Utetezi wa Yanga na wachezaji wake kwa TFF na Mashitaka Juu ya Refa Mu-Israel Mkongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utetezi wa Yanga na wachezaji wake kwa TFF na Mashitaka Juu ya Refa Mu-Israel Mkongo

Discussion in 'Sports' started by mtx2006, Mar 16, 2012.

 1. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana Jamii na wapenzi wa mpira nchini.
  Kwako TFF.

  Nawasilisha utetezi wangu kwako kuwahusu wateja wangu Yanga na wachezaji wake watano uliowapa adhabu hivi karibuni. Yanga anahusika kwa vile umemnyima haki ya kuwafanyisha kazi waajiriwa wake halali kwa vipindi mbali mbali.

  Utetezi wa 1: Ukubwa wa adhabu
  Bila kujali kama wamefanya kosa au la napenda nawasilisha utetezi kuwa adhabu uliowapa ni kubwa sana na inaonyesha kuwa na agenda nje ya kosa lenyewe. Kwa kawaida unapotaka kumhukumu mtu yeyote aliye fanya kosa, lazima utumie sheria, kanuni zilizopo bila kusahau hukumu ulizokwisha pitisha kwa wengine waliofanya makosa kama hayo. Napinga ukubwa wa adhabu kwa wachezaji wa Yanga kwa kutumia hoja ya hukumu ulizowahi kupitisha kama ifuatavyo:

  1. Katika mchezo dhidi ya Simba na Oljoro JKT mchezaji Patrick Mafisango alimsukuma mwamuzi Isihaka Shirikisho baada ya kumuonesha kadi nyekundu mchezaji mwenzake Haruna Moshi. Kamati yako iliamuadhibu Mafisango kwa kuamuru simba imwandikie barua ya onyo kali kwa kitendo chake hicho ambacho kinafanana sana na hiki cha wateja wangu. Source:Mafisango Aonywa, Simba Yapigwa Faini . Au tuseme ni kwa vile ulikosa ushahidi wa video kutoka redio clouds ukimuonyesha mafisango akikimbia kutoka mbali sana kama alivyofanya mchezaji wa Yanga, na kuja kumsukuma mwamuzi?

  2: KIPA Juma Kaseja wa timu ya Simba alionyesha utovu wa nidhamu cha kugoma kupeana mkono na aliyekuwa mgeni rasmi katika mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Kamati yako ilimuadhibu kwa kumfungia mechi tatu na faini ya shs 500,000. Ndio tuseme Refa ni zaidi ya mgeni rasmi?

  3. Mchezaji Aziz Sibo wa African Lyon alifungiwa kutocheza mechi tatu na faini ya sh 500,000 kwa kosa la kumtandika kichwa mchezaji wa Polisi ya Dodoma

  source:TFF yatoa adhabu kwa watovu wa nidhamu


  Kesi kama hizi ziko nyingi ambazo kumbukumbu zake unazo. Kwa hoja hii naomba utengue uamzi wako wa kuwafungia wachezaji wa Yanga zaidi ya mechi tatu.

  Utetezi wa 2: Kuwanyima nafasi ya Kujitetea
  Ni kitendo cha haki kumsikiliza mtuhumiwa kabla ya kumpa adhabu. Kitendo hiki sio tu kinatoa haki bali pia uwezesha wenye mamlaka kugundua tatizo la ndani ambalo ni kiini cha tatizo lililotokea. Kwa vile wateja wangu hawakupata haki hiyo naomba utengue hukumu yako mara moja.
  Hii ni sawa na kesi iliyokuwa inawahusu Rage na Sendeu kwa kitendo chao kilichodhaniwa ni kuhujumu mechi. Pamoja na kwamba walisikika redioni wakieleza nia ya kugomea mchezo bado kamati ya Tibaigana iliwataka walete maelezo ya kujitetea kabla ya kuwahukumu.
  Source:Tibaigana kuwahoji Rage, Sendeu

  Utetezi wa 3: Uhalali wa Kamati iliyotoa hukumu.
  Kamati iliyotoa hukumu ni kamati ya ligi ambayo hata kama inayo mamlaka bado ina wajumbe ambao wana Conflict of Interest katika hili swala, mfano Nyange Kaburu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Simba, timu pinzani na wateja wangu. Kwa hili pia naomba adhabu itenguliwe mara moja.

  Utetezi wa 4: Kutompa adhabu refa.
  Refa wa mchezo huo alionekana wazi kushindwa kumudu mchezo na hivyo kusababisha fujo. Mfano alimpa Niyonzima kadi kwa kosa la kumtukana, kosa ambalo ni lakufikirika zaidi na kanuni zinamtaka refa kuweka kosa hilo kwenye ripoti ili mchezaji husika achunguzwe. Refa pia alishindwa kumpa mchezaji wa Yanga, Mwasika kadi nyekundu pamoja na kumbughuzi wakati wa mchezo. Refa alishindwa kuwaadhibu wachezaji wa Yanga kwa rafu mbaya walizo kuwa wanafanya. Refa alishindwa kumpa kadi Tegete kwa kosa la kuingia uwanjani. Refa alishindwa kuwahusisha waamzi wenzake ili kuweza kufanya maamzi yasiyo na shaka n.k.
  Mfano wa kesi kama hii upo, na kamati hiyo hiyo ilishawahi kuwafungia waamuzi Peter Mujaya wa Mwanza aliyechezesha mechi namba 101 kati ya JKT Ruvu Stars kwa miezi 12 kwa kushindwa kumudu mchezo, kumuondoa Isihaka katika orodha ya waamuzi kwa kushindwa kumuadhibu Mafisango ambaye alimsukuma baada ya kumuonesha kadi nyekundu Haruna Moshi wa Simba.

  Ndio kusema Mu-israel Mkongo alimudu mchezo? aliwaadhibu wote waliohusika na rafu mbaya?....
  Source: Waamuzi, Kamishna Waondolewa VPL

  Utetezi wa 5: Ushahidi uliotumika
  TFF wanadai waliweza kubaini waliofanya fujo kwa kutumia ushahidi wa video ulioonyeshwa na TV hususa ni CloudsTV ambayo ililipigia debe sana swala hilo. Katika technologia ya leo chochote kinaweza kufanyika ikiwemo ku-edit picha na video ili kujenga hoja ya jambo ambalo mwandishi wa habari anataka watazamaji waelewe. TFF inapaswa kutumia video ambazo hazija editiwa na ambazo zinatoka kwenye source ambayo haiponyeshi mgongano wa kimaslahi hata chembe kama ilivyo CloudsTV ambayo mtangazaji wake wa kipindi ni kiongozi wa Simba.

  Utetezi wa 6: TFF kupuuza malalamiko ya Yanga kuhusu kuongwa kwa Refa
  Wateja wangu waliwaletea malalamiko kuwa wana wasiwasi na refa wa mchezo huo ambaye anaonekana kama ameongwa na timu ya Azam ili atoe maamuzi ambayo sio sahihi. La kushangaza TFF hamkuchukua hatua yoyote na kusababisha mchezo kuvurugika. Mfano ni case ya Arsenal na Barcelona ambapo mwamuzi aliyetazamiwa kuchezesha mechi kati yao ya UCL alionekana mitaani huko kwao amevalia fulana ya Barcelona. UEFA ilisikia malalamiko hayo na kumuondoa huyo mwamzi mara moja. Najua kwa kufanya hivi kunaweza kusababisha kila timu kulalamikia mwamzi, lakini kwa kuiga wenzetu, TFF inaweza kumuondoa refa anayelalamikiwa na kuomba mlalamikaji alete ushahidi, na endapo akishindwa basi achukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kulimwa faini.

  Kwa utetezi huu naomba wateja wangu waondolewe adhabu mara moja na Mwamuzi afungiwe maisha kujihusisha na mchezo tunaoupenda wa mpira wa miguu. Naomba niseme wazi kuwa hata mimi sifurahi vitendo vya kupigana uwanjani, lakini nachelea kusema kuwa TFF ndio inachochea kwa kufanya Timu na wachezaji kuona kuwa hakuna anayewasikiliza pindi wanapotoa malalamiko yao kuhusu marefa.

  Napenda pia kuwaomba TFF waanzishe uchunguzi kuhusu AZAM maana imelalamikiwa na timu zaidi ya 5 kwa vitendo vyao vya kuwashawishi marefa kutoa maamuzi mabaya.

  Nawasilisha utetezi.
  Wakili wa Kujitolea
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Umesomeka Mkuu
   
 3. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,151
  Likes Received: 2,195
  Trophy Points: 280
  Kama uwakili ndo huu naapa hii sheria nnliyosoma naijivua,kifupi mkuu umedhalilisha taaluma yetu,hata kwa hakimu mwnye diploma awezi ruhusu kufunguliwa kesi kama hii isiyo kua na muelekeo.nnamashaka na uwakili wako,inawezakana we ndo wakili wa tanesco.
   
 4. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Yes nakumbuka tukio la kaseja kuadhibiwa kwa kutopeana mkono na mgeni rasmi.lakini bdae clouds walimtetea na adhabu ile ikatenguliwa.nahisi tff wanapangiwa nini la na clouds.
  **but kisheria adhabu ya mchezaji kumpiga refa ni miezi miezi3 hadi mwaka 1.na si zaid ya hapo.sasa je mwasika angempiga refa kwa mangumi na mateke au na siraha juu yake angepewa adhabu ipi?
  ***kuhusu tegete,huyu ndo ameonewa kuliko wote coz adhabu ya mchezaji au kocha kuingia uwanjani ni rnd card.ambapo anatakiwa akosn mechi1 tu. Lakn hayo hao clouds hawataki kuyadiscuss.
  ** refa hakumpa red card police alieingia uwanjani bila ruhusa.refa akitoka nje ya uwanja amevunja mechi but yy alikimbilia nje.
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wakili wa kujitolea, mimi si mwanasheria ila naipenda sana hiyo fani. Sina mashaka na uwezo kisheria maana kwa ulivyoandika wewe ni mtalaam mzuri wa sheria ila unakosa due diligence na objectivity. Unatetea mambo kwa kutumiwa kwa maslahi binafsi. Unachokosa kingine ni uzoefu katika soka na mfano ulioutoa wa arsenal vs barca ni wa kusimuliwa. Nikukumbushe kuwa katika masuala yote ya uhalifu au kuvunja sheria/kanuni kinachojadiliwa ni EVENT na wala siyo CAUSE. Ningekuona wa maana kama ungeanza kwa kulaani kitendo cha wachezaji na viongozi wako waliokupa hiyo posho uwatetee. Na wewe na usomi wako unatoa maneno yale yale kama ya wazee wa yanga. Ulipaswa ujiweke kando na kauli za wazee wa yanga.
  Kwamba nilibaka kwa sababu..........
  Niliiba kwa sababu..................................
  Nilimpiga kwa sababu...........................
  dont jeopadize your professional bana!
   
 6. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  kuhusu CAUSE AND EVENT unakumbuka zidane alimpiga vichwa materazi,na fifa baada ya kugundua kua materazi alikua anamtolea zidane lugha chafu na za karaha,walimfutia adhabu na zaidi ya hapo wakamhadhibu materazi.same to mkongo ambae anaye anarugha chafu.hata edo kumwembe alizungumzia yuliyomkuta kutoka kwa huyu refa wakati wa mechi ya kosti jinsi alivovomtukana
   
 7. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  yaani ndo unazidi kunitia hasira tu. Nijibu kwa kifupi, wachezaji wa yangu walikuwa na haki ya kumpiga mwamuzi?
  Halafu wasipewe adhabu eti kwa sababu kuna mchezaji mmoja alishawahi kufanya kosa kama hilo na hakupewa adhabu kama walizopewa wachezaji wa yanga? Wewe sio wakili ni wakula
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kamavipi wafungiwe kabisaa hatupendi miugomvi isiyokuwa na maana mbona niyonzima alipopewa kadi aliondoka bila ya fujo yoyote..
   
 9. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ningekuheshimu kama ungetumia utaaluma wako kupangua hoja baada ya hoja kuliko kusema unachosema. Jenga hoja na wewe kama unataka kuliko kujisemea tu.
   
 10. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  sheria ndivyo ilivyo. hukumu moja inajenga msingi wa maamuzi yanayofuata. fair play ndugu yangu ipo kwenye maamuzi
   
 11. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Mimi kama wakili maslahi yangu ni wateja wangu waepuka adhabu . nashangaa unapoukataa mfano wa refa wa arsenal na barca. huwezi ku google tu mara moja kuhakikisha kabla ya kubisha. polisi unaniangusha. siku zote nyie mapolisi mnatupa shida sana sisi wanasheria ujue kwa kutojua kwenu mambo muhimu
   
 12. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Simba na Yanga zinaua mpira wa Tanzania na kinachosubiriwa ni kifo tu cha soka. Kila idara inayohusu soka kuna mwana simba au yanga anayetaka timu yake ipate upendeleo au anatumia mamlaka yake vibaya kuzipendelea. Matokeo yake ni kuwa timu zingine zinanyimwa haki na hazipati manufaa ya uwekezaji katika soka. Na kama Azam wamejiingiza katika mkumbo wa kuhonga waamuzi basi ujue soka limeoza. Kuna haja gani ya kuwekeza katika mfumo rushwa? Nchi ya hovyo huishia kufanya vitu vya hovyo katika kila jambo
   
 13. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  hii hoja kuwa yanga na simba zinaua mpira wa nchi hii nimeisikia sana. lakini ukiuliza kivipi mtu atakwambia mambo ambayo kama una watu makini ndani ya tff na viongozi bora katika yanga na simba unaweza kuyadhibiti kabisa. mfano kwa nini tff isiwaunganishe viongozi wa yanga na azam kwenye hizi fujo. mimi nimewakwepa viongozi wa yanga kwa vile ni wateja wangu lakini wanatakiwa walete ushahidi walio nao kuhusu tuhuma za azam kumhonga refa jambo ambalo pia ndilo lililofanya wachezaji wa yanga kuamini wanaonewa na refa.
   
 14. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Sasa huyo boxer Mwasika kapewa adhabu gani? Mbona tunapenda kutetea ujinga?
  Kitendo walichokifanya wachezaji wa Yanga ni cha AIBU sio kwa klabu yao tu bali hata kwa taifa zima. Hii inapaswa kuwa funzo kwa mchezaji yoyote mwenye mawazo ya ki Mwasika aachane nayo mara moja.
   
 15. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  hoja hapa ni kwamba kutokuwa makini kwa kamati kuadhibu vitendo hivi huko nyuma kwa mujibu wa kanuni kumewafanya baadhi yao kutafasiri kuwa adhabu ya matendo kama haya ni ndogo. pia kuondoa double std wateja wangu nao hawapaswi kuface adhabu hiyo. kwenye kesi nyingine kamati ya tibaigana iliwahi kumpunguzia mchezaji adhabu kama hii kwa madai kuwa itaua kipaji na ajira yake.
   
 16. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kama kazi yako ni kutetea basi ungesema wachezaji wa yanga hawajampiga mwamuzi na ukatetea kuliko huu utumbo unaotulazimisha tuamini. Mpira unachezwa kwa miguu kama vipi washauri waende kwenye ndondi kama huko wanapaweza zaidi
   
 17. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  sijakulazimisha kuamini ila nimejenga hoja kwa misingi ya utawala wa sheria. kama ni hivyo si zombi angefungwa tu. tusizoee kudiscuss bila hoja kama walevi. nia hapa ni tff kuexplore udhaifu uliopo ili kuweka policy zitakazotawala mchezo bila kujali ni timu ipi. sawa afande!
   
 18. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nimekugundua kitu kwenye hii thread, wanazi wa Yanga wanamkubali huyu wakili. Lakini wanazi wa simba wanapinga.
   
 19. S

  SURN JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yanga fara 2 ingawa na mimi ni yanga
   
 20. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  sheria za FIFA zinasemaje kwa songombingo kama ile...
   
Loading...