Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, aliyekuwa Mnadhimu wa Jeshi hilo Luteni Jenerali Abdulahman Shimbo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuvitaka vyama vya siasa kutokugomea matokeo ya uchaguzi kwa madai ya kulinda amani ya nchi.
Kauli ile ya Shimbo ilichukuliwa na wengi kama ya kisiasa na ya kibaguzi ambayo ililenga kuvididimiza vyama vingine na kuibeba CCM.
Ni ukweli usiopingika leo jeshi letu chini ya Jenerali Davis Mwamunyange kwa mara ya kwanza limekataa kujiingiza kwenye siasa za ushabiki wa vyama.
Ni matumaini yangu katika kipindi kilichobaki Jeshi la polisi chini ya IGP Mangu litatenda haki na kujitenga na ushabiki wa vyama kama ndugu zao wa JWTZ.
Asante Mwamunyange kwa mapenzi uliyonayo kwa nchi yako na hongera kwa JWTZ.