Hongera Halotel

gabs2014

Member
Jan 27, 2014
93
62
Wadau, nimejaribu kufuatilia hili jambo kila niwekapo kifurushi katika mtandao wa Halotel salio la sms,mb na dk linaongezewa katika kifurushi cha sasa.
je wadau mmelingundua hili jambo?
 
Mi nimechukua laini yao ya University Offer... offer naona kibao. Na Offer zao zinaanza Tarehe 1
 
Hawa jamaa nao ni jipu.

TISS ifanye kazi yake wakati Mh. Majaliwa akiandaa mikasi na plasta.
 
Mkuu promo ya nn tenaa!! kama vifurushi vipo tuoneshe kwa screenshot au tuandikie poa tuu swala si kujua kilichokuvutia mpaka ukatoa pongezi kwa Halotel... tujuze na sis tuamie kama kuna neema
 
Hawafuati taratibu za kazi.
Haieleweki anayewapa kiburi ni nani.

Hii kampuni ililetwa wakati ule wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais
na inasemekana walitoa fedha nyingi kwa mmoja kati ya wagombea wa ccm na ndio wakaletwa kufunga mitambo yao haraka haraka na bila kufuata utaratibu!! Sasa yule aliyewaleta alishindwa na hawana godfather tena hivyo wanatapatapa!! Yule engineer Natty wa Kinondoni anaweza kueleza nani aliwaamuru wafunge mitambo hovyo hovyo wilaya ya Kinondoni!!
 
Hii kampuni ililetwa wakati ule wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais
na inasemekana walitoa fedha nyingi kwa mmoja kati ya wagombea wa ccm na ndio wakaletwa kufunga mitambo yao haraka haraka na bila kufuata utaratibu!! Sasa yule aliyewaleta alishindwa na hawana godfather tena hivyo wanatapatapa!! Yule engineer Natty wa Kinondoni anaweza kueleza nani aliwaamuru wafunge mitambo hovyo hovyo wilaya ya Kinondoni!!
Mie nadhan ni speculations tu...kampuni inamilikiwa na jeshi la vietinam...kwa maono yangu katika miaka mitatu ijayo pengine hii kampun itasumbua sana kampun zingine za simu. Jamaa wanamtaji wa kutosha with latest technology...imewachukua muda mfupi sana kuwekeza kwenye almost kona zote za nchi hii...mie nadhan tuwape muda....
 
Mkuu @Bulesi, kila mtu anaongea la kwake.

Nadhani wahusika wakifuatilia itajulikana hili jipu ni la aina gani na limekaa eneo gani.
 
Mkuu @MR UNINFORMED, haukukosea kujipa hiyo ID. Aliyekwambia hawa Viettel wanatumia latest technology ni nani? Hii tabia ya Watanzania kuongea vitu tusivyovijua kama vile tunavijua tuliitoa wapi?

Njia inayotumiwa kuunga cable na hawa jamaa Ulaya ilishasahaulika na haitumiki tena.

Voda na tiGo watu wanadai ya kwao kidogo ina unafuu japo sijajionea.

Kama haujui kitu uliza usiwe unaandika usiyoyajua.
 
wadau niliombwa screen shoot, nimeileta nimejiunga kifurushi leo ambapo nilikuwa na salio la data,msg na dk ambavyo vimejumuishwa katika kifurushi kipya.
 

Attachments

  • IMG_20151228_213223.jpg
    IMG_20151228_213223.jpg
    12.7 KB · Views: 28
wadau niliombwa screen shoot, nimeileta nimejiunga kifurushi leo ambapo nilikuwa na salio la data,msg na dk ambavyo vimejumuishwa katika kifurushi kipya. IMG_20151228_213223.jpg
 
Back
Top Bottom