Hongera tff | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera tff

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Ruttashobolwa, Mar 13, 2012.

 1. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,699
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Nachukua nafasi hii kuwapongenza TFF kwa kuwachukuli hatua za kinidhamu wavunjifu wa amani kwenye mpira wa miguu. si wengine ni yanga ambao walionekana kuwa tyson dhidi ya refa ,hivyo basi wachezaji wapatao watano wa yanga awataonekana uwanjani mpaka msimu unaisha,pia yanga wamepigwa faini isiyopungua mil 4. nafikiiri hii ni funzo kwa wote maana watoto ujifunza kutoka kwa wakubwa. jamani ni dhamu ni chachu ya maendeleo.
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,532
  Trophy Points: 280
  hii ni nzuri,
  mpira wacheze wao, ngumi wao
  wengine watafanya nini.
   
 3. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mchezaji ambae hatacheza msimu mzima ni Stephano Mwasika ambae amefungiwa mwaka mmoja. Nadir Haroub Cannavaro na Jery Tegete wamefungiwa mechi 6(watacheza mechi mbili za mwisho).Omega Seme na Nurdin Bakari wamefunghwa mechi tatu( watacheza mechi tano za mwisho) Klabu imepigwa faini ya milioni nne. Anyway siwasapoti wachezaji wa Yanga kwa utovu wa nidham walioufanya lakini haya maamuzi ya marefa wetu yanasababisha vurugu hizi zitokee. TFF na kamati ya waamuzi inabidi warekebishe mapema tatizo hili vinginevyo maafa kama ya Misri yanaweza kutokea hapa Bongo. Haileweki kuwa maamuzi haya ya utata ya Marefarii wetu yanasababishwa na kiwango duni cha Marefa au kuna manufaa binafsi wanayopata kutokana na maamuzi hayo ya utata. Unaweza kuwalaumu wachezaji wa Yanga kwa nidham mbaya walioionyesha lakini ukifuatilia malezi ya wachezaji wetu toka utotoni utagundua kitu. Namalizia kwa kusema kuwa kwa Maamuzi kama yale na malezi ya wachezaji wetu na watazamaji wengi wanaokuja uwanjani tunategesha bomu ambalo siku yoyote linaweza kulipuka. POLENI YANGA..
   
 4. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Aiseee,nimeipenda hii,labda nidham ya mpira itarudi maana!
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Wanajisahau na kufikiri wapo nje ya sheria..fine ni ndogo hiyo pia kama club ilitakiwa iwe fined kama walivyoadhibiwa Simba kwa makosa ya Simba fans
   
Loading...