kiLimIlire
JF-Expert Member
- Apr 8, 2012
- 311
- 639
Sikubaliani na wote wanaobeza kile kilichofanywa na Taifa Starz katika mechi ya leo dhidi ya Senegal katika mashindano ya AFCON. Nasema hivyo si kwa kuwa sijui soka bali kwa kuwa kati ya milioni zaidi ya 50 tuliopo nchini hapa hao ndio wameweza kuwepo uwanjani kutuwakilisha, bila shaka wao ndio bora kuliko sie wengine, vinginevyo nasi tungekuwa kati yao.
Sasa basi hatupaswi kuwakatisha tamaa, kila mmoja wapo alionekana kujituma vilivyo, jasho limewatoka haswa, kama mfumo haukuwa mzuri ni kwa kuwa walivurungwa na wapinzani wao Senegal ambao kwa takwimu za ubora wa soka barani Africa wanashika namba moja, sisi tukiwa wa 36.
Kubwa kabisa ni maumbo ya wachezaji, tofauti kati yao na sisi ni kubwa kubwa mno, kwa waliowahi kucheza soka wanafahamu kabisa ilivyoshida sana kukabiliana na mtu anayekuzidi mwili, wakati ukijaribu kuupata mpira yeye huuweka mbali na wewe akiwa kakukinga na mwili wake, ukikaza sana utaishia kumkwatua na kusababisha faulo kama ambavyo mmeshuhudia katika mechi hii, na kuambulia kadi za njano kadhaa na nyingine kuachwa kwa huruma ya mwamuzi.
Hivyo basi, kama ni lawama tuzibebe watanzania wote kabisa kwa kupungukiwa mikakati ya kuwapata wachezaji bora zaidi ya hawa tulionao. Na tatizo kuu kabisa ni kushindwa kupata wachezaji wenye maumbo makubwa miongoni mwetu. Najiuliza, hivi ni kweli kwamba hatuna vinasaba vya watu warefu wa kulisaidia taifa? Hatuna watu wanaoliona hilo!! Kuna wakati ili kujiunga na majeshi yetu kimo kilizingatiwa sana, sera hiyo inaweza kutumika sasa katika timu za watoto, academy mbalimbali na hatimae tukaepuka unyonge wa kuonekana watoto mbele ya timu za Africa Magharibi. Katika mechi hii hata Bocco alionekana mdogo kiumbo.
Poleni wachezaji wa leo kwa shughuli ya leo, fanyeni lililo ndani ya uwezo wenu msijefia uwanjani kwa mipango yetu dhaifu..
Amunike asilaumiwe na mambo ya vyama vya siasa yasiingizwe kwenye mjadala huu, sio kila mtanzania ni mwanasiasa ila Taifa stars ni ya kila mtanzania.