Hongera naibu spika, hakika umebadilika

Hongera naibu spika, hakika umebadilika

Ngoja tusubiri mpaka siku yenyewe ifike...Kesho unaweza shangaa pepo la CCm likampanda akaongea mambo ya ajabu..
 
Wadau amani iwe nanyi...hakika nafurahishwa na namna mh Ndugai anavyoliongoza bunge kwa kuruhusu mijadala na kupokea ushauri kutoka kwa wabunge ambao wamekuwa mwiba kuona kwamba muhimili wao umekuwa ukiingiliwa kwa kuifanya mahakama kuwa ni kichaka cha kuwaficha mafisadi wa nchi hii...

Tuungane pamoja kumpongeza naibu spika na tuwe na imani kwamba mbivu na mbichi za escrow zitafichuka ndani ya bunge hili.
kweli,naye anaganya hivyo kuepuka kumwagwa ubunge kwenye jimbo lake mwakani
 
Wengi wanaweka matumaini katika bunge.......... Kwani hata wakitajwa kwa kuandikwa katika gazeti la serikali ndiyo itakuwa nini? Tanzania tatizo ni impunity.
Mimi naweka matumaini yangu zaidi katika nchi za Ulaya (yes, wakoloni wetu!). Hizi zikiendelea na uzi wa kuzuia msaada mpaka wahusika waadhibiwe...hiyo tu ndiyo itatusaidia. Maana Tanzania itaporomoka kama embe kutoka juu ya mwembe katika siku chache tu. Hatuna stamina ya Kenya au Zimbabwe hata punje.
Cha kufanya: Tuanzishe ukurasa wa petition (maombi) kwa nchi wafadhili hapa JF tuwatake watusaidie katika hili kwa kuendelea na msimamo wao. Let's hope JF haikumegewa- maana TZ nchi ya wonders!
 
Jinsi jana wabunge walivyokuwa na mhemuko hata kama angekuwa mawig angeishia kutukanwa kama angeleta za kuleta.

Tushukuru kwamba Ndugai katoa hiyo nafasi maana haikuwepo kwenye ajenda za siku hiyo. Mawig angeipotezea tu. Angetoa kama taarifa hamna mjadala.
 
Wana jimbo la Kongwa tulikuwa makin kweny luninga kuona kama angepindisha ishu hiyo ya escrow kwan angepoteza 40% ya kula ukizngatia amekwisha poteza 55%,angebakiwa na 5% za wazee wasiojua kuksoma na kuandika nao pia kwakua wanaenda na vijana wa kuwapgia kula basi habar yake ingeishia hapo!
 
Aisee sasa huko umefika mbali...... yaani sisi ni wafu...tungekuwa maiti hili sakata lingekuwa katika hatua tuliopo sasa ...... halafu mkenya kaongea hivyo na wewe unashabikia..... hivi unaufahamu ufisadi unaotokea kenya..... ukiachia mbali gema na wenzao walivyohodhi ardhi yote huku wengi wao wakiwa hohe hahe....
Mkulu naomba ufute kauli hapa.... licha ya kuwa haitafutika moyoni.

watz tunazingua ni ngumu sana kutawala kongo kuliko Tz

ukiniuliza nani Rais bora kati ya Kabila na Kikwete

Nitakuambia JK wa Kongo ni bora kuliko JK wa bongo.
 
Mwanzo mzuri, japo matokeo ya maamuzi yenye tija kwa taifa kutoka kwenye mhimili anaouongoza mh Ndugai ndio yatatoa nafasi ya sisi kumpatia pongezi na sifa dhidi ya alichokifanya.
 
Aisee sasa huko umefika mbali...... yaani sisi ni wafu...tungekuwa maiti hili sakata lingekuwa katika hatua tuliopo sasa ...... halafu mkenya kaongea hivyo na wewe unashabikia..... hivi unaufahamu ufisadi unaotokea kenya..... ukiachia mbali gema na wenzao walivyohodhi ardhi yote huku wengi wao wakiwa hohe hahe....
Mkulu naomba ufute kauli hapa.... licha ya kuwa haitafutika moyoni.

mtakalia kufuta kauli tu wakati watu wanapiga hela, nyie ndo maiti wa siku nyingi kabisa..
 
Kila unapokaribia mwaka wa uchaguzi mkuu ****** hujitia kutoa haki sawa ndani ya Bunge. Ni mnafiki tu, anaubana upinzani dhahiri kwa miaka minne na kuuachilia kwa mwaka mmoja ili kuombea kura kwa wananchi. Wala sina mpango naye.
Ova
 
Ukiwa sisiem lazimauwe mnafiki, Ndugai msalaba umemng'ang'ania inabidi akomae nao, lakini akimpata "Simon wa Kirene" akampokea msalaba, hamtaamini macho na masikio yenu! Msimsifie amekosa wa kumtupia msalaba tu, hata Mzee Sitta alikuwa hivyo hivyo kwenye Richmond lakini mnaona alivyotufanya kwenye Katiba mpya?
 
Wadau amani iwe nanyi...hakika nafurahishwa na namna mh Ndugai anavyoliongoza bunge kwa kuruhusu mijadala na kupokea ushauri kutoka kwa wabunge ambao wamekuwa mwiba kuona kwamba muhimili wao umekuwa ukiingiliwa kwa kuifanya mahakama kuwa ni kichaka cha kuwaficha mafisadi wa nchi hii...

Tuungane pamoja kumpongeza naibu spika na tuwe na imani kwamba mbivu na mbichi za escrow zitafichuka ndani ya bunge hili.
Wanachi tuna kitu cha kufanya ambacho kinaweza kikawa na matokeo mazuri zaid ya kupongeza. ulivyo toa mada yako kama vile wananichi hawana mamlaka ya kutolea maamuzi ya swala hili zaidi ya bunge.
Tambua kuwa wananchi wana mamlaka kuliko vyombo vyote vya dola, iwe police, jensi, mahakama, hata bunge. mkuu kwenye TV hatuangalii mpira, cinema, miziki pekee. Huoni na kusikia kinachotokea kwenye nchi za wenzetu!
 
Kuna aliyewahi kuwa Rais wa Kenya aliwahi kusema Viongozi wa Tanzania wanaongoza Maiti. mkuu huyu ni bwana JOMO KENYATA alimwambia mwalim nyerere 'WEWE UNASEMA NCHI YAKO INA AMANI?AMANI IPO KWA AJIL UNATAWALA MAKONDOO.

Na mimi nasema Kibaki na Uhuru wameongoza/wanaongoza funza. Familia ya Kibaki imefanya biashara ya dawa za kulevya huku wako Ikulu kupitia mkewe Mary Wambui na binti yake Winnie Wangui Mwai.
Si ndio maana wakawaua kwa sumu Waziri wa Usalama wa Ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode, ikiwa ni saa 48 tu kabla hawajaifumua familia ya Kibaki Bungeni kwa kuuza dawa za kulevya.
Uliza nani anamiliki sehemu kubwa ya ardhi ya Kenya? Uliza Uhuru anamiliki ardhi kiasi gani?
Ova
 
mtakalia kufuta kauli tu wakati watu wanapiga hela, nyie ndo maiti wa siku nyingi kabisa..

Watanzania hatujafa..... ndiyo maana unaona vijana wanawakomalia mazee ya kifisadi bungeni mpaka mahela yanarudi.....
 
Back
Top Bottom