Egwugu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,558
- 8,551
Wasalaam Watanzania nyote.
Leo nina jambo moja la kumhusu huyu Mh.Mbunge wa jimbo la Misenyi Nampongeza sana huyu mzee.
Kwanza niseme wazi, (mie sina chama) ila ninao utashi tu wa kumuangalia mtu mmoja mmoja kwa kadili ya matendo yake na hasa katika nafasi yake. Binafsi naamini kabisa approach yangu hii inanisaidia sana, nakuwa huru mda wote kupongeza na kusifia yeyote yule ama kukosoa na kamwe sibanwi na mipaka ya vyama "vyao".
Tokea uchaguzi umalizike na huyu mzee kuibuka kidedea, kuusema ukweli pasipo kuuma maneno na wala kumuonea mwingine, huyu mh. kweli ni kati ya wabunge wachache sana kutoka CCM na hata upinzani wanaoifanya kazi yao. Na hata staili yake anayoitumia ya kelele kidogo na matendo mengi a.k.a mzee wa kimya kimya iko safi sana.
Hadi kufikia leo, ni mbunge pekee kutoka mkoa wa Kagera aliyeweza kulizunguka jimbo lake kwa zaidi ya mara tatu.
Nimesoma na kuzidi kumfatilia baada ya kuvutiwa sana na anavyokuwa karibu na wanajimbo wake, huyu mzee anastahili pongezi hata kama hana anachowapa. Ninajiuliza kwa wapinzani, achana na mizigo ya CCM ambayo tumeshaizoea, ni kwanini wa upinzani walio wengi hawana spirit ya kutumikia vyeo vyao zaidi ya kuonekana wako busy na kuratibu maandamano kana kwamba waligraduate katika kuandaa maandamano
Kwa wapinzani na Lwakatare akiwemo, wanatakiwa kuelewa mahitaji ya jamii za watu wao na mahitaji yao, bora liende na mob politics havitawasaidia kamwe. Nendeni majimboni mkafanye kama Nassari a.k.a dogo janja, nendeni mkafanye kama Prof. Muhongo, fanyeni kama Dr. Diodorous Kamara. Mkitaka kuendelea kuwa wauza sura mijini mtambue 2020 siyo mbali na watanzania hawatasita kuchukua maamuzi "sahihi".
Atakaye mwona Mh. Mbunge huyu naomba ampe salaam zangu nyingi.