Hongera Magufuli Kwa Kuwapasha CHADEMA

Hongera Magufuli Kwa Kuwapasha CHADEMA

MAFILILI

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,377
Reaction score
1,200
Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli amewapasha madiwani wa Chadema kupitia Meya wa Manispaa ya Musoma kuacha kuwaongopea wananchi kuwa miradi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema.

Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM".

Dr. Magufuli ameyasema haya akiwa katika mkutano wa hadhara, mtaa wa Mukendo, Musoma Mjini.

Chanzo; Gazeti la Majira, Machi 8, 2013.
 
Huyu jamaa wakati mwingine huwa na wasi wasi na ubongo wake
 
... Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. ...
...
... lakini imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema !! Magufuli hakutakiwa kukanusha ukweli, ila alitakiwa kuongezea kuwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM. Sasa kama sio kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema, aseme hiki ni kipindi gani basi!
 
Kipenda roho hula nyama mbichi,huyu jamaa hawezi hata siku moja kusifia kazi nzuri ya CHADEMA maana anaogopa kuweka kitumbua chake mchanga.
 
Aje hapa aseme TANROADS ndanui ya uongozi wake inadaiwa Hela kiasi gani? Unafiki wake ndo umechangia Tanzania kuwa na madeni makubwa hivi
 
Lakini pia hiyo miradi kwanini haikutekelezwa vipindi vilivyopita kabla chadema haijaongoza halmashauli?.Tangulini gamba likaisifia Cdm?.Mleta mada ulitegemea huyo Gamba magufuri asemeje?
 
Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli amewapasha madiwani wa Chadema kupitia Meya wa Manispaa ya Musoma kuacha kuwaongopea wananchi kuwa miradi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha halmashauri kuongozwa na Chadema.

Dr. Magufuli amewaambia wananchi wa Musoma kwamba miradi yote ya maendeleo iliyofanyika ndani ya manispaa imefuata yale yaliyoanishwa katika ILANI YA UCHAGUZI ya CCM ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM. "Chadema hawana uwezo wa kutekeleza miradi husika kwa vile fedha zimeshikiliwa na kuamualiwa matumizi na serikali iliyo mikononi mwa CCM".

Dr. Magufuli ameyasema haya akiwa katika mkutano wa hadhara, mtaa wa Mukendo, Musoma Mjini.

Chanzo; Gazeti la Majira, Machi 8, 2013.

Mbona huu ni mwaka takiribani wa hamsini CCM ikiongoza Musoma na sera zake hizo haziku tekelezwa zinatekelezwa kipindi hiki cha CDM.
 
Labda miaka hamsini iliyopita ilani iliyokuwa inatumiwa ni ya CHADEMA, mwaka huu wametumia ilani ya CCM
 
Mipasho kama hii ilisababisha mbunge wa ccm igunga kupokwa ubunge wake.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Pumba. Tumezizoea.

kWANI KUSOMA NI KUELIMIKA ? HUYU ----- MPAYUKAJI HAJUI ASEMALO. HATA KAMA MIPANGO INATEKELEZWA NA SERIKALI LAKINI TOFAUTI NI KUWA HALIMASHAURI IKIONGOZWA NA CHADEMA HAKUNA WIZI UNAFANYIKA LAKINI ZIKIONGOZWA NA MAGAMBA NDO MAFISI WANALAMBA PESA ZOTE. TOFAUTI NDO HIYO
SIO KWAMBA SERIKALI HAIPELEKI PES KWENYE HALIMASHAURI ZOTE , LA HASHA ZIKISIMAMIWA NA MAGAMBA ZINALIWA
 
Mimi huyu jamaa pamoja na watu wengi kumuon kama mchapakazi mie kwangu namuona kama ni attention seeker tu. Huwa anaongea lolote lile analolifikiria kuliongea .....................
 
aangalie yasije yakamfika ya igunga,nasikia hawasalimiani na kafumu
 
[QUOTE=Kwanini kila jambo anafanya Magufuri.Ana kimbelembele sana anapenda kila leo asikike,mtindo huu ataiangusha CCm.Kadiri anavyoropoka watu wengi wanaanika uozo wake.Huko Musoma inawezekana anasubilia kwenda Kenya kushuhudia Odinga anaapishwa.Pili Tz lazma tuamke SIASA isitawale SERIKALI ila serikali itawale siasa.Hakuna cha Ilani ya Chama kwa sababu maela yote ya serikali ni kodi za wananchi bila kujali itikadi za vyama.Ina maana barabara ya ubungo mwendo kasi tuseme ni ya Chadema.Au tuseme mikoa ya kusini haina maendeleo ya kasi kwa kuwa asilmia kubwa ni upinzani.Hawa akina Magufuri msipotoshe wananchi.Kwanza jimbo lake la Chato linachukuliwa na upinzani:lying:
 
Mwacheni aendelee kutafuta sifa huku wananchi wa Chato wakiendelea kutaabika , ni msimu wake wa mwisho 2015 hawezi kurudi .
 
Back
Top Bottom