Hongera Rais Magufuli kwa kumruhusu Dangote achimbe Makaa ya Mawe, bado Reli na Gesi...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,602
Wanabodi,

Wakati wa lile sekeseke ya Kiwanda cha Dangote kusitisha uzalishaji sementi kufuatia gharama kubwa za uzalishaji, kuna watu tulishauri humu, kama Tancoal wameshindwa kuzalisha makaa ya mawe, then Dangote aruhusiwe kuchimba mwenyewe.

Leo akiwa katika sherehe ya uzinduzi wa magari 580 ya Dangote, rais Magufuli amemruhusu Dangote kuchimba mwenyewe Makaa ya Mawe na kuyasafirisha kwa matumizi yake na akiweza kuchimba ya ziada auzie wengine. Kwa hatua hii, Rais Magufuli anastahili pongezi za dhati sana.

Sasa bado aruhusiwe kujenga reli yake, aruhusiwe kujenga bandari yake Mtwara, aruhusiwe kuchimba gesi yake.

Kuhusu gesi wengi humu tulimtetea Dangote kwa nini auziwe gesi kwa bei ya Dar es Salaam. Ameamrisha ndani ya siku saba apewe bei elekezi kwa mkoa wa Mtwara.

Pamoja na matatizo mengine ya rais wetu kama hili la udikteta, kwenye mazuri jamani tumpongeze huyu Msukuma. He is very practical, ameondoa lots of red tapes.

Hongera sana rais wetu Magufuli.

Wale matajiri wetu, kina Mengi, MO Dewji, Manji, Mfuruki and the like, kiukweli Watanzania would have like to see hizo opportunities alizopewa Alhaj Aliko Dangote, wangepewa pia kina Dangote wetu.

Paskali
 
Amemshirikisha waziri Muhongo kwenye hili au kama kawaida yake mkuu wa kila kitu dereva na utingo niyeye peke yake!
 
Pascal Mayalla!

Swali lakizushi hivi Dangote ameshaanza kununua Gesi Asilia kutoka Madimba? Na anauziwa na TPDC kwa bei gani? Kama amepata gesi kwa bei nafuu Makaa ya Mawe anayataka kwa ajili ya kazi gani. Kuwa mwangalifu unapojibu.

Ili uwashe makaa ya mawe unahitaji gesi kuwashia. Akipata hiyo gesi bado ataendelea kuzalisha umeme kwa kuzumia Industrial Diesel Oil au atazalisha kwa kutumia makaa ya mawe au gesi asilia?

Waulize Tanesco na Waziri wa Nishati na Madini kwa nini wasichangamkie tenda ya kuzalisha umeme wakamuuzia Dangote? Au mpaka Rais awaagize si ni biashara nzuri tu!
 
Nimemsikia moja kwa moja kupitia AZAM TV, Naungana nawe Paskali. Nimefurahishwa kwa jinsi anavyoondoa urasimu katika maamuzi ya kibiashara(uchumi). Ameeleza, katika dunia ya sasa, hakuhitaji kuchelewachelewa katika kufanya mambo yaende.

Hongera zake na washauri wake katika suala hili.
 
Pascal Mayala!
Swali lakizushi hivi Dangote ameshaanza kununua Gesi Asilia kutoka Madimba? Na anauziwa na TPDC kwa bei gani? Kama amepata gesi kwa bei nafuu Makaa ya Mawe anayataka kwa ajili ya kazi gani. Kuwa mwangalifu unapojibu. Ili uwashe makaa ya mawe unahitaji gesi kuwashia. Akipata hiyo gesi bado ataendelea kuzalisha umeme kwa kuzumia Industrial Diesel Oil au atazalisha kwa kutumia makaa ya mawe au gesi asilia? Waulize Tanesco na Waziri wa Nishati na Madini kwa nini wasichangamkie tenda ya kuzalisha umeme wakamuuzia Dangote? Au mpaka Rais awaagize si ni biashara nzuri tu!
Mkuu Kapustakasha, kwenye production zote watu wanakuwa na altenative sources just in case, hata katika mitambo ya umeme ya Kinyerezi, japo inatumia gesi, standby generators za dizel zipo.
Hivyo hata akitumia gesi, hayo makaa atawauzia wengine.

Paskali
 
Back
Top Bottom