Hongera Rais Samia kwa kutimiza miaka mitatu tangu uape kuwa Rais

Leo imetimia miaka 3 Tangu Rais Samia aape kuwa Rais wa Tanzania.

Kwa miaka hii 3 ,Nchi imepata mafanikio makubwa kwenye nyanja zote za Uchumi na kijamii Kwa mda mfupi kushinda wakati mwingine wowote kwenye historia ya Tanzania.

Ni wazi amesimama na kuonesha Wanawake Wana weza zaidi ya kuweza tofauti na kasumba ambayo ilikuwepo Kwa miaka Mingi.

Mojawapo ya mambo ambayo amefanikiwa na kuonesha Uongozi unaoacha alama kubwa ni haya hapa 👇👇

-Kutekeleza na kukamilisha Miradi Mikubwa Iliyoanzishwa awamu ya 5
-Demokrasia na Uhuru wa Maoni/Habari
-Kero ya NIDA
-Maji
-Afya
-Elimu
-Miundombinu hasa Vijijini
-Utalii
-Diplomasia ya Uchumi.
-Kilimo
-Micheso na Sanaa

My Take
Hongera sana Rais Samia kazi umeiweza.

View: https://www.instagram.com/p/C4r_rCjq1vm/?igsh=NHpjdDBicjEzajBt

View: https://www.instagram.com/reel/C4rwaSiKUFB/?igsh=MXM2Z3Z5aDI0c2dxaA==

View: https://www.instagram.com/reel/C4qplBMtrz5/?igsh=YWt6Z3U2Nzlxdm11
 
Na Amosi Richard

M3.jpg

Ingelikuwa ni kitabu cha hadithi basi ingekuwa hadithi nzuri isiochosha yenye kuvutia sana kuanzia kwa msimuliaji na hadhira yake, lakini ni kazi tu za Mwanamke mmoja kutoka ardhi ya Kizimkazi ndani ya Visiwa vya Marashi ya Karafuu aliyeweza kubadilisha maono yake kuwa uhalisia na kubeba hatma ya Watanzania zaidi ya milioni 61. Hadithi yake inasisimua na ni funzo la Uongozi kwa wanawake, hadithi yake imeweka alama ya uimara walionao wanawake katika kustahimili nyakati ngumu na kuzibadilisha kuwa nyakati bora.

Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema "Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kwa paka kufungwa kengele shingoni; tabu ni kumpata panya wa kufanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana kwa kudhani paka watajifunga au kufungana kengele”.

Tarehe 19 Machi, 2021 aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akaapa kulinda Katiba ya Jamhuri, akaapa kuwatumikia Watanzania Kama Rais na sio Makamu tena.

Kama Amiri Jeshi Mkuu akakagua Gwaride lake la kwanza na bendera yake ikapandishwa, kuanzia hapo historia ikabadilika, aliekuwa Makamu wa Rais sasa ndio Rais wa Jamhuri kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri.

Sitofahamu zote zilizokuwa na minogono yote ikazima Tanzania ikapata Rais wa kwanza Mwanamke na safari mpya ya kuijenga Tanzania ikaendelea na hapa ndipo mfano wa paka aliousema Baba wa Taifa, alipofungwa kengele na Amani ikapatikana kwa Watanzania wote na kuanza kuyaona maono ya Uongozi wa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan yakitafsiriwa kwa Vitendo kwenye Sekta zote nchini.

Tukumbuke ni mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi kushika wadhifa wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Tanzania, Mwanamke huyu watu wengi wakawa na hofu atawezaje kuiongoza Tanzania katika kipindi kigumu cha majozi lakini kwa ujasisri alisimama na kukiri yeye ndio Rais na hakuna kitu kitakachoharibika.

20240318_231031.jpg

"Kwa wale mliokuwa na Mashaka, mwanamke huyu ataweza kuwa rais wa Tanzania! Nataka niwaambie Alie simama hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye Jinsia yake ni Mwanamke" Mhe.Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wahenga walisema Wali wa kushiba huonekana kwenye sinia lakini pia ni dhahiri kwamba dalili za mvua ni mawingu na mwenye macho haambiwi tazama. Mhe. Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametudhihirishia umadhubuti na uhodari wake kama kiongozi mwenye Maono na Dira halisi ya maendeleo katika Taifa letu.

Aliipokea nchi ikiwa katika kipindi kigumu cha Msiba lakini pia Ugonjwa wa Covid 19 ambapo Mataifa mengi yalikuwa yamefunga mipaka yake kujilinda dhidi ya maambukizi lakini Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan alikuja na mikakati maalum iliyoleta mabadiliko na maendeleo ambayo yamekuwa hadithi kamili ya kusimulia miaka 3 iliyo na kishindo kikubwa.

Ndani ya muda mfupi wa miaka 3 ya Uongozi wake amefanya mapinduzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi wakati huo nchi ikiwa katika hali ya amani na utulivu wa hali ya juu, amekuwa kimya na kuacha kazi zake zizungumze, amefanya mabadiliko katika Sera za Nje, Demokrasia, Utekelezaji wa Miradi Mikubwa ya Kimkakati, kubuni miradi mipya ya Maendeleo, Kuboresha Huduma za Jamii (Afya, Maji, Elimu), Maendeleo ya Sekta za Kiuchumi, Kilimo na Viwanda, haya yote ni ishara ya uwezo wa hali ya Juu wa uongozi wa matokeo chanya kwa Mwanamke.

Mhe.Dkt.Samia Suluhu ameasisi falsafa yake ya uongozi ya 4R ,ambayo inajumuisha Ustahimilivu Upatanishi, Mabadiliko na Kujenga Upya (Reciliance, Reconciliation, Reform and Rebuilding) yote hii ni kuonyesha dhamira yake ya dhati kujenga Taifa ambalo lina Umoja na kila Mtanzania anafurahia Utaifa wake.

Rais Samia amehakikisha Demokarsia inashamiri kupitia dhana ya Maridhiriano kwa kuhakikisha wanasiasa wote waliokuwa uhamishoni nje ya nchi wanarejea nchini na kuwahakikishia usalama wao kama raia wengine wote, waliokuwa na kesi za kisiasa kufutwa, wenye madai kulipwa lakini kubwa zaidi kuruhusu mikutano ya hadhara ili Vyama vya Siasa vijipambanue kwa sera zao.

Rais Samia amekuwa muumini wa uongozi shirikishi anaamini katika kujifunza na sio kuendesha mambo bora yaende , tumeshuhudia Mawaziri wake na Makatibu wakuu wa Wizara wakiwekwa kambi kupata semina na Mafunzo namna bora ya kuwahudumia wananchi kwani anaamini Uongozi ni dhamana na Uongozi ni huduma.

20240318_231019.jpg

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja kujifunza zaidi. Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo". Maneno haya ndiyo anayaishi Rais samia kwa kuruhusu mafunzo ya mara kwa mara kwa wateule wake ngazi zote ili wasiwe kikwazo cha maendeleo kwa wananchi.

Rais Samia amedhihirisha kuwa ni Mwanademokrasia wa kweli na wala haogopi hoja kinzani dhidi ya uongozi wake, wale wote wenye mawazo mbadala au tofauti na Chama chake hakuwafungia milango bali ameendelea kuwapa nafasi ya kuwasikiliza na kuruhusu mpaka maandamo waseme yale wanayojisikia kusema na wanayoona ni sahihi kwao bila bughudha ya aina yoyote.

Tumeshuhudia Ujenzi wa Madarasa nchi nzima, Ujenzi wa Vituo vya Afya, Hospitali na Zahanati, Ujenzi wa Barabara kila kona ya nchi, Uboreshwaji wa mifumo ya Upatikanaji wa haki kwenye mhimili wa Mahakama kwa kuunda Tume ya Haki Jinai, lakini pia tumeshuhudia ukamilishwaji wa Miradi mikubwa ya kimkakati, Bwawa la Kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere, Reli ya Kisasa, Daraja la Kigongo Busisi, Ununuzi wa Ndege za Abiria na Mizigo, Uboreshwaji na Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Kuikuza Diplomasia ya nchi yetu Kimataifa na mengine mengi.

Mpigania Uhuru mmoja wa Afrika Kusini aliyejulikana kwa jina la Solomon Kalushi Mahlangu aliwahi kusema "Damu yangu italisha miti ambayo itazaa matunda ya Uhuru. Waambie watu wangu kwamba ninawapenda. Lazima vita iendelee"

Rais Samia kazi zake zimepanda miti ya Uhuru wa Kiuchumi, Upendo wake umedhihirika kwa Wananchi wake kwa huduma kedekede za Kijamii, amedhihirisha kweli yeye ni Kiongozi ambaye ni Mama wa Watanzania wote.

Hongera Mhe.Rais. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka mitatu ya Uongozi wako katika Taifa letu, kazi zako zinaongea nasi twaridhishwa na utendaji wako, endelea kuchapa kazi.

Kazi Iendeleee

simoniamosi5@gmail.com
+255 686 054 224 / +255 747 084 224
 
Hongera sana kwake.

Amechukua Nchi ikiwa kwenye mgawanyiko Mkubwa sana wa Kikabila na Kikanda.

Changamoto bado zipo ila ajitahidi kujitenga na Matajiri maana bado bei ya Sukari ipo juu, bei ya Petrol imepanda tena n.k

Lingine muhimu, bado Zanzibar wanatunyonya Bara.

Hebu tufanye mpango wa ku-review terms and conditions za huo Muungano wetu ili kuwe na win - win conditions
 
Kwa hakika Rais wetu na Jemedari wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka,chuma cha reli,shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,simba wa nyika,nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge amefanya kazi kubwa sana katika kuwakwamua na kuwainua kiuchumi wananchi.amekata kiu ya watanzania njii ya mengi waliyo kuwa na kiu nayo na kuyahiyaji katika mioyo yao. Amegusa maisha ya watanzania wote na kumfanya kila mtu kuwa na uhakika wa kutimiza ndoto yake.

Rais Samia Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe.
 
Ingelikuwa ni kitabu cha hadithi basi ingekuwa hadithi nzuri isiochosha yenye kuvutia sana kuanzia kwa msimuliaji na hadhira yake, lakini ni kazi tu za Mwanamke mmoja kutoka ardhi ya Kizimkazi ndani ya Visiwa vya Marashi ya Karafuu aliyeweza kubadilisha maono yake kuwa uhalisia na kubeba hatma ya Watanzania zaidi ya milioni 61. Hadithi yake inasisimua na ni funzo la Uongozi kwa wanawake, hadithi yake imeweka alama ya uimara walionao wanawake katika kustahimili nyakati ngumu na kuzibadilisha kuwa nyakati bora.

Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema "Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kwa paka kufungwa kengele shingoni; tabu ni kumpata panya wa kufanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana kwa kudhani paka watajifunga au kufungana kengele”.

Tarehe 19 Machi, 2021 aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan aliapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akaapa kulinda Katiba ya Jamhuri, akaapa kuwatumikia Watanzania Kama Rais na sio Makamu tena.

Kama Amiri Jeshi Mkuu akakagua Gwaride lake la kwanza na bendera yake ikapandishwa, kuanzia hapo historia ikabadilika, aliekuwa Makamu wa Rais sasa ndio Rais wa Jamhuri kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri. Sitofahamu zote zilizokuwa na minogono yote ikazima Tanzania ikapata Rais wa kwanza Mwanamke na safari mpya ya kuijenga Tanzania ikaendelea na hapa ndipo mfano wa paka aliousema Baba wa Taifa, alipofungwa kengele na Amani ikapatikana kwa Watanzania wote na kuanza kuyaona maono ya Uongozi wa Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan yakitafsiriwa kwa Vitendo kwenye Sekta zote nchini.

Tukumbuke ni mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi kushika wadhifa wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Tanzania, Mwanamke huyu watu wengi wakawa na hofu atawezaje kuiongoza Tanzania katika kipindi kigumu cha majozi lakini kwa ujasisri alisimama na kukiri yeye ndio Rais na hakuna kitu kitakachoharibika.

"Kwa wale mliokuwa na Mashaka, mwanamke huyu ataweza kuwa rais wa Tanzania! Nataka niwaambie Alie simama hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye Jinsia yake ni Mwanamke" Mhe.Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wahenga walisema Wali wa kushiba huonekana kwenye sinia lakini pia ni dhahiri kwamba dalili za mvua ni mawingu na mwenye macho haambiwi tazama. Mhe. Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametudhihirishia umadhubuti na uhodari wake kama kiongozi mwenye Maono na Dira halisi ya maendeleo katika Taifa letu .

Aliipokea nchi ikiwa katika kipindi kigumu cha Msiba lakini pia Ugonjwa wa Covid 19 ambapo Mataifa mengi yalikuwa yamefunga mipaka yake kujilinda dhidi ya maambukizi lakini Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan alikuja na mikakati maalum iliyoleta mabadiliko na maendeleo ambayo yamekuwa hadithi kamili ya kusimulia miaka 3 iliyo na kishindo kikubwa.

Ndani ya muda mfupi wa miaka 3 ya Uongozi wake amefanya mapinduzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi wakati huo nchi ikiwa katika hali ya amani na utulivu wa hali ya juu, amekuwa kimya na kuacha kazi zake zizungumze, amefanya mabadiliko katika Sera za Nje, Demokrasia, Utekelezaji wa Miradi Mikubwa ya Kimkakati, kubuni miradi mipya ya Maendeleo, Kuboresha Huduma za Jamii (Afya, Maji, Elimu), Maendeleo ya Sekta za Kiuchumi, Kilimo na Viwanda, haya yote ni ishara ya uwezo wa hali ya Juu wa uongozi wa matokeo chanya kwa Mwanamke.

Mhe.Dkt.Samia Suluhu ameasisi falsafa yake ya uongozi ya 4R ,ambayo inajumuisha Ustahimilivu Upatanishi, Mabadiliko na Kujenga Upya (Reciliance, Reconciliation, Reform and Rebuilding) yote hii ni kuonyesha dhamira yake ya dhati kujenga Taifa ambalo lina Umoja na kila Mtanzania anafurahia Utaifa wake.

Rais Samia amehakikisha Demokarsia inashamiri kupitia dhana ya Maridhiriano kwa kuhakikisha wanasiasa wote waliokuwa uhamishoni nje ya nchi wanarejea nchini na kuwahakikishia usalama wao kama raia wengine wote, waliokuwa na kesi za kisiasa kufutwa, wenye madai kulipwa lakini kubwa zaidi kuruhusu mikutano ya hadhara ili Vyama vya Siasa vijipambanue kwa sera zao.

Rais Samia amekuwa muumini wa uongozi shirikishi anaamini katika kujifunza na sio kuendesha mambo bora yaende , tumeshuhudia Mawaziri wake na Makatibu wakuu wa Wizara wakiwekwa kambi kupata semina na Mafunzo namna bora ya kuwahudumia wananchi kwani anaamini Uongozi ni dhamana na Uongozi ni huduma.

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja kujifunza zaidi. Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo". Maneno haya ndiyo anayaishi Rais samia kwa kuruhusu mafunzo ya mara kwa mara kwa wateule wake ngazi zote ili wasiwe kikwazo cha maendeleo kwa wananchi.

Rais Samia amedhihirisha kuwa ni Mwanademokrasia wa kweli na wala haogopi hoja kinzani dhidi ya uongozi wake, wale wote wenye mawazo mbadala au tofauti na Chama chake hakuwafungia milango bali ameendelea kuwapa nafasi ya kuwasikiliza na kuruhusu mpaka maandamo waseme yale wanayojisikia kusema na wanayoona ni sahihi kwao bila bughudha ya aina yoyote.

Tumeshuhudia Ujenzi wa Madarasa nchi nzima, Ujenzi wa Vituo vya Afya, Hospitali na Zahanati, Ujenzi wa Barabara kila kona ya nchi, Uboreshwaji wa mifumo ya Upatikanaji wa haki kwenye mhimili wa Mahakama kwa kuunda Tume ya Haki Jinai, lakini pia tumeshuhudia ukamilishwaji wa Miradi mikubwa ya kimkakati, Bwawa la Kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere, Reli ya Kisasa, Daraja la Kigongo Busisi, Ununuzi wa Ndege za Abiria na Mizigo, Uboreshwaji na Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Kuikuza Diplomasia ya nchi yetu Kimataifa na mengine mengi.

Mpigania Uhuru mmoja wa Afrika Kusini aliyejulikana kwa jina la Solomon Kalushi Mahlangu aliwahi kusema "Damu yangu italisha miti ambayo itazaa matunda ya Uhuru. Waambie watu wangu kwamba ninawapenda. Lazima vita iendelee"

Rais Samia kazi zake zimepanda miti ya Uhuru wa Kiuchumi, Upendo wake umedhihirika kwa Wananchi wake kwa huduma kedekede za Kijamii, amedhihirisha kweli yeye ni Kiongozi ambaye ni Mama wa Watanzania wote.

Hongera Mhe.Rais. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka mitatu ya Uongozi wako katika Taifa letu, kazi zako zinaongea nasi twaridhishwa na utendaji wako, endelea kuchapa kazi.
IMG-20240319-WA0000.jpg
 
Acha wivu na chuki usio na msingi.Samia ni Game hata kama hupendi 🤣🤣

View: https://www.instagram.com/reel/C4qYdBCNdrO/?igsh=ZXdma3RpajM1c245

Kuongezeka kwa MRI ni tija? Je masikini waiojiweza wana access ya hizo amchine.

NHIF wamepunguza huduma kwenye bima. Ingekuwa kaleta bima ya afya kwa wote angalau ningeona ni tija.

Nichagueni niwe rais nitaleta bima ya afya kwa wote buree.

Mbunge anatibiwa Apolo huku mlalahoi anatembea na karatasi kuomba omba mitaani ili akatibiwe.
 
Hatua Moja huanzisha nyingine.Hizo Mashine sio mapambo hapo kabla Pesa nyingi zilitumika kwenda Nje ya Nchi,unaposema sio Tija utakuwa na matatizo kichwani.

Pili tayari sheria ya Bila ya Afya Kwa wote ameipigisha Samia,kinachoendelea ni kuratibu vyema Ili gharama ziwe affordable na Kwa taarifa Yako tuu Ile sheria inatambua Watu maskini zaidi ya mil.20 watatibiwa free of charge.

Masisitiza Samia ni Game Charger hata kama hutaki.
 
Hivi nyie chawa mnazungumzia nchi gani maana hali ya uchumi huku mtaani ni ngumu balaa.
 
Nchi yenye watu million 60+ mnashangilia kupatikata vitambulisho million 10?

Nyie kuku mnaotembea na vibegi mjini akili zipo kwenye vibegi vyenu.
Vitambulisho ni Kwa watu wazima sio Watoto.

Wewe ni mbumbumbu hujui hata population patterns ya Tanzania.Rudi darasani kasome zile pyramids uje kufuta ujinga ulioandika.
 
Back
Top Bottom