Hongera naibu spika, hakika umebadilika

Hongera naibu spika, hakika umebadilika

ole moringe

Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
27
Reaction score
17
Wadau amani iwe nanyi...hakika nafurahishwa na namna mh Ndugai anavyoliongoza bunge kwa kuruhusu mijadala na kupokea ushauri kutoka kwa wabunge ambao wamekuwa mwiba kuona kwamba muhimili wao umekuwa ukiingiliwa kwa kuifanya mahakama kuwa ni kichaka cha kuwaficha mafisadi wa nchi hii...

Tuungane pamoja kumpongeza naibu spika na tuwe na imani kwamba mbivu na mbichi za escrow zitafichuka ndani ya bunge hili.
 
Ni mipango ya Mungu. Angekuwepo mama mawig angezima mjadala kwa kisingizio cha kanuni. Huko aliko aendelee tu hakuna shida naye
 
Kuna aliyewahi kuwa Rais wa Kenya aliwahi kusema Viongozi wa Tanzania wanaongoza Maiti. Wizi upo wazi kabisa ,lakini zinapigwa danadana.
 
Pinda naye alimegewa mgao wa Escrow, sasa anapigania abaki kuwa waziri mkuu, sasa nahofia kama Ndugai ataweza kuendeleza msimamo wake kama wa jana.
 
Ni mipango ya Mungu. Angekuwepo mama mawig angezima mjadala kwa kisingizio cha kanuni. Huko aliko aendelee tu hakuna shida naye
Jinsi jana wabunge walivyokuwa na mhemuko hata kama angekuwa mawig angeishia kutukanwa kama angeleta za kuleta.
 
Nasita kuchangia sifa ambazo bado sijaziona, bado hajatolea maamuzi, vuta subira kwanza

Whatever the case hawezi rudi nyuma tena, hapa alipofika ni mbele kwa mbele, ngoma inogile, otherwise ccm itaondoka kabla ya uchaguzi ujao
 
Jinsi jana wabunge walivyokuwa na mhemuko hata kama angekuwa mawig angeishia kutukanwa kama angeleta za kuleta.

We mawig humjui...kwanza asivyopenda miongozo we acha tu.. anaminya uhuru wa bunge asingechelea kusema suala lipo mahakamani lisijadiliwe..katibu?
 
Hivi mama Makinda yuko wapi, au yeye haitoshi kwenye hili sakata,

maana nakumbuka Sitta kwenye sakata la Richmond aliwai kumchimba Naibu wake asishughulike nalo mpaka arudi safari.

Ajabu safarii hii Naibu ndio anatoa maamuzi magumu.

Wapi mama Makinda, au kambi za uraisi zinamchanganya.?
 
Yupo sauzi..alichaguliwa kuwa rais wa SADC
 
Kama ameula huko Sadc hatakuwa tena speaker wa hapa? Mwenye uelewa atujuze
 
Ndugai ni kama naye pia ana hasira na Serikali baada ya kutelekezwa hadi wagogo wakachinjwa kule kwao pamoja na kwamba alipiga kelele nyingi before. Alishaona upepo sio mzuri jimboni kwake, hivyo ni bora akasimamia ukweli.
 
Kama ameula huko Sadc hatakuwa tena speaker wa hapa? Mwenye uelewa atujuze

Atakuwa ni spika huku pia ila vikao vikigongana atamwachia naibu spika na wenyeviti wake kuongoza bunge... alikuwa anafanyiwa mchakato wa kuapishwa na kupata mafunzo kidogo ya uendeshaji wa bunge hilo.
 
Back
Top Bottom