Hongera kwenu 'single mothers' wote

nyani jike

Senior Member
Feb 23, 2016
176
223
Leo siku ya mtoto wa Afrika!Namshukuru Mwenyenzi Mungu kwa Neema aliyetujalia sisi waja wake sifa na shukrani kwako Mungu.Wamama wenzangu na mabinti wenzangu hongereni sana,sisi ni jeshi kubwa vita ni vikali lakini tunakuwa washindi Mungu yupo kati yetu.

Single mothers wote uzi huu ni kwa ajili yenu nawapongeza sana wamama wote wanaolea watoto wao wenyewe nafahamu changamoto mnazopitia kuwa mama na baba siyo kitu chepesi,kuwalisha,kuwasomesha,kuwapa malazi bora,kutunza afya zao,kuwa mlinzi,kuwa rafiki mwema na mwalimu kwa watoto wenu,kikubwa zaidi kulia huku unacheka na kutoa tabasamu siyo kitu rahisi.

Sitaki kujua sababu za kuwa single mother coz nazifahamu nyingi ila kiufupi wanawake wanaolea watoto wao na kupata all bills ni makomando,mwanamke huwa akimbii watoto wake.
 
1466056116682.jpg
 
Ila sisi wanaume ni mabazazi sometimes.
Hivi unapata wapi guts za kumkataa mwanao? Damu yako?
Ishu sii kumkataa mwanao, je unakua na uhakika gani kama mtoto ni wako, wenye uhakika na bado wakakataa hapo kuna tatizo lakini unajuaje na unakua na uhakika gani in the first place kua mimba ni yako na uwe responsible na malezi yake hadi mtoto?

Kwangu hiyo ndio naiona changamoto. Wanaume wanakataa watoto kwa sababu nyingi tu(ingawa sio watoto maana wanakua hawajazaliwa, wengi hukataa mimba), kuna sehemu ya kuwalaumu wao na kuna sehemu ya kuwalaumu wamama wa watoto.
 
Kapime DNA kama sio wako unamuacha.
 
Leo siku ya mtoto wa Afrika!Namshukuru Mwenyenzi Mungu kwa Neema aliyetujalia sisi waja wake sifa na shukrani kwako Mungu.Wamama wenzangu na mabinti wenzangu hongereni sana,sisi ni jeshi kubwa vita ni vikali lakini tunakuwa washindi Mungu yupo kati yetu.

Single mothers wote uzi huu ni kwa ajili yenu nawapongeza sana wamama wote wanaolea watoto wao wenyewe nafahamu changamoto mnazopitia kuwa mama na baba siyo kitu chepesi,kuwalisha,kuwasomesha,kuwapa malazi bora,kutunza afya zao,kuwa mlinzi,kuwa rafiki mwema na mwalimu kwa watoto wenu,kikubwa zaidi kulia huku unacheka na kutoa tabasamu siyo kitu rahisi.

Sitaki kujua sababu za kuwa single mother coz nazifahamu nyingi ila kiufupi wanawake wanaolea watoto wao na kupata all bills ni makomando,mwanamke huwa akimbii watoto wake.
Nakubaliana na wewe . Single mothers wanapitia mengi sana kwa kulea watoto wao kwa kweli wanastahili zaidi ya hongera
 
Huu mstari una uhusiano sana na sababu za baadhi ya wanawake kuwa single mother;

Mithali 21:9
Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
 
Pamoja na pongezi hizi Single mothers jifunzeni kutulia na wapenzi/waume zenu wapya kwani mnachukiza sana kwa vitendo vyenu vya kuendeleza mahusiano na wale waliowazalisha angali mshaolewa au kuingia mahusiano na wanaume wengine.
 
Back
Top Bottom