Hongera Magufuli Kwa Kuwapasha CHADEMA

Hongera Magufuli Kwa Kuwapasha CHADEMA

Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM".
Haya ndio matatizo ya kuwa na akili halafu unaamua kuiweka mfukoni,maskini hata hajui kuwa kuna bunge (sio la ccm) ndio linapanga matumizi hela zinaenda kwenye halmashauli zinapangiwa matumizi na nani?
D
 
Nadhami mwananchi wa kawaida anataka tu maendeleo. Hajali maendeleo hayo yameletwa na nani au chama gani.
 
Huyu ni yule aliyemuuzia nyumba ndogo yake nyumbani za serikali
 
Binafsi nashindwa kumwelea Mr misifa,kwa wale waliyo bahatika kupita morogoro road utaona kuanzia mlandizi jinsi barabara ilivyo titia Wakati miezi sita haina, chalinze mkandarasi anaendelea na ujenzi barabara inatitia,mikumi national park ndio balaa.
Lakini atakuja na viroja za km zilijengwa kwa ilani ya nyiemu yao.
 
Tatizo la Magufuli ni kuweweseka anapokuwa na viongozi wake. Anakosa busara anaishia kuropoka. Hajui ni wakati gani aongee kama mtendaji wa Serikali na ni wakati gani aongee Kama kada wa chama.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Serikali inaokoteleza sifa na kuzishikia bango. Kwani hizo hela ni za nani hadi ccm ijivunie? Kwa nini walazimishe kusifiwa sana hata wanapojaribu kidogo kutimiza wajibu wao? Kama hakuna msukumo wa upinzani mbona kabla hawakufanya? Kwa nini kwingine ambako hakuna nguvu ya upinzani hawana pressure ya kuwapelekea hiyo miradi?a

Hivi wanafanya kazi huku tmabango ili wananchi wahadaike na kuwachagua tena 2015, ama ni wajibu wao hata wasipotaka kugombea tena?

Doing right things in unclear ways for wrong motive is fake! Ni fake kwa sababu katika mazingira hayo lazima utaona financial viability and sustainability zinafukiwa. Uchaguzi ukiisha, yanafumuka, tunaanza tena upya huku deni la taifa likizidi kupanda na pato la taifa likishuka na mzigo wote kwa mtz!. Watch out you will see!
 
Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli amewapasha madiwani wa Chadema kupitia Meya wa Manispaa ya Musoma kuacha kuwaongopea wananchi kuwa miradi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema.

Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM".

Dr. Magufuli ameyasema haya akiwa katika mkutano wa hadhara, mtaa wa Mukendo, Musoma Mjini.

Chanzo; Gazeti la Majira, Machi 8, 2013.

Mnapongezana kwa mipasho?
Kweli leo siku ya wanawake...
 
Mzee wa kujilipua.unakumbuka kule kwenye kivuko cha kigamboni alisema asiyeweza kulipa nauli mpya apige mbizi?
Mimi huyu jamaa pamoja na watu wengi kumuon kama mchapakazi mie kwangu namuona kama ni attention seeker tu. Huwa anaongea lolote lile analolifikiria kuliongea .....................
 
Yaani ww huna hata akili ya kufikiri. Kwani baraza la madiwani ambalo ndio lina maamuzi ya kupitisha fungu lolote ndani ya halmashauri linaongozwa na wabunge wa chama gani kwa wingi? kumbe ma ww ni magufuli
 
Lol, ccm kwa pumba bwana, hata ma-Dr nao ni pumba tupu. Wao ccm si walianza kuongoza hiyo halmashauri ya Musoma toka chadema haijazaliwa, mbona huo utekelezaji wa mipango ya maendeleo hatukuuona?
 
Mgema akisifiwa.................mie nimesahau,ila naamin itafika siku atapotea na hata jina lake halitosikika tena kama wastaafu waliosahaulika japo walitenda mema katika nchi hii.

Haizidi miaka miwili mbeleni believe me!!!!
 
Huyu jamaa wakati mwingine huwa na wasi wasi na ubongo wake
Ukiwa katikati ya waridi utanukia kama waridi na ukiwa katikati ya matenga ya samaki utaishia kunuka shombo.
 
mwambie arudi kwa babu hajapona vizuri, hata hivyo hapo hakuna kuumbuka.
 
Back
Top Bottom