lissu bila sababu ya msingi, Mwanasheria Mkuu, Jaji Werema amekiri kuwa HATA YEYE hajaliona tamko hilo la maadishi ya kuridhia muungano.
  Mbaya zaidi sidhani kama anazo hadidu za rejea kwa yaliyo kubaliwa kati ya CCM-Zanzibar na CUF-Zanzibar.
  Na hapo ndio nasema CCM-Tanganyika imewekwa rehani katika muungano, ni wakati muafaka sasa kuirudisha ili tusiendelee kududumia Zanzibar kwa kodi zetu.
   
 12. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyu Chiligati si ni kama mzee wa Manzese anayebishana mambo ya Simba na Yanga. Yupo yupo tu Hana umuhimu wowowte kwenye nchi hii
   
 13. i

  integralboy Member

  #13
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nampa hongera sana mheshimiwa tundu lisu
   
 14. m

  maswitule JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,385
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hakika hata mimi pale waziri wa Muungano aliposema Zanzibar ni nchi, nilishindwa kumulewa maana alisema kama kuna Muungano wa nchi mbili basi Zanzibar ni nchi nikajiuliza na nchi ya Pili ni ipi bila Shaka ni Tanganyika, na nikajiuliza sasa Tanzania ni nini basi? Shirikisho Kama East Africa community?

  Nadhani wanatupotosha wengi tunachojua Zanzibar na Tanganyika Zilikuwa nchi zikaungana na kuwa Tanzania. Hivyo nchi ni Tanzania na si Zanzibar au Tanganyika?

  Wataalamu wa siasa watusaidie kwenye hili maana hata Pinda aliwahi kusema Zanzibar si nchi na ikaonekana hakukosea sasa iweje leo tena waziri wake aseme ni nchi
   
 15. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ukishindwa kujibu hoja una kimbilia kudai msemaji hana elimu ya kutosha.

  Hiyo kitu Wazungu wanaiita Character Assanination

  Badala ya kushambulia hoja unashambulia mtu.


  Janja ya CCM kwisa jua.
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  CCm haijawahi kushinda zanzibar hata siku moja...
   
 17. I

  IAN ULOMI Member

  #17
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabisa tunataka tanganyika yetu.
   
 18. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii hoja ya Utanganyika inakubalika na M4C wakijikita nayo Gamba lazima nao wataigeukia kama ilivyokuwa ya mabadiliko ya katiba yahani sasa hivi jipu limebata mkunaji we ni kuswitch utaona watu wanavyoropoka
   
 19. M

  Mzenji73 JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  am JUST loving this!! heko Mh Lissu .... msaada wenu wahitajika kufikia matakwa ya walio wengi wetu
   
 20. l

  lum JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  sisi wazanzibari ngoma yetu ya kibati tushaicheza toka 2010,na ndio imewafanya watanganyika kuja na mzimu wa katiba mpya,mabadiliko ya 10 yamewafanya sasa waamshe ngoma yao ya kimasai,sasa wacha tuangalie wanavyocheza huku wakikosana mikuki ha ha ha ha ha.

  kilichokuwa kikifanyika na Uamsho wenyewe wenye lugha wanakiita ‘negotiating from a strong position' Mara hii lazima muone joto ya jiwe watu wa upande wa pili\(watanganyika); mambo ndio kwanza yanaanza mushaanza kupatwa na baridi. HATA BADO MWISHO MTATAFUNANA WENYEWE..
  Sisi tunawaambia…
  Zanzibar kwanza

  niliwaambia siku za nyuma humu UAMSHO ni chombo tu cha usafiriiiii imepewa kazi ya kufunga chapter ya mwanzo ya zanzibar mpya na kufungua ya pili na katika kutekeleza majukumu yake kuna steps za kupitia na hakuna wa kuwazuiya znz.WAZANZIBAR NI WATAALAMU WA FANI YA SIASA njonii mjifunze nyinyi watu..
  sasa tumewatia tanganyika kwenywe micrometer gauge''TUNAWATAZAMA KWA MAKINI'' tunawasaidia kutunga katiba ya tanganyika tukimaliza mtakwenda wenyewe NEW YORK kushusha lile tambara la muungano,

  CHEZEA WAZANZIBAR NYIEEEE
   
Loading...