Hongera Rais kwa hili la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo nakuunga mkono 100%

Huu mradi wa Bagamoyo ni tofauti sana na hiyo mifano uliyotoa hapa. Ngoja niufafanue kidogo mradi wa Bagamoyo.

Mosi, mradi wa Bagamoyo ni wa kiuwekezaji na wala sio mkopo. Ni uwekezaji wa kiubia kati ya Oman na China na wanakuja na mtaji wao na technical knowhow ya kukamilisha mradi huo.

Pili, moja ya sehemu ya uwekezaji huo ni bandari ya Bagamoyo. Bandari hii ni ya kisasa mno kiasi kwamba itahudumia meli za 4th generation tu ambazo hakuna bandari yoyote katika ukanda wa mwambao wa Africa mashariki yenye uwezo wa ku-handle hizo meli, only Durban of South Africa can handle them. Meli hizi ndio za kisasa zaidi duniani na zina uwezo wa kupunguza gharama za usafiri wa baharini by more than half! Tofauti na upotoshaji unaofanywa, bandari hii haikusudiwi kushindana na bandari ya Dar es Salaam, bali kufidia mapungufu ya Dar Port.

Tatu, mradi huu utachochea sekta ya usafirishaji kukua kwa kasi kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. Hata hiyo Reli mpya ya SGR itapata cargo ya kutosha kutoka kwenye hiyo bandari.

Nne, mradi huu unashirikisha ujenzi wa viwanda vipya mjini Bagamoyo kwa kuigeuza Bagamoyo kuwa Special Economic Zone. Hii ingeifanya Bagamoyo kuwa powerful economic hub kwa ukanda huu wa Africa mashariki na kati. Ingezaa ajira nyingi na export nyingi na kodi nyingi.

Kwahiyo, serikali ilichopaswa kufanya ni ku-negotiate the best deal possible na hawa wawekezaji, ili kuhakikisha kuwa faida kubwa inabaki Tanzania. Huu ni uwekezaji wa USD 10 Billion, ambazo Tanzania hatutakuwa na uwezo nazo kwa miaka ishirini ijayo hata tungeamua kukopa.
Hayo ni maneno ya wapigaji tuu, angalia; Kwanini Wacongo, Wanyarwanda, warundi, Sudani kusini, mikoa ya kagera, mwanza, Geita, Shinyanga nasikia siku hizi hata Mbeya wote hao wanakimbilia kununua bidhaa Kampala? ukipata majibu sahihi nistue.
 
Tatizo ni kwamba hii mikataba ni ya siri siri. Sasa watz wanaumbuka. Walikuwa hawajui tangu wamesaini?
 
Rais wa CCM hajawahi kosa watetezi au wasifiaji kwa lolote afanyalo ndani ya CCM! Hata enzi za ubinafsishaji pambio za sifa zilikua nyingi lkn leo wale wale waliokua wakisifu leo ndo wamekua wapondaji.
ATA akinya kariakoo watasema imefanya vizuri,wanafikiri siasa ni Mpira was yanga na Simba mbona hamuwaongelei omani ambao pia niI wabia
 
Back
Top Bottom