Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, vyombo vyetu vya habari hasa television vimeshindwa kuwaonyesha watanzania mechi ya mpira wa miguu kati ya timu yetu ya Taifa (Taifa Stars) iliyokuwa ikicheza dhidi ya Moroco.
Wakati vituo vya binafsi vikiendelea kurusha vipindi vyao vya kawaida, Television ya Taifa (TBC) wao walijikita uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kurusha matangazo ya moja kwa moja juu ya ujio wa raisi wa China.
Hivi kweli watanzania tumefika mahali pa kuwathamini wageni kuliko timu yetu ya Taifa? Naamini watanzania walioko Tarime, Tandahimba, Kakonko, Pemba, Namanyele ama Tunduru wangetamani kuishuhudia timu yao ya Taifa kuliko raisi wa China asiye na maslahi yoyote na maisha yao.
Ni dhahiri kuwa viongozi wetu wa sasa wameishiwa kabisa na uzalendo, na ndio maana wanaendelea kufanya mambo ya kijinga huku wananchi wakiwakodolea macho bila kuchukua hatua.
Unampa hongera kwa kushika mimba na kuikubali maana wengi wanatoa angali changa. Na akijifungua unampa hongera kwa kupata mtoto!Ni sawa na mama mjamzito unamwambia hongera wakati bado hajajifungua?
Tz 3 Mor 1.
Samata 2
Ulimwengu 1
Inaitwa TP Mazembe Combinenga.
Tuwe na shukrani jamani, umeshasahau hata huo uwanja wa mpira wamejenga kwa ufundi na pesa yao (baada ya Mkapa kutembeza bakuli:A S shade🙂...Huyu ataondoka na hatarudi kwa mda mrefu, wakati mechi zinachezwa kila wiki...Tuache kulalamika kwa kila jambo.
Haa haa haa. Katika watu wenye ubishi wa kijinga duniani Watanzania wanaongoza. Kweli unaweza kutamba timu ya taifa ina kiwango?
Ndoto za mwendawazimu. Watu wa sampuli yako ndie mnafanya tusisonge mbele kwenye mpira. Mkibahatisha kamechi kamoja mnapiga kelele utafikiri mna vichaa. Wewe kwa kuangalia mchezo wanaocheza timu ya taifa unaweza kweli kufurahia na kujitapa eti hongera. Kesho maumuvi yanakurudia halafu unasikia eti tunajiuliza tumefikaje hapa jamani... kumbe ubishi usio na msingi
Tuwe na shukrani jamani, umeshasahau hata huo uwanja wa mpira wamejenga kwa ufundi na pesa yao (baada ya Mkapa kutembeza bakuli:A S shade🙂...Huyu ataondoka na hatarudi kwa mda mrefu, wakati mechi zinachezwa kila wiki...Tuache kulalamika kwa kila jambo.
Kwa hili muraa nakuunga mkono.Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, vyombo vyetu vya habari hasa television vimeshindwa kuwaonyesha watanzania mechi ya mpira wa miguu kati ya timu yetu ya Taifa (Taifa Stars) iliyokuwa ikicheza dhidi ya Moroco.
Wakati vituo vya binafsi vikiendelea kurusha vipindi vyao vya kawaida, Television ya Taifa (TBC) wao walijikita uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kurusha matangazo ya moja kwa moja juu ya ujio wa raisi wa China.
Hivi kweli watanzania tumefika mahali pa kuwathamini wageni kuliko timu yetu ya Taifa? Naamini watanzania walioko Tarime, Tandahimba, Kakonko, Pemba, Namanyele ama Tunduru wangetamani kuishuhudia timu yao ya Taifa kuliko raisi wa China asiye na maslahi yoyote na maisha yao.
Ni dhahiri kuwa viongozi wetu wa sasa wameishiwa kabisa na uzalendo, na ndio maana wanaendelea kufanya mambo ya kijinga huku wananchi wakiwakodolea macho bila kuchukua hatua.
mganga aliyewafunga hirizi safari hii wamng'ang'anie!!
Kwa hili muraa nakuunga mkono.
Kama hawajaonyesha hii mechi live ni kukosa uzalendo.
Lazima tuwe proud na nchi yetu, ina maana walikosekana wadhamini kabisa?
Unawapongeza kwani wamefuzu? Hili ndo jambo linalowafanya wa tz kuonekana waajabu! Kazi kupongeza hata kitu ambacho hakijatekelezwa..
Acheni ushamba wa kijinga
kichwa cha mwendawazimu kimebahatisha wala hatuna kiwango cha kwenda cheza brazil tuwaache tu kina chamack marudiano tutakunya hata 5 kwao