Dunia nzima imeona,ningeshangaa sana kama TFF ingekaa kimya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dunia nzima imeona,ningeshangaa sana kama TFF ingekaa kimya

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Oct 6, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kama ilivyotarajiwa na wengi wale wachezaji wa kukodi No. 12 na No. 13 waliowawezesha Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Tanzania Bara Simba S.C kutoka droo ya goli 1 - 1 na Mabingwa wa kusakata kabumbu ukanda mzima wa Africa ya Mashariki mpaka kule kwa nchi waalikwa Dar Yong Africans wameadhibiwa na Shirikisho lenye dhamana ya kuendesha mchezo huo hapa nchini kwa kuvurunda, wakati Akrama (Pichani chini) akiondolewa kabisaa kwenye Ligi Msaidizi wake Mzee wa offsides yeye amepewa onyo kali,habari kamili hii hapa:-

  [​IMG]
  Na Prince Akbar wa Bin Zubeiry
  KAMA ilivyotarajiwa na wengi, refa Mathew Akrama wa Mwanza aliyechezesha ovyo mechi ya watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga, Jumatano wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ‘amekwenda na maji’.
  Taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura imesema kwamba, Kamati ya Ligi imewaondoa marefa watatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na kuvurunda.
  Mbali na Akrama ambaye ‘Yanga hawana hamu naye’ tangu siku hiyo, wengine ni Paul Soleji wa Mwanza aliyechezesha mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons, na mwamuzi msaidizi namba mbili kwenye mechi hiyo Mwarabu Mumbi wa Morogoro, wakati mwamuzi msaidizi namba mbili wa mechi ya Yanga na Simba, Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam amepewa onyo.
  Kamishna wa mechi namba 28 kati ya Yanga na African Lyon, Pius Mashera ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi hiyo kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (Pre match meeting) na uwanjani.
  Vilevile Mashera kwenye ripoti yake aliwasilisha malalamiko dhidi ya msimamizi wa kituo cha Dar es Salaam, na kwa vile suala hilo ni la kinidhamu ametakiwa alipeleke kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
  Nayo Simba imepigwa faini ya jumla ya sh. 600,000 kwa kuchelewa kufika kwenye pre match meeting ya mchezo wao dhidi Tanzania Prisons (sh. 100,000) na kwa washabiki wake kuwatupia chupa za maji waamuzi wa mechi hiyo (500,000).
  Pia Kamati ya Ligi imeagiza kuwa kwa vile suala la kipa Shaabani Kado wa Mtibwa Sugar kudaiwa kumpiga kiongozi mmoja wa Ruvu Shooting mara baada ya mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex ni la kinidhamu lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
   

  Attached Files:

 2. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Haya sasa kiko wapi,fedha za yule "Mhaini" zimekuponza,kafie mbele huko!
   
 3. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  "mhaini"
   
 4. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Humfahamu? wee endelea kushangilia usajili mzuri tu
   
 5. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Yule refa ni matapishi kabisa, amekataa goli saaafi la kavumbago .Na yule yondani wa simba (mshika kibendera) achunguzwe vizuri atakuwa kapokea kitu .
   
 6. M

  Masuke JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Marefa mnawachagua wenyewe ili wawabebe, kawabeba hambebeki sasa mlitaka achukue mpira yeye mwenyewe autumbukize kwenye kamba ndo mngeona ni refa bora, timu yenu mbovu ile si ya kulipa tano kajipangeni tena acheni kubwabwaja, Huyo Bahanuzi wenu muda wote yuko nyuma ya mabeki unategemea nini? Na kama ataendelea hivyo hivyo ataishia kufunga magoli ya penati tu lakini ya move atayasikia kwa akina Sunzu, Okwi, Ngasa na Boban.
   
 7. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Dawa ni kuchukua hatua haraka sana bila kupoteza muda. Mechi kubwa kama ile unawezaje kutuonyesha kuwa HUNA AKIRI?
   
 8. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Cwaelewi mna matatizo gani yanga katimu kadogo huezi linganisha na Simba haaaa
   
 9. chamakh

  chamakh JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 692
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 60
  kwanza TFF wachemfu sana ilikuwaje waruhusu huyu refa achezeshe mechi mbili za Yanga mfululizo? yaani baada ya kuwabeba na African Lyon wakamuona anafaa sana kuibeba Yanga

  pili, huyu refa **** sana, kainyima simba penati ya dhahiri baada ya dogo edward christopher kumpiga chenga tutusa twite, dogo kaingia kwenye 18 nadir haroub kamvuta, penati hasa yeye akadai kajiangusha, angejiangushaje wakati beki yuko nyuma yake? **** kwelikweli

  tatu, mwinyi kazimoto kachezewa faulo ya dhahiri kama sio ndani ya 18 basi ilikuwa just outside of the box(at the edge) yeye hata faulo hakupiga maana yake nini kama sio kuibeba yanga?

  nne, ,mechi imeongezwa dakika 5 kwa kuwa berko alijifanya kuumia, yeye akachezesha tatu tu kwa nini?
   
 10. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Afadhari yule mshika kibendera nae hana kazi?
   
 11. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,721
  Likes Received: 7,982
  Trophy Points: 280
  Tofautisha kumvuta jezi na kumshika jezi. Wachezaji hugusana, hushikana na hupushiana. Inategemea amevutwa kwa kiasi gani. Hiyo jezi hata haikuwa stretched utasemaje alivutwa?

  Mshukuruni yule mshika kibendera asiye na haya anayenyoosha bendera kila anpoona rangi ya kijani baada ya kupewa hela
   
 12. m

  mourad77 Senior Member

  #12
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 178
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MHAINI Ni Hans pope mwenyekiti wa FOS Freinds of simba si alipata kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa lakupanga kupindua nchi na kumua rais wa wakati huo HAYATI jk nyerere ila mwaka 1994 mwinyi alimtoa gerezani ndio maana anaitwa MHAINI Sababu kesi yao ilikuwa ikitajwa kama KESI YA UHAINI Na hivyo basi bado anaendeleza UHAINI Wake kwenye soka letu kwa KUHONGA Waamuzi
   
 13. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  Na ile kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa yanga unaizungumziaje?

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 14. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  ile kadi ni halali coz katenda kosa la 2 palepale mbele ya refa wakati anapewa yellow card
   
 15. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Asante Kaka kwa kunisaidia kuwaelezea hawa Watindiga(Wapenzi wa Simba) wa kizazi cha 1990s wasioijua Historia ya nchi hii, wao kazi yao ni kushangilia usajili wa kina Ngassa,Akuffor na wengineo tu uliofanikishwa na yule Mhaini...sijui hata nani alimfungulia bora angeishilia kulekule
   
 16. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  chamakh hivi mechi uliiangalia au umesoma kwenye lile gazeti la Msimbazi?, mana'ke wewe ndo mtu wa kwanza wa Simba kulalamika mechi iliongezwa dakika 3 badala ya 5,wenzako wote walikuwa wanaomba hata dakika zisiongezwe jinsi hali ilivyokuwa tete kwa upande wenu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Unafikiri hawamjui mhaini wao! wanamjua sanaaaa!
   
 18. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  wangemfungia na yule mnywa viroba BABOON!
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Soka la bongo fitna kubwa kabisa!!wamejaa mafisadi wa soka na wanunua marefa,wachezaji ili kuboronga na kuhujumu mechi!woote wanajulikana!
   
 20. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Eti wamempa onyo kali....
   
Loading...