Hongera JWTZ kwa kujitenga na ushabiki wa vyama wakati wa uchaguzi

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, aliyekuwa Mnadhimu wa Jeshi hilo Luteni Jenerali Abdulahman Shimbo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuvitaka vyama vya siasa kutokugomea matokeo ya uchaguzi kwa madai ya kulinda amani ya nchi.

Kauli ile ya Shimbo ilichukuliwa na wengi kama ya kisiasa na ya kibaguzi ambayo ililenga kuvididimiza vyama vingine na kuibeba CCM.

Ni ukweli usiopingika leo jeshi letu chini ya Jenerali Davis Mwamunyange kwa mara ya kwanza limekataa kujiingiza kwenye siasa za ushabiki wa vyama.

Ni matumaini yangu katika kipindi kilichobaki Jeshi la polisi chini ya IGP Mangu litatenda haki na kujitenga na ushabiki wa vyama kama ndugu zao wa JWTZ.

Asante Mwamunyange kwa mapenzi uliyonayo kwa nchi yako na hongera kwa JWTZ.

Ww ukitaka kujua kama wanakuunga mkono, katalia kituoni uone.
 
Tatizo lako mleta maada hii hujui kitu, Shimbo kipindi kile alikuwa amekaimu madaraka ya mkuu wa majeshi tena huyu huyu Mwamnyange, so alikuwa na kofia mbili kipindi hicho;
1. Kaimu Mkuu wa Majeshi(Mkuu wa Majeshi maana mkubwa wake alikuwa nje ya nchi kikazi).
2. Mwenyekiti wa vyombo vya ulinzi na Usalama, na ndo maana mkuu wa polisi alikuwepo, mkurugenzi wa usalama taifa alikuwepo, mkui wa magereza alikuwepo(wakuu wote wa vyombo na usalama walikuwepo)nk.
So, alikuwa anafanya kazi na alitoa tamko hilo la kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani na utulivu. Sasa nini kosa yake? Ucha umburura huo ni wajibu wake kikatiba(Mkuu wa Majeshi/mwenyekiti wa vyombo vya usalama)kuhakikisha amani na utulivu nchini.
Asante kwa ufafanuzi mzuri, maana hawa chadema hawana akili wao kila siku wanawaza kufanya fujo tu, ngoja ipite 25/10 nadhani watajaza magereza. Maana mwenyekiti wao mjanja kajichukulia chake mapemana na sasa anahamisha tu hawa malofa wao wanaishia kupewa viroba tu
 
Kwa taarifa rasmi katika biashara ya siasa hakuna kumuamini mkuu yeyote yule ,hivi mnaijua siasa au ndio mmo mumo tu ? Mnajuaje kama na wao ni waumini wa upande fulani wa chama cha siasa ? Kura zitalindwa na wanachama wenyewe kwa njia wanazozijua wao na kuziamini ,hivi hawa mapolisi si ndio waliokimbia na masnadku ya kura kule Pemba ,mwaka huu maneno ya njiani yatabakia njiani haondoki mtu kwenye kituo kama kuzama na kutota basi kutaanzia hapo !
Sawa jeshi linaweza kuwa linaamini chama fulani lakini sio kujionyesha wazi, ndiyo maana tunalipongeza jeshi letu kwa kufuata maadili ya kijeshi.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri, maana hawa chadema hawana akili wao kila siku wanawaza kufanya fujo tu, ngoja ipite 25/10 nadhani watajaza magereza. Maana mwenyekiti wao mjanja kajichukulia chake mapemana na sasa anahamisha tu hawa malofa wao wanaishia kupewa viroba tu
Usikalili soma tena nilichoandika.
 
Wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, aliyekuwa Mnadhimu wa Jeshi hilo Luteni Jenerali Abdulahman Shimbo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuvitaka vyama vya siasa kutokugomea matokeo ya uchaguzi kwa madai ya kulinda amani ya nchi.

Kauli ile ya Shimbo ilichukuliwa na wengi kama ya kisiasa na ya kibaguzi ambayo ililenga kuvididimiza vyama vingine na kuibeba CCM.

Ni ukweli usiopingika leo jeshi letu chini ya Jenerali Davis Mwamunyange kwa mara ya kwanza limekataa kujiingiza kwenye siasa za ushabiki wa vyama.

Ni matumaini yangu katika kipindi kilichobaki Jeshi la polisi chini ya IGP Mangu litatenda haki na kujitenga na ushabiki wa vyama kama ndugu zao wa JWTZ.

Asante Mwamunyange kwa mapenzi uliyonayo kwa nchi yako na hongera kwa JWTZ.

Limekataa kwani limeambiwa na nani likakataa???Mbona ndivyo kanuni zao zinavyowaongoza kuwa.Hivi Chadema mtaacha lini kuhusisha Majeshi hususani USALAMA Kwenye propaganda zenu.Mna chuki na kila mtu.
 
Limekataa kwani limeambiwa na nani likakataa???Mbona ndivyo kanuni zao zinavyowaongoza kuwa.Hivi Chadema mtaacha lini kuhusisha Majeshi hususani USALAMA Kwenye propaganda zenu.Mna chuki na kila mtu.
Nano amelihusisha kulipongeza ni kulihusisha?
 
Uzi wa kinafiki.lini maji ya mazuri yakatokea kwenye kisima cha chumvi UKAWA
 
Nano amelihusisha kulipongeza ni kulihusisha?

Kwani ni nani kaliambia Jeshi lijiingize kwenye ushabiki wa vyama likakataa??Unaweza kumtaja alielitaka jeshi lijiingize kwenye ushabiki wa vyama na limemkatalia??Jamani mambo ya jeshi yaachiwe wanajeshi wenyewe.Ukikamatwa si Mbowe wala Lowassa watakaokuletea chai MAHABUSU.
 
Jaman ni usiku sasa umeenda mnoo gari la Matangazo linapita usiku huu et Watu wajitikeze kesho kinana atakua na Mtoto wa LOWASA akiongea na kupinga kua Baba ake HAFAI KUA RAIS!!!!

Ikumbukwe hapa ifakara CCM imekufa kitambo vijiji 33 CCM Ilipata vitatu tu na chadema kuzoa 30!

Mama Salma kahutubia hapa juzi hali ilikua mbaya watu wachache utazan wanavunja kikoba!!!!!!

Kuna tetes pia kuwa MKUU WA KAYA alikua na vikao vya siri siku ya jana hapa Ifakara!!!

Pia leo mji ulisimama kwa ujio wa lowassa hapa na wamepata Mshtuko mno!!!

Sasa huyo FREDRIC LOWASSA sijui nikwel kua atakuepo kumpinga BABA YAKE au ni Technique yakupata mafuriko kuficha aibu??????

Nakwann gari lipite sa saba hii kutangaza au waliogopa mawe kwan tumewachoka??????

Nitawapa update Makamanda!!
 
Hivi tujiulize lowasa mikutano inajaa at da same time maguful maguful inajaa same town and same city napata shaka na hii hali
 
Kwani ni nani kaliambia Jeshi lijiingize kwenye ushabiki wa vyama likakataa??Unaweza kumtaja alielitaka jeshi lijiingize kwenye ushabiki wa vyama na limemkatalia??Jamani mambo ya jeshi yaachiwe wanajeshi wenyewe.Ukikamatwa si Mbowe wala Lowassa watakaokuletea chai MAHABUSU.
Sidhani kama unajitambua pamoja na kutoa mfano ya 2010 nina wasiwasi kama umenielewa, sidhani kama jeshi ni wajinga kukamata kila mtu anayelipongeza.
 
Back
Top Bottom