Hongera Lowassa, Hongera UKAWA

Hongera Lowassa, Hongera UKAWA

Hongera lowassa hata Roma aikujengwa siku moja tulipofikia si haba tunapiga hatua tusikate tamaa
 
Lowasa amepata kura milioni kumi. NEC imempa magufuli. Wabung wetu wengi sana wameshinda. NEC kwa maelekezo ya mkapa na kikwete wakiongozwa na makamba, wamezigawa kura zetu kwa ccm

CCm haijashina uchaguzi ila imelazimisha kututawala kwa mabavu. Liwalo na liwe.

Mhh....
 
Hongera Lowasa, kura milioni 6 si utani. Inaonyesha jinsi alivyokubalika na kuaminika.
Hivyo Slaa uchaguzi wa 2010 alifikisha kura ngapi?
HONGERA LOWASSA, HONGERA UKAWA, HONGERA WATANZANIA. Kila la kheri Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kuhusu Slaa ni kwamba alipata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34, hata ungeunganisha na za Prof. Lipumba (aliyepata kura 695,667 sawa na asilimia 8.067) bado kwa namba na kwa asilimia Mamvi ameonesha kukubalika na watanzania wengi kuliko mpinzani yeyote aliyewahi kutokea nchi hii mpaka sasa.
 
Chamuhimu ni tume huru na katiba mpya vinginevyo msitegemee chochote hata miaka 100 mtapiga kelele tu
 
HV TAYARI TUMESHATEPETA NA KUKUBALI UHUNI NA UDHALIMU ASUBUHI HII TU.Are we serious.
 
MPE hongera lowasa kwa kupoteza pesa na sasa anajiuliza anazirudishaje
 
Mimi sikat tamaa sababu raisi wangu ni Lowasa
 
🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃🐃
 
Hongera Lowassa, Hongera UKAWA. Pole sana CCM.
Nimesoma post nyingi sana za kukatisha tamaa kwenye jukwaa hili na kwingineko. Wengi wenu mnafikiri safari ya ukombozi ni sawa na kutembea kwa mguu toka Karimjee kwenda Ikulu. Wengine wananichekesha kuanza kudai ati ?sitapiga kura tena.? We mwehu au umetumwa!!! Sasa usipopiga kura ndio utakuwa unawakomoa usiowapenda? Wendawazimu wakubwa ni wale waoipongeza CCM kwa kushinda uchaguzi. Yaani, unaweza kumpongeza Magufuli kwa jambo moja tu, ?kufanikiwa kukanyaga Ikulu akiitwa rais. Huwezi kumpongeza kwa jambo lolote lingine. Mwenye kustahili pongezi katika uchaguzi huu ni Lowassa na UKAWA.

Wapo wana CCM wanaomcheka Lowassa kwa kuhama CCM na kugombea kupitia CHADEMA na mwisho kutangazwa amekuwa wa pili. Tume ya uchaguzi imempa Lowassa kura milioni sita. Wewe unayemkebehi Lowassa umewahi kushiriki uchaguzi wowote na kupata japo kura elfu mbili tu? Acha ujinga. Lowassa ameonesha kuwa anakubalika kuliko mtu mwingine yoyote Tanzania, na kauli yake inaogopewa sana, na ndio maana jeshi la polisi limeandikisha polisi wengi kuliko idadi. Wanaogopa. Neno moja tu la Lowassa linaweza kusababisha hata huyo mteule wa tume asiweze kuapishwa. Neno moja alilosema Lowassa, ?msifanye fujo na kuwapa sababu.? Ndio maana nasema hongera Lowassa.

UKAWA je, kwanini hongera? Kudadadeki! Hapo ndipo nasema HONGERA tena kwa herufi kubwa zaidi. Pamoja na waasisi kukimbia, UKAWA kamwe haijageuka kuwa ukiwa kama kiongozi mkuu wa CCM alivyosema katika moja ya mikutano. Kama unayesoma ujumbe huu ni mkazi wa Dar es salaam, basi kuna uwezekano kwa asilimia kubwa diwani wako ni UKAWA. Manispaa yako itaongozwa na UKAWA na hata Jiji la Dar es salaam huenda likabadilishwa jina na kuwa UKAWA CITY. Hakuna mwenye uwezo wa kuzuia jambo hilo. Pombe ataongoza toka Magogoni na kando yake tu, pale Karimjee; BENDERA za vyama vinavyounda UKAWA zitakuwa zinapepea, kando ya ile ya taifa au ya jiji. Hapo atakuwepo ?rais? wa Dar akimaliza kero za wananchi. Sasa unategemea wanaukawa waingiwe ukiwa kwa ushindi mkubwa kama huu? Nendeni Dodoma mkaipige hiyo minyimbo yenu ya TOT; kwani hapo Dar nani kaisoma namba? Na hata huko Dodoma, baadhi yao wamepisha siti ili UKAWA waweze kukaa; yaani kama vile mtoto wa shule anavyompisha siti mkubwa wake kwenye daladala. UKAWA anakaa na CCM anashika bomba, kisha atashuka tu kituo kinachofuata.

Ndugu zangu msiweke tena post za kusema pole au kukata tamaa. Wapeni pole hao waliopoteza dira. Unajua mabadiliko sio kuvuka kijito. Ni kuvuka mito, mabonde na bahari. Hapa safari ilipofika sio padogo na tafu ya Ngoyayi haikuwa haba. Wekeni sasa post za mikakati ya sasa na malengo ya kusonga mbele. Na hata kwenye uzi huu ningependa usiweke maneno mengi zaidi ya kusema HONGERA LOWASSA, HONGERA UKAWA.

HONGERA EDWARD LOWASA NA UKAWA kwa ujumula. History will remember Lowasa as the man with a seed of revolutionary minds and Ukawa as the garden of transformation and the followers as the farmers of change. God bless LOWASA, God bless UKAWA.
 
Katika uchaguzi hakuna mshindi wa pili.pole mzee mamvi monduli kunakuhusu sasa!
 
Hakuna kurudi nyuma katiba mpya ya wananchi na tume huru ya uchaguzi ni lazima tuvipate. Wabunge wetu wapigane kufa na kupona hadi haya mambo mawili yapatikane. Wizi uliofanyika baada ya kupiga kura ni mkubwa mno!Ksa cha kukataliwa kukaa mita 200 ndio hicho! Masanduku yalibadilishwa fasta! Mbinu zot wasimamizi wa vituo husika walizijua hence tume haiwezi kukwepa lawama.
 
""Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima"" Lowassa

Kweli?
 
Lowasa amepata kura milioni kumi. NEC imempa magufuli. Wabung wetu wengi sana wameshinda. NEC kwa maelekezo ya mkapa na kikwete wakiongozwa na makamba, wamezigawa kura zetu kwa ccm

CCm haijashina uchaguzi ila imelazimisha kututawala kwa mabavu. Liwalo na liwe.
Wabunge wapi? Kila ck maibiwa hivi huwa mnalala vituoni? Acheni kujifarishi mkubali mmeshindwa sasa kazi tu. Maisha yanaendelea
 
Katika uchaguzi hakuna mshindi wa pili.pole mzee mamvi monduli kunakuhusu sasa!

Duh kumbe fools still exist, with a shallow argument damn. Sasa Lowasa alivyosema elimu, elimu, elimu. Sasa nadhani uende shule upate akili mana u are so stupid for u to live in the 21 century.
 
Mimi sikat tamaa sababu raisi wangu ni Lowasa
Pole sana rais ni Magufuli huyo wa kwako labda rais wa wafugaji wa monduli. Uhamie huko usije ukakwaza maendeleo ya majimbo mengine
 
Hongera Lowasaa , Hongera UKAWA........
 
Back
Top Bottom