Hongera mama Anna-ACT

Hongera mama Anna-ACT

Nimesoma nipashe la leo kuwa anaumwa homa. Namtakia apone haraka.
 
Duuh! mbona kafunikwa hivi? hata hasikiki yani hadi hiruma. ok tutampa ujumbe wa nyumba hapo singida mjini
Dotto, ujumbe wa nyumba kumi ni uongozi eti. Tena wa kupewa kwa heshima. Nikipewa watu 10 nikaweza kubadili maisha yao, nikahakikisha tunaunda umoja wa nyumba zetu, tunasaidiana kwa kila jambo mhimu, tunachangia elimu ya watoto wetu kuanzia chekechekea hadi chuo kikuu, tunatafuta eneo la kulima na kuzalisha kwa chakula na biashara, tunapanga mambo yetu, si ni kazi tosha kabisa? Hongera wewe ulifaa kwa nafasi kubwa. Ninajaribu kuongoza chama kichanga kielewe maana ya siasa na maendeleo, kutumia siasa kuinua agenda za maendeleo, kuunganisha wanasiasa wakubwa kama wewe, Lowasa, na wengine wa aina na ngazi yako...si haba vile. Pole pole watu wanaanza kufikiri kuwa siasa si lazima iwe chafu, tuitumie kwa mambo mema pamoja na kupeana hoja za msingi. Mtaa wako ni upi pale Singida mjini nije kutembelea. Mitaa yote ninajua na sijakutana na mmoja wenye mkakati wowote wa maendeleo. Hata madiwani na wabunge wake wote waliopita na waliopo, huja wakati wa kampeni tu. heri wenye utambuzi maana huona mbali ya upeo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom