Hongera Prof. Makenya Abraham – Mwenyekiti Mpya wa TCU

Hongera Prof. Makenya Abraham – Mwenyekiti Mpya wa TCU

Joined
Jan 13, 2025
Posts
17
Reaction score
13
Hongera sana Prof. Makenya Abraham kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa TCU.
IMG_3711.jpeg


IMG_3712.jpeg
Tunakupongeza kwa uteuzi huo na tunakuombea Mungu akupe hekima katika kuliongoza jukumu hili muhimu.

Hata hivyo, kwa muda fulani kumekuwa na changamoto katika namna TCU inavyofanya maamuzi yanayogusa vyuo vikuu. Wakati mwingine maamuzi hayo hufanyika bila kuzingatia kikamilifu uhuru wa vyuo vikuu (self-autonomy)katika kuandaa na kuendeleza programu zao kwa msingi wa tafiti za kitaaluma.

Vyuo vikuu vina wataalamu na vinafanya tafiti nyingi kabla ya kuanzisha au kuendesha programu. Kujadiliana na vyuo husika hakutasaidia tu kutatua changamoto, bali pia kutaimarisha na kulinda safe autonomy ya vyuo vikuu. TCU inapaswa kuwa mlezi na mshirika wa vyuo vikuu, badala ya kuonekana kama mamlaka inayofanya maamuzi makubwa bila ushirikishwaji wa kutosha.

Tunaamini chini ya uongozi wako, TCU itaweza kujenga uhusiano mzuri zaidi na vyuo vikuu, kusikiliza maoni yao, na kutatua changamoto zilizojitokeza hapo awali ikiwemo kufungwa kwa baadhi ya kozi katika vyuo kama UDOM na UDSM etc bila majadiliano ya kina na taasisi husika.

Kwa mara nyingine tena, tunatoa pongezi zetu za dhati kwa uteuzi wako na tunakutakia mafanikio mema katika kuiongoza TCU kwa hekima, ushirikiano na kwa manufaa ya maendeleo ya elimu ya juu nchini.
 
Back
Top Bottom