Hongera sana Mama Joyce Mhaville

Hongera sana Mama Joyce Mhaville

Najaribu kulinganisha hizi hongera zako ulizompa Mama Joyce Mhaville na lawama za kila siku za Wafanyakazi wa Radio One na ITV kuwa wana maisha magumu, huku kutwa wakiishia tu ' Kugongea ' Mihogo pale Kona ya ITV na kwenda kula Chakula cha ' Kushea ' pale Kambi yao Kuu ya Maryland Hotel huku ' mishahara ' yao ikicheleweshwa na kulimbikizwa.

Ama kweli leo nimeamini kwamba ' usilolijua ni sawa na usiku wa giza '.

Hongera sana Mama Joyce Mhaville kwa hizi pongezi / kongole za ' Kinafiki ' ulizopewa.
Pia mbaguzi huyu mama nasikia TV yake wanawake hawaruhusiwi kuvaa Hijabu, huko ni kuwanyanyapaa wanawake wenzake ndio maana wengi wamejitoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nampongeza huyo mama lakini mwambie anayeongoza EAST AFRICA RADIO NA TV kazi imemshinda ,hana changamoto mpya ,vituo hivyo vimepooza , havina shamrashamra ,yaani kwa kifupi wamejibweteka ....yaani hata efm media imeanza juzi lakini inakula sahani moja na clouds media kwa umaarufu kwa vijana na habari za burudani....

Tafadhali wahusika wa channel 5 na ea radio meneja abadilishwe yaani mara 10000 hata Kibonde na Garner wanaweza kazi hiyo japo hawana elimu

Kama vipi mpe hata Mrs Jackline a.k.a Kyln maana mwanao biashara ya ushindani imemshinda
 
I like her, she is a straight forward woman, no bling bling. She studied in Russia. Dah ila hana mtoto wala mme. Some time kutokuolewa nako ni kuzuri especially kwa career woman kuexel zaidi.
Duh! Si kweli kuna wenye familia na wamefika mbali. Hiyo hali ya huyo mama sidhani hata kama yeye yuko comfortable.
 
Nakupa like za kutosha.... Pale Maryland wakikaaga wanaboa sana yaani.

Katika Watu / Wafanyakazi ambao nawajua tena mmoja mmoja in and out ni wa hiyo Media. Nimpongeze tu tena Mama Joyce Mhaville kwa kusifiwa / kupongezwa ' Kinafiki ' hivyo wakati ukweli wa ' Kampuni ' anayoiongoza na matatizo yake yasiyoisha unajulikana na ' Wafukunyuku ' tuliotukuka kama Sisi.
 
Mama Mhavile lazima apewe big up SANA! Kama ana viji-tatizo vya hapa na pale ni sawa. Kwani ni binadamu gani mkamilifu? Kumbuka ITV imepewa nishani ya SUPERBRAND na sio mara moja. Na inapendwa na watu wengi sana mimi nikiwa mmojawapo. BIG UP MAMA!
 
Tukienda na ukweli ITV ni bure kabisa
Angalia habari zao hazina utafiti
Hawana vipindi vizuri
 
Katika Watu / Wafanyakazi ambao nawajua tena mmoja mmoja in and out ni wa hiyo Media. Nimpongeze tu tena Mama Joyce Mhaville kwa kusifiwa / kupongezwa ' Kinafiki ' hivyo wakati ukweli wa ' Kampuni ' anayoiongoza na matatizo yake yasiyoisha unajulikana na ' Wafukunyuku ' tuliotukuka kama Sisi.
Wewe jamaa kujifanya unajua kilakitu ipo siku utakalia kijiti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom