Naona ITV wanataka tuwasuse kama TBC-CCM.
Jamani lakini naona ITV afadhali, TBC kwa kweli ni matope. TBC wanaishi kwa kodi ya mtanzania, hivyo wanatakiwa kuripoti habari kwa maslahi ya watanzania wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, kidini, ukanda au ukabila. Nchi imebadilika, siyo ya chama kimoja tena, hivyo TBC waondokane na ukiritimba wa chama kimoja, hausaidii nchi yetu. Unabomoa, wasikilizaji na watazamaji wa chombo hiki kikubwa wanazidi kupungua. Ushindani unazidi kuongezeka na yule atakayehimili ni yule ambaye anajiweka (positioning) kuhudumia jamii mtambuka. Huwezi kuwaghilibu tena watanzania wa leo. Watu watapenda kuangalia habari na michanganuo (analysis) inayozingatia ukweli na hali halisi ya nchi yetu.
Upinzani na CCM sasa ngoma droo tena kwa wastani upinzani unapendwa zaidi na watanzania walio wengi. Kuudhalilisha upinzani kwa kuto-kuripoti kihalali mambo yao kunavunja heshima ya vyombo husika. TBC ifanye maamuzi ya haraka na ITV warekebishe kidogo tu watakuwa sawa.
ITV waangalie vipindi vyao vifuatavyo:
1. Dk 45: It has to be real. Yaani mahojiano yawe ya ukweli, kuna a lot of staging currently - yaani inaonyesha kuna maandalizi na uchakachuaji unafanyika kwanza kabla ya kurusha kipindi. Muendasha kipindi awe anasoma na kujielimisha mambo ya ndani kumhusu mgeni na mada husika. Asome habari za sasa (current issues), utafiti kwenye nyanja husika na aulize maswali yanayogusa jamii. Hapo siyo bungeni, unaweza kumpa maswali makuu lakini maswali fuatizi aulizwe na atoe majibu. Kujikanyaga siyo aibu au jambo baya kila wakati, ndiyo uhalisia wa binadamu. Hakuna msikilizaji atakayemwona mtu fulani wa ajabu sana eti tu kwa sababu ameshindwa kujibu swali moja au mawili kati ya ishirini, labda ukishindwa kuanzia matano kati ya ishirini tutahoji, huyu waziri vipi.
2. Malumbano ya hoja: hiki kipindi ni tatizo kubwa. Waendeshaji wako mbele mno kumlinda kiongozi fulani au serikali hadi inakuwa too much waswahili husema. Saa zingine waendeshaji wanatia maneno mdomoni mwa msemaji. Na watanzania hawa walivyo waoga ukiwatisha tu ndo kabisaaaa hawasemi. Tuwaache watu wawe huru. Kuna mzee mmoja huwa wanamwita kipindi cha Pima Joto chini ya mzee Masako, mbona huachwa tu awe huru. Kitu cha kuwasaidia wasemeje wakimsema kiongozi, wawe tu na takwimu au ushahidi. Msiwaingilie sana. Kipindi kisiwe student-ish sana. Ni vizuri kuwafundisha vijana wetu kujenga hoja na kuzitetea kwenye public lakini isiewe tu ni kama debate ya wanafunzi. Audience/wageni msiwaalike kwa kuwachambua, mruhusu tu hata wageni nasibu. Itachangamsha mjadala zaidi.
Huu ni ushauri wa bure kwa dada yangu Joyce Mhaville. Jaribuni kuwa na ulinganifu badala ya kuikingia kifua serikali kana kwamba nyie ni wasemaji wake. Wapeni nafasi watu wa serilika na vyama, wasije wakasema wananyimwa nafasi, lakini hali halisi ya wananchi iwekwe wazi pia. Hakuna tunayemsaidia kwa kujaribu kuwaridhisha viongozi. Wao wamesharidhika tayari, wananchi ndo wenye matatizo tuwape nafasi.