Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,075
Kuna watu, nadhani ni kwa kukosa maarifa na uwezo wa kusoma mazingira, wanamlaumu Mbowe kwa nini amefikia hatua ya kuwa karibu na Serikali, na zaidi kuwa na maelewano ya karibu na Mh. Rais Samia juu ya Mstakabali wa Taifa. Wengine wanatoa hoja za kipuuzi kabisa eti Mbowe analambishwa asali wakimaanisha kuwa anapewa pesa na Serikali. Kwa upande mwingine wapo wanaomlaumu Rais Samia kuwa amekuwa legelege kwa CHADEMA. Kwao kiongozi shupavu ni yule wa kutumia jeshi la Polisi kuwatesa wapinzani au kuwanyima haki zao za kikatiba za kufanya siasa.
Wanaomlaumu Mbowe, walitaka Mbowe na CHADEMA waje na kauli zile kali na hata kutumia nguvu dhidi ya Rais, Serikali na CCM.
Wote hao siyo wanafunzi wa wakati na mazingira.
Mwanzoni CHADEMA iliona ingeweza kufikia mafanikio kwa kutumia nguvu kulazimisha yale ambayo wanaamini ni matakwa ya wananchi. Na ndiyo sababu ya kuwa na ile kaulimbiu ya Peoples Power. Lakini baada ya kwenda na mtazamo huo, kuna mengi viongozi wa CHADEMA na Mbowe walijifunza. Kwanza hakukuwa na Peoples Power. Nguvu ya umma haikuwahi kuonekana hata mara moja. Kila mara viongozi wa CHADEMA walipoenda mbele wakijua nyuma yao kuna mamilioni ya Watanzania, waliishia wao magerezani na haikuonekana nguvu za wananchi. Sugu akapelekwa jela, Mbowe mahabusu mara nyingi, Lisu mahabusu na risasi juu, Halima Mdee, Msigwa, Heche, Mwalimu, n.k. Magerezani na mahabusu wakabakia pekee yao. Watanzania waliotajwa kama ndiyo Peoples Power, wakawa kimya.
Baada ya mateso mengi, na bila ya wananchi kuonekana kupigania haki zao, Mbowe akajaribu kutafuta approach tofauti. Akamwomba Marehemu Rais Magufuli kufanyike maridhiano, marehemu akatupilia mbali pendekezo la Mbowe na badala yake akaamua kuendelea na falsafa yake ya kufuta vyama vya upinzani.
Ugandamizaji wa haki za raia wakati wa awamu ya 5, Serikali taratibu ikaanza kutengwa na Dunia:
1) msaada wa MCC wa kila mwaka wa zaidi ya shilingi trilioni 1.4 ukafutwa. Pesa hii ndiyo iliyotusaidia sana kusambaza umeme vijijini.
2) Msaada wa zaidi ya trilioni 1 toka Jumuia ya Madola, ukafutwa kwa sababu ya kuharibu uchaguzi wa 2020, na hivyo Bunge kukosa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.
3) Msaada wa kibajeti wa 40% ya bajeti yetu yote, ukaanza kupigwa panga.
Kwenye mazingira hayo ndiyo Samia anakuwa Rais. Anataka kutekeleza miradi mingi ya maendeleo lakini taswira ya Tanzania kwenye uso wa Dunia ikiwa imechafuka, na upatikanaji pesa umekuwa mgumu.
Rais Samia aliwahitaji wapinzani ili kubadilisha taswira mbaya ya Serikali na CCM. Mbowe alihitaji sana Rais ambaye ana busara na hekima anayeweza ku-accommodate mfumo wa vyama vingi kwa vitendo. Kiongozi mwenye upeo mpana anayetambua kuwa upinzani haimaanisha ugomvi.
Wawili hawa wakawa wamekutana wakati sahihi wakiwa ni watu sahihi wa kuwezesha kupatikana Tanzania mpya inayoanza kumea sasa.
Rais Samia mambo yote yanayolalamikiwa ameanza kuyafanyia kazi, sasa utakuwa ni mtu wa aina gani, kwa kiongozi wa namna hiyo eti ukaanze kutoa kauli kali dhidi yake? Kwa busara ya Rais Samia, leo hii Polisi wamebadilika. Rais Samia ametuonesha kuwa Polisi siyo wabaya, ukiona Polisi wanatenda mambo mabaya, utambue mnaye Rais mbaya.
Ombi Kuu
Rais Samia kama ulivyoahidi kuanzisha taratibu za upatikanaji wa katiba mpya, tunaomba iwe mapema sana. Hiyo itakuwa ni identity na footprint ambayo haitafutika. Hofu yetu kubwa, katiba mpya isipopatikana wakati wa uongozi wako, kuna hatari siku moja tukampata kiongozi shetani, tukarudi tena kule kule kwenye tawala za kishetani.
Wale wapebda siasa za kishetani bado wapo, hivyo ni muhimu sana viongozi wa upinzani kupnesha hekima kama mnavyofanya. Wale wapenda siasa za kishetani waliopo ndani ya CCM wamenuna, Rais pamoja na dhamira yake njema, lakini akageuka ndani ya chama chake akakutana na kundi la wapebda siasa za kihayawani wanaompinga, halafu aje kwa vyama vya upinzani, awakute wenye kumkejeli, anaweza kukata tamaa. Katika uongozi wake huu wa hekima kubwa, Watanzania wengi bila ya kujali utofauti itikadi za chama, ni muhimu sana kuungana na Rais ili tutekeleze jukumu hili kuu la msingi. Wale wachache wanaofurahia mambo ya hovyo, tuwapuuze.
Kwenye haya mazingira ya Taifa letu ambapo watu hawawazi maendeleo ya Taifa bali namna wanavyoweza kubakia katika vyeo vyao, Rais Samia omba sana hekima, kama alivyoomba mfalme Sulemani.