Hongera naibu spika, hakika umebadilika

Hongera naibu spika, hakika umebadilika

Yangu macho kwanza hadi Mkuu wa kaya arudi.

Kwani atasema "Ni upepo huo utapita"


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kuna aliyewahi kuwa Rais wa Kenya aliwahi kusema Viongozi wa Tanzania wanaongoza Maiti. mkuu huyu ni bwana JOMO KENYATA alimwambia mwalim nyerere 'WEWE UNASEMA NCHI YAKO INA AMANI?AMANI IPO KWA AJIL UNATAWALA MAKONDOO.
 
Hata mimi naona kama kuna mabadiliko kidogo. Tusubiri tuone atakachokiamua maana hawa watu ni sawa na magari ya Ikulu kuwa na vibao vya namba zaidi ya kimoja...
 
Poa tumwombee naibu spika ili aongozwe na roho wa MUNGU.
 
Napatwa na hofu huyu ndugai akipewa mgao ataendelea kukomaa
 
Nasita kuchangia sifa ambazo bado sijaziona, bado hajatolea maamuzi, vuta subira kwanza

Hakika mkuu ndani ya CCM lolote linaweza kutokea kumwagia sifa ndugai kwa sasa ni mapema mno, nani alitgemea Sitta atayafanya yale aliyoyafanya katika BMK ukizingatia alijipatia sifa wakati ni spika.
 
Ndugai ni kama naye pia ana hasira na Serikali baada ya kutelekezwa hadi wagogo wakachinjwa kule kwao pamoja na kwamba alipiga kelele nyingi before. Alishaona upepo sio mzuri jimboni kwake, hivyo ni bora akasimamia ukweli.

Ndugai is very strategic. Anajua muda wa awamu hii umekwisha. Anajua kama ataibuka mshindi ana uhakika wa kuwa spika bunge lijalo kwani atakumbukwa jinsi alivyoshughulikia escrow.
 
Mahakama imetia aibu kwakweli. Wanaungana na serikali kuiba? majaji wanapokea mgawo tutarajie nini zaidi ya mambo ya ajabu ajabu kama haya
 
Hivi mama wa mjengoni yupo wapi? kwahili...aendelee kukaa huko huko, asije akarudi kutuharibia shughuli.
 
Napatwa na hofu huyu ndugai akipewa mgao ataendelea kukomaa

Muda huu hawatoi mgao tena...inawezekaa mkakati ni ama unalishwa sumu, unatengenezewa ajali, ama unaimba na risasi ya moto...!
 
Wadau amani iwe nanyi...hakika nafurahishwa na namna mh Ndugai anavyoliongoza bunge kwa kuruhusu mijadala na kupokea ushauri kutoka kwa wabunge ambao wamekuwa mwiba kuona kwamba muhimili wao umekuwa ukiingiliwa kwa kuifanya mahakama kuwa ni kichaka cha kuwaficha mafisadi wa nchi hii...

Tuungane pamoja kumpongeza naibu spika na tuwe na imani kwamba mbivu na mbichi za escrow zitafichuka ndani ya bunge hili.

Hakuna Jipya hapo

hao wate wanafanya Kazi kwa maelekezo na miongozo, na ndio maana huwezi kuwatabiri, leo anakuwa Ndege kesho Mnyama. kinachombadirisha Ndugai sasa ni nini zaidi ya Maelekezo, Wa/anatafutwa mtu/watu hapo wa kutolewa Sadaka
 
ni upepo wa msimu tu...na maigizo ya CCM...everything is planned...
i bet utakuja kuikana kauli yako one day
 
It is premature to shower accolades on him. kati ya sasa na Nov 25 arm-twisting inawezakufanyika hadi akanywea na kuijisalimisha. Hata hivyo tumwombee ashikilie msimamo aliouonyesha awali.
 
Atakuwa ni spika huku pia ila vikao vikigongana atamwachia naibu spika na wenyeviti wake kuongoza bunge... alikuwa anafanyiwa mchakato wa kuapishwa na kupata mafunzo kidogo ya uendeshaji wa bunge hilo.

Ki~english sio tatizo kwake mawigi isije kuwa yale ya Ubunge wa EAC
 
Mahakama imetia aibu kwakweli. Wanaungana na serikali kuiba? majaji wanapokea mgawo tutarajie nini zaidi ya mambo ya ajabu ajabu kama haya

wangese ni sisi wananchi ngoja wazidi kutuibia, ibeni tena mafisadi ikiwezekana hamishieni safe za BOT kwenu, watz watafunguka lini
 
Kuna aliyewahi kuwa Rais wa Kenya aliwahi kusema Viongozi wa Tanzania wanaongoza Maiti. Wizi upo wazi kabisa ,lakini zinapigwa danadana.

Aisee sasa huko umefika mbali...... yaani sisi ni wafu...tungekuwa maiti hili sakata lingekuwa katika hatua tuliopo sasa ...... halafu mkenya kaongea hivyo na wewe unashabikia..... hivi unaufahamu ufisadi unaotokea kenya..... ukiachia mbali gema na wenzao walivyohodhi ardhi yote huku wengi wao wakiwa hohe hahe....
Mkulu naomba ufute kauli hapa.... licha ya kuwa haitafutika moyoni.
 
japo siamini kama amefanya hivyo kwa kuzzingatia maslahi mapana ya nchi yetu tofauti na maslahi membamba ya wasaka ikulu lakini uamuzi huokwa vyovyote unatusaidia kama taifa.viva #ndugai
 
Hata mimi naona amebadilika vizuri kama Mwigulu. Hicho ndicho wananchi tunachokitaka sio bla bla na kesi fake za kijinga za kigaidi
 
Back
Top Bottom