Hongera Rais kwa hili la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo nakuunga mkono 100%

Sijawahi na sitarajii kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.mimi ni mtu huru na napenda sana kuwa huru. Penye ukweli huwa nasimama bila unafiki
Kweli mkuu, huu uzi umekuja baada ya Job Ndugai kusema bandari ingekua na faida kuliko SGR!
 
i thought unahoja za maana kumpongeza rais kumbe ni ngonjera za njaa tuu, kwani hakuna miradi mingine rais huyu huyu ameisain na mchin?? so nayo unasemaje??
acheni sifa za kutokufikiri kwa akili, ishu ni hivi kwa taarifa mkata wa ile project ya bandari bagamoyo haujakaa sawa kimaslai, ungekuja na sababu hii ningeona kweli unatoa pongezi.
 

Hii bandari haijengwi kwa hela za Tanzania, inajengwa kwa hela za China na Oman, eneo walilochagua wao ni Bagamoyo kulingana na hesabu zao, sisi tunatoa eneo tu.. Issue sio kuboresha hizo Bandari, bali issue ni mizigo itatoka wapi? tujaribu kuishi kivitendo na si kwa nadharia..
 
Sijawahi na sitarajii kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.mimi ni mtu huru na napenda sana kuwa huru. Penye ukweli huwa nasimama bila unafiki
Tatizo hujui unachozungumza unaongea porojo tu. Unajua Ikulu ya Dodoma inajengwa na nani sasa hivi? Mbaya zaidi wamekariri bandari tu, wakati mradi una package nyingi tofauti tofauti. Pia Ni China na Oman, usimtusi mchina peke yake
 
kiuhalisia hakukuwahi kuwa na sababu ya msingi ya kujenga bandari ya bagamoyo kwa gharama kubwa, wakati ingewezekana kupanua bandari za mtwara na lindi.
 
mbona hili swala, lilipingwa sana na wapinzani mkuu,
Ni kweli. Ni muhimu jambo baya linalohusu Taifa au mradi mbaya tukaupigia kelele wananchi wote kwa sababu hasara na maisha Yakiiwa magumu huwa hayabagui uchama. Ila huu mradi wa Bagamoyo ni Useless
 
mradi wa bandari wa bagamoyo unafanana na mradi wa pakistan wa bandari ya Gwadar,ambayo sasa imekamilika na ina operatiwa na china lakini ni mali ya pakistan,au mradi wa iran wa Chabahar,uliojengwa kwa ushirikiano wa india,ni miradi inayokwenda kuwa na faida sana,tatizo wabongo ujuaji mwingi
 


 
Zito alikuwa anajaribu kuulinganisha mtadi wa Mji wa Shenzhen na huu wa bagamoyo ili kupata uhalali wa kujenga hoja. Lakini kiuhalisia, kuulinganisha mradi wa Shenzhen na huu wa bagamoyo ni sawa na Mbingu na dunia.

Kwanza mjue hiyo shenzen Serikali ya china iliu plan huu mji uwe ni mji wa ki electronics. Yaani bidhaa zote za umeme dunia nzima zitoke hapo. Na wamefanikiwa kwa 100% kijiografia Shenzhen imepakana na Hong Kong. Na upande wa China imepakanana na Guangzhou ambao ni mji mkubwa sana wa kibiashara za Kimataifa China.

Wateja wa Shenzhen wanatumia viwanja viwili vikubwa vya ndege . Kiwanja cha Hong Kong Airport na Baiyung Airport,Uwanja wa ndege wa Hong Kong una get 198 na get zote ndege zinapakia masaa 24 na zipo full. Uwanja wa Baiyung una get 226 zote zipo full masaa 24, sasa unaweza ukaimagine ni ukubwa wa kiwango gani biashara zinafanyika Shenzhen. Kwa hiyo kutaka kufananisha huu mradi wa bagamoyo na Shenzhen ni kutaka kutupiga mchanga wa macho.
 
wewe unadandia tu bila kutafakari, huo mkataba ulishauona? Eti hawatukopeshi wanawekeza! Mkataba ni miaka 90 na mradi wanauendesha wao mpaka pesa zao zitakaporudi. Ikiisha miaka 90 Kama pesa zao hazijarudi wataongeza mkataba. Shithole
 

Huu mradi wa Bagamoyo ni tofauti sana na hiyo mifano uliyotoa hapa. Ngoja niufafanue kidogo mradi wa Bagamoyo.

Mosi, mradi wa Bagamoyo ni wa kiuwekezaji na wala sio mkopo. Ni uwekezaji wa kiubia kati ya Oman na China na wanakuja na mtaji wao na technical knowhow ya kukamilisha mradi huo.

Pili, moja ya sehemu ya uwekezaji huo ni bandari ya Bagamoyo. Bandari hii ni ya kisasa mno kiasi kwamba itahudumia meli za 4th generation tu ambazo hakuna bandari yoyote katika ukanda wa mwambao wa Africa mashariki yenye uwezo wa ku-handle hizo meli, only Durban of South Africa can handle them. Meli hizi ndio za kisasa zaidi duniani na zina uwezo wa kupunguza gharama za usafiri wa baharini by more than half! Tofauti na upotoshaji unaofanywa, bandari hii haikusudiwi kushindana na bandari ya Dar es Salaam, bali kufidia mapungufu ya Dar Port.

Tatu, mradi huu utachochea sekta ya usafirishaji kukua kwa kasi kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. Hata hiyo Reli mpya ya SGR itapata cargo ya kutosha kutoka kwenye hiyo bandari.

Nne, mradi huu unashirikisha ujenzi wa viwanda vipya mjini Bagamoyo kwa kuigeuza Bagamoyo kuwa Special Economic Zone. Hii ingeifanya Bagamoyo kuwa powerful economic hub kwa ukanda huu wa Africa mashariki na kati. Ingezaa ajira nyingi na export nyingi na kodi nyingi.

Kwahiyo, serikali ilichopaswa kufanya ni ku-negotiate the best deal possible na hawa wawekezaji, ili kuhakikisha kuwa faida kubwa inabaki Tanzania. Huu ni uwekezaji wa USD 10 Billion, ambazo Tanzania hatutakuwa na uwezo nazo kwa miaka ishirini ijayo hata tungeamua kukopa.
 
Sasa huo mradi wa bandari ya Bagamoyo kama ni uwekezaji wa China/Oman by 100% si wawekeze tu, kwani wakiwekeza fedha zao sisi inatupa tabu gani.

Kama baada ya kukamilika wakija kukosa mzigo si hilo litakuwa ni swala lao? Labda kama hao hawataumiliki kwa hiyo 100% na tunalishwa vitu vingine au kuna makandokando mengine kama ilivyozoeleka.
 
Ahadi na matokeo ni vitu viwili tofauti. Tusisahau ahadi waliyoapa Mugabe baada ya Wazungu kuondoka na matokeo yalivyo Leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…