Hongera Jeshi la Zimamoto kwa mikwara

Hongera Jeshi la Zimamoto kwa mikwara

Jasusi Mbobezi

Senior Member
Joined
May 17, 2020
Posts
194
Reaction score
851
Katika mambo yanayonifurahisha hapa duniani ni mazoezi ya utayari yanayofanywa na Jeshi la Zimamoto.

Yaani wanaenda sehemu kama airport wanawasha moto halafu wanajipigia simu wanakuja kuuzima kwa wakati, wengine wana act wamezimia, wanabebwa na kupewa huduma yakwanza.

Baada ya hapo wanaongea na vyombo vya habari kujisifia kwa kuwa tayari kudhibiti majanga muda wote, very funny [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Huwa mnanikumbusha kisa cha rafiki yangu mmoja aliyekuwa mtaalamu wa michezo ya karate, kila siku anatuonesha style za kupambana na adui siku moja akaingia kwenye 18 za muuza mkaa akachezea kichapo cha hatari, badae akatwambia maadili yao hayaruhusu kupigana hovyo ila anatwambia hivyo akiwa hoi[emoji23][emoji23][emoji23]

Sasa zimamoto nao kwenye mazoezi real wana sababu nyingi balaa mara barabara mara maji [emoji23][emoji23][emoji23] duuuh
 
Hawa wahuni tu, ingekuwa amri yangu ningewafuta kabisa, imagine kuna mtoto alizama kwenye bwawa karibu na mlimani city, wakaenda na magari yao, kufika pale wakaanza kupekecha maji na vijiti, jamaa mmoja raia akaona hawa wajinga, akajitosa majini akazama akamtafuta mtoto akaibuka naye.

Waziri wao wa mambo ya ndani wakati huo Nahodha wa Zanzibar akasema ingependeza wamuajiri yule jamaa aliyezama majini maana ilikuwa aibu kwa kikosi kizima cha fire
 
Hawa wahuni tu, ingekuwa amri yangu ningewafuta kabisa, imagine kuna mtoto alizama kwenye bwawa karibu na mlimani city, wakaenda na magari yao, kufika pale wakaanza kupekecha maji na vijiti, jamaa mmoja raia akaona hawa wajinga, akajitosa majini akazama akamtafuta mtoto akaibuka naye
Kati ya majeshi dhaifu ni hili la zimamoto. Linatakiwa kuokolewa kabla ya kuokoa mali za raia.
 
Baada ya hapo wanaongea na vyombo vya habari kujisifia kwa kuwa tayari kudhibiti majanga muda wote, very funny
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Yaani waache kabisa hizo sinema zao. 😡😡
 
Tuiondoe serikali ya ccm, siyo sikivu wapo kulinda tu maslahi yao,
Uza mavieite yote ya chama na serikali, nunua magari ya kisasa ya fire na ambulance peleka kila wilaya gari 5
Unataka kuiweka serikali ipi?,ikiwa wote ni binadamu na ni wale wale
 
Uliza bajet wizara upewa bei gani kwajili ya kununua vifaa vya kuzima moto na majanga, kuna vitongo viko vizuri kama kile cha kuzibiti wapinza kile kikovizu sana
 
Back
Top Bottom