Hongera CCM

Shonza

unapenda sana kuchuma mboga, haya basi njoo huku bonde la msimbazi la sukita uje uchume mchicha ukichelewa kuja, basi mchicha utakomaa na kuwa mkubwa kama mbuyu.
 

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanikiwa kunasa siri za mipango ya hujuma zilizokuwa zimeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne za Jiji la Arusha, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika, zimebainisha kuwa CHADEMA katika uchaguzi huo kilifanikiwa kushinda kata hizo baada ya kuvunja ngome ya CCM iliyokuwa ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
Kwa mujibu wa habari hizo, mipango karibu yote iliyokuwa ikifanywa na CCM, ikiwemo halali na haramu, ilivuja na kufika mikononi mwa wapinzani wao ndani ya muda mfupi hata kabla ya utekelezaji.
Imedaiwa kwamba baadhi ya watu waliokuwa katika kambi ya CCM, waliamua kwa siri kufichua mipango hiyo na kuifikisha kwa mahasimu wao kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa kushiriki katika mambo ya kidhalimu.
Habari zinasema maofisa kadhaa wa CCM ambao wamekuwa wakiratibu na kusimamia mipango karibu yote miovu dhidi ya wapinzani, waliamua kwenda kinyume na makubaliano hayo, na kwa njia ya siri wakafanikiwa kutoa mpango mzima hadharani.
Mmoja wa maofisa wa CHADEMA ambaye awali alikana taarifa hizo, kabla ya kukiri baada ya kubanwa, amedai zilifikishwa kwao na watu wenye mapenzi mema na nchi.
“Hata nasi awali tulishangaa, lakini tulilazimika kuziamini baada ya kuzifanyia kazi na kubaini kwamba zilikuwa za kweli.
“Kwa mfano taarifa za kuwepo kwa mipango ya kutumbukiza kura bandia, kununua shahada za kupigia kura ilivuja mapema nasi tukaamua kuweka mitego kila mahali tulipoambiwa, kiasi cha kuwafanya washindwe kutimiza lengo lao,” alisema ofisa huyo.
Habari zimezidi kufichua kuwa, kambi hiyo ya CCM ilianza kuyeyuka mapema mchana wa Jumapili, siku ambayo ilikuwa ya uchaguzi, baada ya kuhisi kuwa mambo yao yamekwama kutokana na viongozi na vijana wao kuonekana katika maeneo yote muhimu yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho tawala kuendesha hujuma zake.
Chanzo kimoja cha habari cha kuaminika kimeliambia Tanzania Daima kuwa ‘usaliti’ huo wa baadhi ya watendaji wa chama hicho tawala umetokana na kutopendezwa na mtindo wa utendaji kazi za kisiasa unavyoendeshwa na Mwigulu na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho tawala.
“Wameanza kuchoshwa na siasa za majitaka ambazo zimezidi kulichafua taifa na kuangamiza maisha ya watu.
“Ni kweli tunataka ushindi, lakini wengi hawataki utokane na kuumiza watu ambao wana haki ya kuunga mkono na kufuata chama wanachotaka,” kimesema chanzo hicho, ambacho kimeomba jina lake lisitajwe kutokana na sababu za kiusalama.
Mbali na sababu hizo, taarifa zimebainisha kuwa sababu nyingine zilizowafikisha baadhi ya watendaji wa CCM kusaliti, ni kasi ya CHADEMA kuungwa mkono na wananchi, pamoja na vitisho, na vitendo vingi vya ukatili ambavyo viongozi na wanachama wa chama hicho pinzani wamekumbana navyo.
Hadi sasa, viongozi wakuu wote wa CHADEMA wameonja adha ya polisi kwa kukamatwa, wengine kupigwa na hata kufikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali.
“Tunao wanachama waaminifu ambao wamo ndani ya CCM na wamekuwa sehemu muhimu ya intelijensia ya chama chetu,” - Wakiwemo bibie JULIANA SHONZA na MTELA MWAMPAMBA.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
CHADEMA wanasa siri za CCM
• Wapenya ngome ya Mwigulu

na Mwandishi wetu


[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff, align: center"] <a href="http://adserver.adtech.de/adlink/3.0/1332/4486816/0/357/ADTECH;loc=300" target="_blank"><img src="http://adserver.adtech.de/adserv/3.0/1332/4486816/0/357/ADTECH;loc=300" border="0" width="200" height="600"></a> [/TD]
[/TD]
 
Kwa haya mawazo yako ccm itakuwa kama matembele sio mchicha....lakini endelea hivyo hivyo kuiua ccm....unarahisisha kazi ya mageuzi...utakumbukwa kwa kuipigia debe CDM wakati upo CCM...
 

[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]

Yeah sweety nimegundua uko makini na unasoma mstari kwa mstari huyo mwenzio ndo ameshafika hapo anajiona yuko mbinguni.
 
Si kujua wewe ndivyo ulivyo! Unaweza kulinganisha CCM na CDM kama vile mchicha na mbuyu!! Ingekuwa opposit hapo ningekuelewa. Mungu wangu, nikiona post zako sitakuwa na muda wa kusoma tena....:help:
 
kwanza wewe ni muongo kama ungetaka japo kuaminika kidogo ungeandika takwimu sasa za uchaguzi wa mwanzo CHADEMA ilipata viti sita na sio vinne kama unavyopotosha,CDM ilishinda SENGEREMA,ISEKE,DONGOBESH,BASHINETI,IFAKARA NA IYELA MBEYA .

Ile kata ya SENGEREMA kwa fisadi NGELEJA inaitwa NYAMPULUKANO!
 
Shida ya watu wa magamba na makada wao hata hesabu rahisi tu hawajui. Kata zinazozungumziwa na Shonza si sahihi kuwa waliongoza. Ikumbukwe katika kata CDM ilishinda ni pamoja na kata mbili au tatu zilizokuwa chini yao. Hivyo katika duru ya tar 16 Juni CDM walipata ushindi kwa kuwanyang'anya magamba kata zao. Lugha hapa walitetea 14 na kupokonywa 2. Ndio maana tunaomba improvement kwenye shule za kata wanakotokea hawa wajue hata hesabu na michanganuo ya matokeo kwenye chaguzi zetu.
Shonza, Mwampamba, Mwigulu, Nape hoyeeeeee! Peopleeeesssss Powerrrr!
 
Juliana masahihisho baada ya uchaguzi wa kata zote 26 nchi nzima CCM wamepata kata 16 hii ikiwa ni kupoteza kata zaidi ya 6 ( 4-Arusha, 1-Kilombero, 1-Mbeya na zingine sikumbuki), CHADEMA kata 10 hii ikiwa ni ongezeko la kata 8!
 
Dogo haijui CCM vizuri hana takwimu za CCM...moyoni bado anaiwaza CHADEMA, anaiongelea CDM kila siku anyway
 

asante
 
Ata uku ccm hatukutaki ww na mwenzako mnatuaribia chama chetu..kwa taarifa yako kuna vikao vinaanza kuwatimua tunaisi mmetumwa nyie kuaribu chama chetu
 
Dada angu kipenzi sio, kata 8 cdm wamepata jumla ya kata 10, ba nyie ccm kata 16
, nilikuwa nakusahihisha tu,
 
Tunashukuru sana "Kamanda"Juliana leo umemtoa FAIZA FOXY kutoka TORA BORA karibu FF ukifungua tu lazima nikupatie KINANA BARIIIIDI! Ni kweli kabisa SHOKA MOJA MBUYU CHINIIIIIII... LOL

 
Kwako Juli,

Salam saana ama baada ya salam mimi sijambo. kusudi la maandiko haya ni kukumbusha kuwa mi bado nakupenda.

1. Napenda mikono yako na vidole vyako unapopika, si unapokaa mbele ya pentium 2 na kuandika utumbo
2. Napenda midomo yako unapokuwa unaongea na mimi si unapozungumza yasiyo na maana kwenye mikutano ya CCM
3. Napenda miguu yako unapokuwa unatembea chumbani si pale unapokimbia huko na huko kutetea wala rushwa na mafisadi.
4. Naupenda mwili wako unapotumika kwa ajili yangu na si pale unapomuachia Savimbi autumie ..... aaaghh .... kinyaaa
5. Nakupenda ukiwa umevaa zile nguo tulizonunua pale Woolworth na si hayo ma-uniform ya wakoloni weusi, walioamua kwa nguvu kujimilikisha nchi hii.

Nakuomba ukumbuke upendo wako wa kwanza. Ninao uwezo wa kukuhudumia kwa hiyo nakusihi uache kufurahi pesa zilizonyang'anywa wale maskini kule vijijini na hata mijini. Njoo tule pesa zetu tunazotolea jasho na kulipa kodi.

Ingawa umeamua kushikana mikono na Savimbi mimi bado nakupenda, nimemwambia na nanihii anifikishie ujumbe huu kwako kwani nasikia siku hizi umekuwa kiguu na njia kuranda huko na huko kurubuni vijana kwa pesa za richmonduli ambayo mwanzo ilituuma sana mimi na wewe.

Karibu mupenzi mimi nakupenda
 

thi is an insult to CCM, ina maana CCM ndio iko level ya mchicha arusha??? wakati tunafahamu kwamba chadema ni chama cha juzi tu??

tafahali sana naomba usidharau chama kikongwe kuliko vyote cha siasa nchini na arusha imeshawahi kutoa wabunge wengi tu wa ccm

labda useme mnara wa babeli umeporomoka, lakini kuifananisha ccm na mchicha arusha ni matusi ya nguoni na dhihaka kubwa kwa wanaccm wote wa arusha na tanzania kwa ujumla including mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mh. Jakaya M Kikwete
 
Dah huyu ndiye Juliana ambaye mwenyekiti wa chama alimpokea pale Dodoma,maskini chama changu.....katika mchezo wa karata kuna karata flani huitwa sijui garasa ama gharasa amh apa chama changu kilil:help:amba garasa/gharasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…