Hongera Maulid Kitenge

Hongera sana Maulid wa Kitenge, wewe ni Miongoni mwa wanahabari bora kabisa Tz, Tunajivunia sana kwako
 
hahaahah kwa kuwa kazi zao wanafanya kwa siri basi tumejenga picha ni watu wenye akili za hali ya juu, kumbe ukiwaleta hadharani ni ma bashite sana. amini mkuu ndo hao vilaza
"ati amini mkuu"-nimecheka
 
Hata mimi nimeshangaa sana wanausalama gani silaha zimekaa kama bongo movie wako location kiasi kwamba akitokea mtu aliyejichokea anamalizana nao hapo hapo
Bongo movie yenyewe wanayaigiza hayohayo yaliyoko kwenye idara hii kama ilivyo kwa kina 007 kuigiza kile wanachokifahamu juu ya idara yao
 
Kuna kale kachalii nilikaona kwenye hiyo prukushani kalivoona bastola kalitoka nduki,yani ni kaoga kama jicho..,teh,,teh...
 
Kitenge kakuta bastola imesharudishwa kiunoni, kakuta malumbano ndio akayaingilia, pia alitumia kauli za busara kumtoa yule kijana na kumuomba kuacha kutumia nguvu kwa mh nape ambae ni kijana mwenzao. Nimeongea nae jana anasema alikua mbali hakuona tukio la bastola ila kama sifa na pongezi anafurahi sana kuzipokea
 
...Kama ukifatilia Vizuri hiyo clip...Kitenge katoa wapi ujasiri wa kumzui huyo jamaa huku anamuambia unaharibu mambo...
Kama isingelikuwa na yeye usalama asingesema chochote..

Nahisi kitenge mtu wa usalama!
Kwani watu wa usalama peke yao ndo wajasiri?
 
Ni walewale. Maana alisikika akimwambia huyo jamqa... mkuu umeharibu na inawezekena kitenge ni bosi wake
 
Kitenge anapiga nondo balaa, jamaa kapigwa kibega akapepesuka mita kumi, hapo hajakatwa mtama.

Wale manjagu kitenge alikuwa na uwezo wa kukomaa nao wote, shezea kijana wa fumagila wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…