DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,127
Habari!
Nikiwa kama mtanzania ambaye nimezaliwa na kukulia kanda za nyanda za juu kusini sikuwahi fika kigoma, niliijua kigoma kwenye Ramani na mikoa ya Tanzania niliyofundishwa darasa la nne. Nilikuwa pia nikiisikia kigoma taswira ninayopata; kama wengi wetu ambao hatujafika tunavyopata taswira ya kigoma, kuwa ni mkoa/mjini ulio nyuma kwa kila kitu lakini binafsi nimegundua kweli kigoma ya sasa si ya zamani kama wasemavyo wao.
Nimefika kigoma takribani wiki moja sasa na nimeweza kutembelea maeneo yafuatayo; stand kuu, Mwasenga, Mwanga yote, ujiji hadi makumbusho ya Dr. Livingston, Bandari, station ya train, Lake Tanganyika Hotel nk. yafuatayo nimejifunza kinyume na nilivyotarajia;
1.Mji ni msafi sana na tulivu
2. Mji umepangwa vizuri, hata maeneo ambayo ni ya muda mrefu na yana nyumba za hali ya chini bado zipo kwa mpangilio tofauti na maeneo mengine.
3. Barabara za lami katikati ya mji zenye taa zinazofanyi mji kupendeza hasa wakati wa usiku.
4. Sijaona wapiga debe stand hivyo hakuna bughuza kama maeneo mengine.
Kwa ujumla mji ni mzuri kinyume na wengi tunavyodhani, changamoto kubwa ni kukosekana kwa miundombinu mizuri ya kuunganisha mkoa huu na mikoa mingine.