Hongera Job Ndugai

Mkuu wanasiasa wote ni watu wa kuchukuliwa kwa tahadhari na kama ingewezekana wawe wanaongea chini ya viapo!!!!!!!!

Hao viapo hawavijali , huoni kila leo wanavyovunja kiapo cha kuiheshimu na kuilinda katiba ya JMT?

Hakika wanasiasa wanaweza wakawa ndiyo kundi la watu wanaoongoza kwa kuwa na laana ya kuvunja viapo.
 
ndugu yangu moja ni ngumu sana kwa sababu wazanzibari hawataki na wao nguvu yao kubwa kisiasaa,tanganyika ndio tunao wabembeleza ktk ndoa hii ya muungano,namnukuu baba wa taifa pale aliposema"ningekuwa na uwezo ningevisukuma mbali katika bahari ya hindi visiwa hivi kwani hawa watu laki 3 (wakati huo) watakuja kuwaumiza vichwa watu mil.12(wakati huo)wa tanganyika."
 

Kwa kauli hii anastahili pongezi. Huyu ni mzalendo na siyo shabiki wa chama.
 
Mtu anayevunja katiba aliyoapa kuilinda anachukuliwa hatua gani?
 
Bado naamini kuwa ili kupata Katiba bora itakayoweza kutuunganisha ni lazima iwe ya maridhiano, si kwa wingi au uchache wa waungaji mkono. Bado pia naamini kuwa si mfumo wa Serikali mbili au tatu utakaotatua kinachoitwa kero za muungano na hasa kama tutauchukua bila maridhiano ya pande zote. Bahati mbaya sana maridhiano haya yanaongozwa na wanasiasa, kwani matakwa ya kisiasa (political will) ndiyo kuu katika suala hili.

Kuyapata maridhiano ni lazima kutokane na kuaminiana kwa Wajumbe na mchakato ulio sahihi unaokubalika na pande zote. Nikiangalia jinsi mambo yanavyokwenda, hivi vyote havipo. Sijaona Wajumbe wakijadili hoja bali misimamo. Mchakato wenyewe unaonekana kupingwa na pande zote ikiwemo hasa ule wa msingi wa tunda wanalojadili huko Dodoma! Kama hawaamini mchakato wa tume ya Katiba (na Wajumbe wake kwa pamoja na binafsi) na tunda lake sijui watafikiaje maridhiano na hasa sijui wanachokifanya Dodoma. Tunaona mashindano ya kupata mshindi na mshindwa ndani na nje ya bunge. Hii ni bahati mbaya kweli kweli!

Misimamo ya makundi na hasa ya kivyama imevuruga sana mchakato huu. Imefanya Wajumbe na watu nje ya bunge kuhairisha kufikiri na kusimamia misimamo hii. Imani zimekuwa kwenye misimamo hii. Mjumbe anasimama na kuanza kwa kutamka yeye ni 'muumini wa dini' gani - mbili au tatu! Ukisikiliza hoja anazotoa unabaki kinywa wazi kama anaelewa maana ya mfumo anaouchagua.

Sijasikia mjumbe ambaye ameongelea kwa kina ni masuala gani ya muungano, ama ndani ya Serikali tatu au mbili yatauimarisha muungano wetu. Muungano umefikisha miaka 50 badala ya kuuimarisha kwa kuongoza mambo tunayoshughulikia na kusimamia kwa pamoja eti tunayapunguza na kujitapa kuwa tunaimarisha muungano!

Mungu atubariki, tupite salama.
 
...ni kweli katika hili swala la unafiki kutawala linaweza kupewa nafasi; lakini tukumbuke kwamba katika kundi la wapenda serikali 2 walioko humo si kwamba wote wameridhia au wanaunga mkono kwa matakwa yao; wako hivyo kwasababu ya mfumo tu, usije kushangaa na wengine wakajitokeza na kuanza kutoa kauli za style ya Job Ndugai, kwa mtu mwenye kufikiria Haki kuliko Dhuruma lazima aungane na wapenda Haki wenzake.
 
Hongera Mheshimiwa Job Ndugai kwa kuona mitazamo mikali ya wana Intarahamwe haitufikishi kokote. Ntarahamwe mwenzio Lukuvu kesha chafua hali ya hewa kule Zanzibar kwa kauli zake za kipumbavu kanisani na mjengoni.
 
Nina hakia tume ingetoa mapendekezo yanayolingana na chama tawala, sasa hivi wangekuwa wanalaumiwa na kudharauliwa na wapinzani...
 

Naungana pamoja na andiko lako kwa kiasi kikubwa umejikita zaidi kwenye majibu ya kutupatia katiba mpya kwani bila maridhiano hakuna katiba mpya.

Wabunge wanadhani misimamo itazaa katiba haiwezekani hata kidogo.kwani huwezi kuandika katiba ukiwa na upande wenye misimamo mikali kama ccm katiba haitapatikana.
 
Mpango wake wa urais umeyeyuka kama nailoni kwenye moto.

Yaani mkuu hapa duniani usipokuwa makini na ukashindwa kutumia akili vizuri utaumbuka mchana na historia itakukana.

Sitta alijenga heshima kupitia Uspika wa Bunge , na sasa Uenyekiti wa Bunge umemmaliza.Hana cha kujivunia tena.
 
 
Last edited by a moderator:

"........Wote waliompokea aliwapa uwezo kuwa wana........"
 
Nimerejea tena jukwaani ili tuendelee kupeana za hapa na pale kwa kadri ya mungu anavyotuongoza.awali ya yote nawashukuru tena wachangiaji wote na wasomaji wa jukwaa hili tuendelee kuelimishana na mwisho tupate katiba mpya.

Kwa mara nyingine tena niwakumbushe kuwa huu mchakato bila ukawa kurejea bungeni hakuna katiba mpya.kwa nini nimesema hivo ni kwasababu mh.waziri mkuu mizengo pinda amekifuraia kitendo cha ukawa kutoka bungeni hivyo nae amesema atatoka bungeni na kuzunguka kwa wananchi nchi nzima kama ukawa wanavyotarajia kufanya.
 
Yaani mkuu hapa duniani usipokuwa makini na ukashindwa kutumia akili vizuri utaumbuka mchana na historia itakukana.

Sitta alijenga heshima kupitia Uspika wa Bunge , na sasa Uenyekiti wa Bunge umemmaliza.Hana cha kujivunia tena.

Nafasi bado anayo kupitia ukawa kama amegundua mtego wake adandie hoja za ukawa tu basi.upepo unabadirika.
 
Job Ndugai bila shaka leo emekula pasaka kwa amani sana.usitusaliti endelea kuzungumza na chama chama ili misimamo ifutwe twende kwenye kura ya siri.
 
Hahaha@nuruyamnyonge hawa ccm siyo watu wa kuamini sana.wanahofu sana na serikali 3 wanaogopa maendeleo yatakuja kwa kasi af wananchi watawachukia mpaka kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…