Hongera Magufuli Kwa Kuwapasha CHADEMA

Hongera Magufuli Kwa Kuwapasha CHADEMA

Kwa nini utekelezaji huo usifanyike Mtwara, Masasi, Lindi na kwingineko ambako ccm inaongoza halmashauri kwa takriban 100%.

Tena ambako wameamua hata kwenda kinyume cha yaliyomo ndani ya ilani yao wenyewe, mpaka Ndugu zetu wa huko walipoamua kutumia nguvu ya umma kuishinikiza serikali....Rejea mgogoro wa gesi MTWARA!
 
Mpongeze na mwenyekiti wako pia kwa kutekeleza "ilani " yenu ya uchaguzi ya 2010, kwa kuanzisha mchakato wa uandikaji wa katiba mpya!
 
Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli amewapasha madiwani wa Chadema kupitia Meya wa Manispaa ya Musoma kuacha kuwaongopea wananchi kuwa miradi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema.

Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM".

Dr. Magufuli ameyasema haya akiwa katika mkutano wa hadhara, mtaa wa Mukendo, Musoma Mjini.

Chanzo; Gazeti la Majira, Machi 8, 2013.

mleta uzi,mpashaji na gazeti wote dugu moja.kwahiyo hayo maneno yake yatabadilisha upepo wa kisiasa?
 
Magufuli uwazi unamponza, Chadema wamezoea kupewa misifa, ukweli wa mambo kuambiwa hawataki. Yoyote kwa CCM kipo madarakani hivyo kinawezesha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2010 kama ilivyopitishwa na wapiga kura nchini Tanzania
 
Kama uongozi wa CDM umeweza kuhakikisha miradi ikafanyika, iwe imeletwa na nini au nanani swala ni kusimamia utendaji wake na kuhakikisha pesa inafanyika kama ilivyokusudiwa bila kufisadi, basi PONGEZI ni kwa uongozi wa CDM.
 
Mpongeze na mwenyekiti wako pia kwa kutekeleza "ilani " yenu ya uchaguzi ya 2010, kwa kuanzisha mchakato wa uandikaji wa katiba mpya!

1. Kuanza kwa ujenzi wa daraja la Kigamboni
2. Kumalizika kwa ujenzi wa barabara jimboni Vunjo
3. Kumalizika ujenzi wa barabara jimboni Hai
4. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mbeya
5. Uboreshaji wa miundo mbinu ya usambazaji maji, jimboni Ubungo
6. Ujenzi wa daraja la Malagarasi
7/ Mradi wa DART jijini DSM
8. Kutoa vibali vya maandamano kwa CDM

hayo ni mambo machache ya kutembelea kifua mbele kutokana na ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 ambayo ilipata uungwaji mkono mkubwa na watanzania kupitia sanduku la kura
 
Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli amewapasha madiwani wa Chadema kupitia Meya wa Manispaa ya Musoma kuacha kuwaongopea wananchi kuwa miradi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema. Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM". Dr. Magufuli ameyasema haya akiwa katika mkutano wa hadhara, mtaa wa Mukendo, Musoma Mjini. Chanzo; Gazeti la Majira, Machi 8, 2013.
Pole sana, kwataarifa tu; kazi ya mbunge na diwani ni kuifanya serkali ifanye kazi na kutimiza wajibu wake kwa wananchi. Kwa hiyo iwapo serkali imefanya miradi ya maendeleo Musoma ni kwa sababu inasimamiwa ipasavyo na ndo maana hawakutekeleza kabla ama hawakupeleka miradi hiyo sehemu nyingine ya nchi yenye shida na mahitaji kama Musoma
 
hata ccm wanajua magufuli ni mzee wa mipasho kama hadija kopa vile.safi sana kwa kumpongeza gamba mwenzio.
 
Mimi huyu jamaa pamoja na watu wengi kumuon kama mchapakazi mie kwangu namuona kama ni attention seeker tu. Huwa anaongea lolote lile analolifikiria kuliongea .....................

Thats true Mkuu!
 
Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli amewapasha madiwani wa Chadema kupitia Meya wa Manispaa ya Musoma kuacha kuwaongopea wananchi kuwa miradi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema.

Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM".

Dr. Magufuli ameyasema haya akiwa katika mkutano wa hadhara, mtaa wa Mukendo, Musoma Mjini.

Chanzo; Gazeti la Majira, Machi 8, 2013.

Madiwani wa CHADEMA wanatakiwa wapongezwe kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kusimamia maendeleo katika halmashauri hiyo.maendeleo ambayo yanapaswa kuletwa na ccm ambao wanakusanya kodi kwa wananchi na CHADEMA ambao ni wasimamizi na wahamasishaji wa maendeleo katika maeneo wanayoyaongoza na wasiyoyaongoza.pia ccm nao wanatakiwa wapongezwe kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kutokuwahujum CHADEMA katika halmashauri hiyo kwani CHADEMA wanauwezo wa kusimamia maendeleo vizuri sana katika maeneo wanayo yaongoza wasipo hujumiwa na ccm.
 
Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli amewapasha madiwani wa Chadema kupitia Meya wa Manispaa ya Musoma kuacha kuwaongopea wananchi kuwa miradi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema.

Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM".

Dr. Magufuli ameyasema haya akiwa katika mkutano wa hadhara, mtaa wa Mukendo, Musoma Mjini.

Chanzo; Gazeti la Majira, Machi 8, 2013.
mbona tumeshuhudia zinazoongozwa na ccm ndo huwa zinabolonga hapa tunazungumzia matumizi mazuri ya rasilimali wanazopewa!
 
1. Kuanza kwa ujenzi wa daraja la Kigamboni
2. Kumalizika kwa ujenzi wa barabara jimboni Vunjo
3. Kumalizika ujenzi wa barabara jimboni Hai
4. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mbeya
5. Uboreshaji wa miundo mbinu ya usambazaji maji, jimboni Ubungo
6. Ujenzi wa daraja la Malagarasi
7/ Mradi wa DART jijini DSM
8. Kutoa vibali vya maandamano kwa CDM

hayo ni mambo machache ya kutembelea kifua mbele kutokana na ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 ambayo ilipata uungwaji mkono mkubwa na watanzania kupitia sanduku la kura

Naaam.ndiyo maana tunataka CHADEMA washike dola ili wafanye zaidi ya hayo yaliyofanywa na ccm ambao wanafanya kazi ya kuuma na kupuliza ili kuwahadaa wananchi.
 
Kumbe Magufuli ni mpashaji, unampa mtu ongera kwa kuwapasha watu hii hajabu kweli, mipasho inawenyewe kama na magufuli yumo hiyo ni balaa
 
kumbe Magufuli nae bogus kiasi hicho? Pesa za miradi ya Maendeleo zinatokana na kodi ya wana ccm au ya Wananchi wote??Wananchi tunakatwa kodi tunahitaji maendeleo sasa msitumie kodi zetu kujinufaisha kisiasa kwanza CCM ndio mnaorudisha maendeleo nyuma kwa kulea ufisadi kwenye halmashauri mbalimabali!
 
Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli amewapasha madiwani wa Chadema kupitia Meya wa Manispaa ya Musoma kuacha kuwaongopea wananchi kuwa miradi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema.

Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM".

Dr. Magufuli ameyasema haya akiwa katika mkutano wa hadhara, mtaa wa Mukendo, Musoma Mjini.

Chanzo; Gazeti la Majira, Machi 8, 2013.

Akumbuke kuwa miradi ya maenedeleo katika halmashauri husika inasimamiwa na halmashauri/madiwani,hata kama pesa itatoka mbinguni....Halmashauri legelege zinapelekewa hela....au zinatafunwa,au zinafanya miradi isiyokuwa na viwango,au zinarudishwa hazina mwisho wa mwaka wa fedha wakati wananchi wanabaki wakilia matatizo.....Magufuli analijua vizuri hili,na anatakiwa awapongeze halmashauri ya musoma chini ya uongozi wa CHADEMA.
 
Hahahaaa hua anakaririr Uongo Mpwa, fuatilia takwimu zake utajua ni Uongo, si anaamini kuwa wengi wetu hatusomi na wala hatuna data
unajua kukariri sana nako kuna matatizo, nasikia john boha gufuli ni bingwa wa kukariri.
 
Hapo ni ilani ya CCM sawa, basi na haya pia ni ilani yao:
1. Maisha magumu
2. Mauaji Mwangosi
3. Kibanda
4. Massive failure
5. Migomo
6. Mifuko ya hifadhi

7. Udini
e.t.c.
 
Back
Top Bottom