Hongera Lema! Hongera Chadema!

Hongera Lema! Hongera Chadema!

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Posts
629
Reaction score
72
Nachukua nafasi hii kuwapongeza Chadema na Mhe. Lema kwa ushindi kwenye kesi ya Ubunge wa Arusha.

Nilidhani na leo mtasema CCM, Nape na Ikulu wameingilia kesi....MKISHINDA HAKI IMETENDEKA, MKISHINDWA KUNA MIKONO YA IKULU...! Ndo mnakua lakini, mkikua mtaacha mtajifunza majibu ya watu wazima kwenye mazingira kama hayo.

Mdogo wangu Lema umeiona Arusha ilivyokuwa imetulia bila maandamano na kelele zisizo na msingi? Endeleza utulivu huu ambao naamini umejifunza kwa kipindi ulichokaa nje ya bunge....!

Kiongozi ni kuonyesha njia, onyesha njia ya maendeleo sio maandamano na fujo. NARUDIA KWA HILI HONGERENI CHADEMA,HONGERA LEMA!!!
 
Yani kweli wewe ndio una akili za ajabu kweli kweli, kuna mtoto wangu wa darasa la nne kasoma hii thread kasema "BABA NA MIMI NIMEANDIKA KAMA HIVI LEO SHULENI....." hivi unakalia unafiki hapa, kijana kama wewe na unafiki huu, ukiwa kama akina Mzee Kingunge utakuwa unatembea uchi ukiwa mchawi kwenye nyumba za watu usiku.

Hatutaki ujinga wako wala pongezi zako. Na maadamano yataendelea kama mtaendelea na upuuzi wenu. Yani mnaendesha nchi kizembe halafu tuwaangalie tu.
 
Ndugu Nnauye Jr,

Kwa niaba ya wanachadema wote, napokea hongera zako za kinafiki. Pamoja na hilo naomba nikupe ushauri... msidhani mtashinda mechi kwa kucheza rafu, wakati ni dakika ya 85, na mmeshachapwa 6-0. kama ni rafu nasi tunazijua. Hizi rafu mnazocheza kupitia kwa baadhi ya wanajifanya kuwa BAVICHA, hakika nakuapia hazitawaacha salama...

Chakufanya Nape, ni serikali ya CCM i-deliver... Watu hawaichagui CDM kwa sababu ni chama kizuri sana tu, bali kwa sababu wamechoshwa na utendaji mbovu wa serikali ya CCM...

Ulitoa hongera Arumeru, Igunga, Sumbawanga, na sasa Arusha. Kubali tu kutoa hongera za ikulu 2015...

Kwa heri...
 
Safi kaka unaonesha ni namna gani ulivyo mwanasiasa mahiri na msema kweli na ukomavu katika siasa.Ni kweli hawa jamaa haki ni pale wanaposhinda wao lakini wakishindwa ni kelele.Hawa ni kama watoto ni wakuvumiliwa tu.Hata kuwa na kadi mbili babu wao wanao sawa,ila angekuwa anazo zitto ungewasikia wakimtaka ajiondoe chamani.Ni chama ch kikanda,ukabila na udini
 
Wewe ni nani wa kuwasifia Chadema na Lema? Punguza unafiki Nape, umbea wewe, unafiki wewe??? Tangu lini ukawa unawasifia Chadema?? Pole sasa umekalia kudandilia hoja za makamanda. Wewe endelea na kamchezo kako ka kuvuruga cdm????????????? Chezea peoplesssssssssssssssss????????? Nape sasa tunaelekea Sumbawanga mjini na Igunga tukakumalizie kabisa:majani7:
 
Utulivu bila amani mioyoni mwetu ni bure wewe NAPE kaa mkao wa kula na magamba wenzie arusha itabaki kuwa arusha na kinachofanyika arusha kitafanyika nchi nzima mwakani.
 
Kweli Nape na CCM yako ni janga la Taifa, Nape hizo ni dalili za Mvua Mvua yenyewe inakuja, sie Chadema tuna Mungu na Wazalendo wakati ninyi ccm mna wataalamu wa propaganda na wizi wa kura. Mwisho tunawahakikishia kuwa kamwe tabia zenu za wizi wa haki ya Umma, arobaini zake zimewadia.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Pia weye Nape Musa Salumu Nnauye ( Nje Cup) maandamano yataendelea tu hakuna wa kutuzuia, Marekani wanaandamana, Uingereza wanaandamana, Ujerumani wanaandamana na hata hao magamba wenzako wanaandamana kwanini cdm...makamanda wa ukweli, mapeoples wasiandamane? Ungekuja arusha leo ujionee mwqenyewe watu wanavyosonga mbele.....................Mapeoplessssss peoplesssssssssssssssss...malizia mwenye weye Nape Musa Salumu Nnauye :majani7:
 
kwa hiyo nape unataka kusema mlimshitaki lema il Arusha itulie? Ni utulivu ganu unaouzungumzia maandamano na mikutano ya hadhara sio ishara ya vurugu ni haki ya kikatiba ya wananchi.
 
Kauli ya Kikwete Ccm mjitegemee sasa habari ya kupakatwa na mahakama polisi na usalama wa Taifa iwe mwisho.
 
man we kweli ni jasiri! vp una maoni gani kuhusu masalia wa cdm? ungependa kuwaambia nini katika kipindi hiki kigumu wanachopitia? unamshauri nini zzk kuhusu kutegemea sangoma kuyalinda maisha yake?
 
.... Mdogo wangu Lema umeiona Arusha ilivyokuwa imetulia bila maandamano na kelele zisizo na msingi... Endeleza utulivu huu ambao naamini umejifunza kwa kipindi ulichokaa nje ya bunge....!
NARUDIA KWA HILI HONGERENI CHADEMA,HONGERA LEMA!!!

Kama kweli Lema ni mdogo wako kiumri. Na kazi na hoja zako ni hizi; bhasi umri ni jambo la kipuuzi sana kutumika katika kupima upeo na Uwezo wa mwanadamu.
 
Nnauye Jr

Hivi wewe kumbe huna upeo kabisa!!

Maneno gani ya kipuuzi haya eti Arusha imetulia, waliotulia ni kina nani? na waliompigia kura Lema ni kina nani?

Hiyo hongera ya kinafiki....Ikiulu imeshinda kuingilia kwani kulikuwa hakuna hoja yoyote ya maana ya kupora ushindi wa Lema!

Majaji nao wameanza kuona aibu kwa maamumuzi ya hovyo mnayowaagiza kuyafanaya!! wameona watende haki tu!

Haya sasa iagizeni tume yenu ya uchaguzi iitishe uchaguzi wa ubunge Igunga na S/wanga tukawafanye kitu mbaya!!
 
Last edited by a moderator:
pole Nape !pole CCM!
hatimaye ccm yazikwa rasmi arusha...!

attachment.php
 

Attachments

  • SAM_0553.JPG
    SAM_0553.JPG
    72.9 KB · Views: 431
Back
Top Bottom