Hongera Kubenea kwa kupotezea uzinduzi wa hosteli za UDSM

Ni aibu lile koloni lao la kura tanga mjini pia wamelitupa kisa lipo chini ya upinzani na hajakanyaga tangu achaguliwe kama unawapenda sana wapinzani haya nenda tanga kawaulize wana shida gani maana wanadai fidia ya barabara na kipindi cha kampeni mliwaihidi kuwalipa mara moja sio ile ziara ya kizushi ya majaliwa kipindi cha msiba wa baba yake ummy mwalimu
 
Aaahhaa jamanii ...hatakama hakutaka kuonekana..mwishoo wake 2020 huyooo...wee kama mbungee hudhuriaa ujuee unaweka platfom ya kiungoziii....hayoo mambo ya kususia inamaana hujiamini kma mbungee....acheenii zenuu
Samahani naongezea kususa ni tabia za kike mkuu na utamkimbiaje mwanaume mwenzako.
 
Kwa akili hizi, Dar inarudi CCM 2020, na tusisikie visingizio vya "tumeibiwa".
Mburaaa,Wana Dar wanajielewaa vizur hata atoe nn hawaoni ndani, majumba karibu na reli yamebolewa,Chinga pale Karume wamefurushwa Kama nyau, mafisiem watapa ilala ndio kwao
 
Sasa Kubenea angesaidia nini awepo asiwepo mradi ushakamilika.
Tanzania siasa zetu za kitoto sana ndio maana tunapewa ahadi za kudanganywa wakati wa uchaguzi.
 
Huo ulikuwa mkutano Waccm. Yeye hakuhitaji kuhudhuria. Haukawii kusikia "ccm oyee!"
 
Tafuta yaliyo tokea kwenye uzinduzi wa kinyerezi 2 na uzidunzi wa daraja la kigamboni.
Magufuli Hana mahusiano mazuri si na wapinzani tu bali hata wana ccm wenzake, nadhani hata nje ya siasa atakuwa hivyo.
Na upinzani wana uhusiano mzuri na rais? Mheshimiwa rais ajapoteza kitu hata kama kubenea akuwepo kwenye hafla.
 
Hivi matatizo ya jimbo hutatuliwa kwenye uzinduzi tuu? Wakati mwangine rais hatekelezi matatizo ya raia wake ehhh nijibuni hapo kwanza!
Inamaana hujui kaza za mbunge ktk jimbo? Au unazani kazi zao niku-sign posho tu....? Kwa akili hizi ndo maana wanasiasa wanatuburuza.
 
na alikwenda mbali baada ya kuona kutokuwepo kwake aseme ooh nilitaka aje hapa aombe chochote anachotaka ili nimsaidie
Ha ha ha ana taka kumusaidia mbunge badala ya kuwasaidia wananchi,kama shida ilikuwa ni kumusaidia mbunge siamufuate nyumbani kwake.
 
Habari wanajamvi

Juzi kati wakati raisi wetu wa JMT akizindua hostel mpya za chuo kikuu,

Tulisikia kwa masikio yetu akimtafuta mbunge wa ubungo mh kubenea ili aje asalimie,
na alikwenda mbali baada ya kuona kutokuwepo kwake aseme ooh nilitaka aje hapa aombe chochote anachotaka ili nimsaidie

Kauli ya kujikosha haya mimi namsaidia mbunge jimbo ubungo lina matatizo ya maji,

labda nimpongeze mh kubenea kwa kupotezea ile ghafla maana inajulikana uwepo wake ingekuwa mbuzi wa kafara na kebehi ikiwezekana kuulizwa upinzani kama mbunge hostel mmechangia ngapi

Kama alivyodhalilishwa yule mbunge wa cuf kule kusini

Na ikumbukwe kuna siku mbunge alikwenda kuweka mambo sawa kiwanda cha urafiki matokeo yake tunayajua mkuu wa wilaya alifungua kesi ya kutukanwa bila ya msingi ili hali alikasirika tu uwepo wa mbunge

kwa hili la juzi nikupongeze

kinyelezi alishadhalilishwa mtu kwenye ufunguaji wa mitambo ya gesi

Zinduzi zote waachiwe wenyewe!

Nadhani ulipashwa umpe hongera ya kuwa Mtu wa hovyo hovyo na siyo kumpongeza kwa kitendo cha Kipumbavu kabisa alichokifanya. Hivi ni nani aliyekuambia kuwa katika umati ule wa Watu wote pale UDSM katika Uzinduzi ule wa Magufuli Hostels wote wale walikuwa ni wana CCM tu na kwamba mule kulikuwa hakuna Watu wa CHADEMA au CUF au TLP au ACT? Yaani Kubenea kafanya jambo lisilo na afya Kidemokrasia halafu bado tu tena ' Hopeless Creatures ' wengine humu mnamsifia na kumuona Shujaa pasipo hata kupima madhara yake katika Jicho la Kimaendeleo yatakuwaje.

Acheni tu Wazungu watucheke na watudharau kwa Upumbavu wetu wa Kiasili wa sisi Waafrika.
 
Mbunge wa Bukoba mh Lwakatare aliomba wananchi waondolewe kodi kwenye mabati ili yapate kwa bei nafuu itakayowasaidia kujijengea nyumba baada ya kuathiriwa na tetemeko,akajibiwa kuwa wajenge kiwanda chao hata wakiuziana mabati kwa shilingi 1000 sawa tu.
 
Nadhani ulipashwa umpe hongera ya kuwa Mtu wa hovyo hovyo na siyo kumpongeza kwa kitendo cha Kipumbavu kabisa alichokifanya. Hivi ni nani aliyekuambia kuwa katika umati ule wa Watu wote pale UDSM katika Uzinduzi ule wa Magufuli Hostels wote wale walikuwa ni wana CCM tu na kwamba mule kulikuwa hakuna Watu wa CHADEMA au CUF au TLP au ACT? Yaani Kubenea kafanya jambo lisilo na afya Kidemokrasia halafu bado tu tena ' Hopeless Creatures ' wengine humu mnamsifia na kumuona Shujaa pasipo hata kupima madhara yake katika Jicho la Kimaendeleo yatakuwaje.

Acheni tu Wazungu watucheke na watudharau kwa Upumbavu wetu wa Kiasili wa sisi Waafrika.
Kwani mh rais hajui matatizo ya wananchi mpaka aombwe na mbunge?huyo alikuwa anataka kutoa mipasho tu kwa Kubenea.
 
Kwani mh rais hajui matatizo ya wananchi mpaka aombwe na mbunge?huyo alikuwa anataka kutoa mipasho tu kwa Kubenea.

Naona umerudia tena upuuzi ule ule nilioukemea kama pepo hapo juu. Hivi Mkuu kichwani mwako hizo waya za kupeleka mawasiliano ya akili katika Ubongo wako ni nzima au zimezimika ghafla kusubiri matengenezo? Yaani Wewe unataka kutuambia kuwa Rais anaweza kujua 100% matatizo ya Wananchi wake kuliko ambavyo Mbunge husika anaweza kuyajua? Hivi unajua tofauti ya Kimajukumu kati ya Rais wa JMT na Mbunge wa JMT? Leo hii Rais akiyajua matatizo yote ya Wananchi wake je Kazi ya Mbunge itakuwa ni nini au uwepo wake Bungeni au pale Jimboni utakuwa na faida gani?

Enyi mnaojiita Wasomi wa Tanzania hebu muwe basi mnajitahidi saa zingine kutumia vizuri akili zenu kwani kuna wakati huwa nikiona comment ya Mtu ambaye anajiita kabisa Great Thinker humu JF lakini imejaa ' upupu ' mtupu huwa napatwa na wasiwasi mno na Elimu inayotolewa nchini Tanzania. Yaani kabisa Mtu mzima na mwenye akili zake anasema kuwa Rais anapashwa kujua matatizo ya kila Mwananchi wake huku akimtoa Mbunge ambaye logically na kiuhalisia tu yeye ndiyo kimbilio la kwanza la Wananchi kisha Mbunge ndiyo huyafikisha malalamiko au shida zao katika ngazi za juu ama kwa Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa na kwa Waziri husika na pia huweza kuitumia fursa hiyo hiyo pia ya kufikisha hayo malalamiko ya Wananchi wake kipitia Bungeni na Rais huyapata kiurahisi sana kupitia Wasaidizi wake.
 
Na upinzani wana uhusiano mzuri na rais? Mheshimiwa rais ajapoteza kitu hata kama kubenea akuwepo kwenye hafla.
Upanue akili zaidi ndugu yangu. Mbunge kutokuwepo kwasababu za rais kuhusiana vibaya, Mimi naona ni kupoteza. Katika hili rais ndo tatizo.
Nakusihi pia urejee uzinduzi wa week ya usalama pale Biafra kinondoni.
 
Back
Top Bottom