Hongera Prof. Ndalichako kwa kuliona hili la vitabu vibovu vya TIE

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Feb 25, 2013
1,459
699
Wiki mbili zilizopita kama mdau wa elimu nilitoa maoni yangu kuhusu vitabu vibovu vya taasisi ya elimu. Hongera waziri kwa kuliona hilo, waliohusika kuandaa vitabu hivyo vibovu kwa kutumia kodi za wananchi wawajibishwe na viondolewe mashuleni kwani ni kudidimiza elimu badala ya kuwa mkombozi.

Serikali ifanye mchakato mbadala wa haraka kununua vitabu vyenye ubora toka kwa wachapishaji binafsi (sisi waalimu tunajua wanavyo bora) kuondoa upungufu tunaokabiliana nao huku mikoani shuleni. Hongera waziri ndalichako kwa kusikia kilio chetu.
 
hatujaelewa leta habari kamili,kwamba imekuaje? au waziri kachukua hatua zipi?
 
ADHABU ZA WALIOHARIBU VITABU VYA TAASISI YA ELIMU
IANZE NA WAZIRI WA ELIMU - J. NDALICHAKO


Ninashtuka kwa nini Ndalichako apongezwe? Apongezwe kwa lipi?
Ina maana waziri Ndalichako hakujua kilichoandikwa ndani ya hivyo vitabu vibovu? Ndalichako amekuwa akizunguka na wakuza mitaala mikoani akifungua/kufunga semina elekezi kwa waalimu namna ya kutumia vitabu hivyo vibovu, iweje apongezwe? Angekuwa na nia nzuri na elimu ya watoto wa kitanzania angekataza wasiendeshe hizo semina kwa sababu ni upotevu wa fedha za walipa kodi. Kushindwa kufanya hivyo ina maana kuwa HAFAI kuwepo kwenye nafasi ya uwaziri wa elimu. Waziri Ndalichako linda heshima yako kwa kujiuzulu tuu. Kama sivyo mamlaka yake ya uteuzi iangalie hili na ampangie kazi nyingine japo hatushurutishi kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom