Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe iwenu.
Wakati mwingine tunahitaji Serikali yenye roho ngumu kuweza kupambana na maovu. Bila shaka madawa ya kulevya ni janga kuu ambalo linateketeza maisha ya watu wengi. Kwa upande wangu, nilikuwa nahuzunika sana nikipita maeneo ya stendi hasa za Jijini Dar es Salaam na kuona jinsi vijana wengi walivyoharibika huku wakilazimika kuwa wapiga debe huku sauti zao zikiwa zimekauka. Hali hiyo ilininyima raha na kunikosesha amani.
Uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wa kuasisi mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ijapokuwa umepata msukosuko mkubwa umeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la mateja Jijini Dar es Salaam. Nimeshtushwa baada ya kuwasili Dar kuona jiji likiwa katika hali ya utulivu na wale jamaa zangu wanaokaukiwa na koo kutokana na vilevi vikali na madawa ya kulevya wakiwa wamepungua.
Nichukue fursa hii kuwapongeza sana Serikali. Kwa kweli wamefanya uamuzi mzuri kuasisi mapambano hayo na kuyashinda. Nasikia pia kuwa hata ajali za barabarani hasa za bajaji na bodaboda zimepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na kupigwa marufiku matumizi ya viroba.